PatPending
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 491
- 101
Mkuu Mag3 na wengineo, takwimu ulizoweka hapa zinadhihirisha kitu kimoja kikubwa ambacho ni kwamba upinzani bado una kazi ya ziada ili kuweza kupenya katika jimbo la Igunga na Tabora kwa ujumla. Badala ya kupoteza muda kuwarihisishia CCM kazi ya kuvipaka matope CUF, CHADEMA, NCCR na wengineo, kwa nini msiweke tofauti zenu kando ?
Ni imani yangu kwamba hakuna chama cha upinzani kitakachoweza kuin'goa CCM madarakani peke yake. Ni vyema tofauti na vijembe visivyo na tija viwekwe pembeni na nguvu zikaunganishwa kuweza kuwashinda hawa watawala wa sasa.
Lengo la vyama vyote vya siasa (ikiwemo CCM yenyewe) ni sharti liwe moja, kuongoza taifa katika dira mbadala na hii ya CCM ambayo imeleta miaka 50 ya majuto.