Great thinkers hii habari siyo ya kweli, binafsi nipo igunga na nilihudhuria mdahalo, na haya ndio matatizo ya hawa CCM B kwa sababu hawana stragegy zaidi ya kurembua kwa mabosi wao, kwanza kabisa ni kichekesho wakati halmashauri inakashfa kibao za mabilioni ya pesa za wananchi, ikiwemo taarifa ya mdhibiti mkuu wa mahesabu iliyowekwa pale wazi, eti watu wanazungumzia shilingi milioni 16 ambazo hata hivyo mgombea wa chadema alikuja kumjulisha mpaka balance iliyobaki na kwamba utendaji wake huo ndio uliompa cheo. tatizo CUF hawajipangi na wanaonekana wazi tatizo lao ni wivu kwa chadema, jamani hii taarifa ni kichekesho mimi ni mwandishi niliyeko huku na kwa bahati nzuri nimesikia tangazo kwamba mdahalo huo utarushwa leo saa tatu mpaka tano usiku star tv angalieni muone, kijana wa cuf sio mbaya lakini sio mzuri kiasi hicho na hilo wanalosema sio kweli.