CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni

Nilishangaa nilipowekewa pesa kwenye CRDB Account na mi nizichukue huku (MAlaysia)
Nikajua kahela kenyewe ka ngama nakuwa naenda ATM kila ninapohitaji, zikatoka poa tuu baada ya kutoa mara mbili tatu naambiwa BAlance haitoshi mhhh nikashtuka
Kuuliza nikaambiwa gharama ya kutumia hii card inakata Malaysian Ringit 140 (USD 40) kwa kila unapotumia hii card hata kwa kuangalia Balance.
Duuuuuh niliishiwa nguvu si unajua dola 40 kwa mwanafunzi tena nyingi sana hizo, Nikaiweka kabatini na siitumii tena.
 
Nilishangaa nilipowekewa pesa kwenye CRDB Account na mi nizichukue huku (MAlaysia)
Nikajua kahela kenyewe ka ngama nakuwa naenda ATM kila ninapohitaji, zikatoka poa tuu baada ya kutoa mara mbili tatu naambiwa BAlance haitoshi mhhh nikashtuka
Kuuliza nikaambiwa gharama ya kutumia hii card inakata Malaysian Ringit 140 (USD 40) kwa kila unapotumia hii card hata kwa kuangalia Balance.
Duuuuuh niliishiwa nguvu si unajua dola 40 kwa mwanafunzi tena nyingi sana hizo, Nikaiweka kabatini na siitumii tena.

Pole sana mtu wangu ...

Kwa wale washabiki wa kupenda vya nyumbani, utashangaa huyu mwenzetu akipunguza kuvipenda?
 
Ila ukiwa Bongo ukilinganisha CRDB na benki zingine kubwa zenye mtandao mkubwa mikoani na walayani kama NBC na NMB bado nakiri CRDB wana unafuu!

Hivi ulishaenda NBC Co-oporate uangalia huduma? Unakuta wateja 300 na madirisha mawili tu yanafanya kazi! Na NMB yaani foleni balaa!

Mie mteja wa CRDB na NBC...ila kwa huduma pamoja na matatizo yote haya CRDB ni bora zaidi!
 
Hoja hii ilijadiliwa muda mrefu uliopita nadhani hoja ya mwisho ilitolewa Machi 2009, Na mimi ni mara ya kwanza kuingia katika jamvi hili la JF, nilifuatilia thread hii kwa makini sana,
Sasa na nina mpango wa kutafuta visa card ili niitumie kwenye mtandao maana kuna programu moja ambayo iko mtandao ambayo natakiwa kuinunua na gharama yake ni Dola takribani $90. Na jinsi ya kuipata au kui-dwnload inatakiwa nitumie Visa Card. Lakini kabla ya wazo hilo la Visa card nikaamua kutembea Jamvi hili na ndipo nikafanikiwa kuona mjadala huu.
Kwa kuwa wazo langu la kupata programu hiyo liko palepale, Nakusudia kuwa na kadi mbili, moja ni kwa ajili ya kuhifadhi tushilingi twangu na nyingine iwe maalumu kwa mtandao. Kwa mfano katika kadi hii ya mtandao naweka kiasi kile tu kinachohitajika katika manunuzi yangu.
Maswali: Je hawa CRDB bado kuna kale kamchezo kama ilivyochangiwa na wanaJF mbalimbali? hasa kuhusu usumbufu wa kupata statement.
Na wizi wa pesa mtandaoni bado haujadhibitiwa?
Na je kuna marekebisho yoyote yaliyofanyika na CRDB kuhusu kale kamkataba ka kuiruhusu card itumike kwenye mtandaoni?

Waheshimiwa naomba kutoa hoja,
 
Mbona mwanzilishaji wa mada hii ana mambo ya kizamani, every who engages in having a visa card with is online active should expect to encounter such risk. cha msingi ni kujua what are the risks involved basi and the be careful. another important factor is to know the safe sites on the internet. Stop being a bigot and embrace technology.
 
Ndugu ni kitu gani hicho unachotaka kununua ambacho tanzania hakuna ? Naomba unifahamishe naweza kukuelekeza duka wanalouza au kampuni inayo deal na programu hiyo

ahsante
 
Ni programu ya music inaitwa Notation Composer Software, nadhani wale wanaofahamu mambo ya do re mi fa so la ti do wanafahamu, kama wana taarifa zaidi au wapi inapatikana wanijulishe
 
Mbona mwanzilishaji wa mada hii ana mambo ya kizamani, every who engages in having a visa card with is online active should expect to encounter such risk. cha msingi ni kujua what are the risks involved basi and the be careful. another important factor is to know the safe sites on the internet. Stop being a bigot and embrace technology.

Asante kwa mchango wako mzuri, na hongera kwa kufanikiwa ku-embrace technology. Sisi wengine utatusamehe, upeo mdogo.

Bigot maana yake ni nini tena?

Anyways, mimi nilidhani tulichojaribu kufanya hapa ni kuwaambia watu "what are the risks involved basi". Kama unadhani hilo ni kosa, basi samahani. Tungeomba labda utuelekeze njia ambazo watu wanaweza kutumia kutambua hizo risks involved.
 
Last edited:
Nashukuru, kunipa hiyo link, tatizo langu ni jinsi ya kuinunua ili niweze kuitumia kwa muda mrefu nitakao. Programu nilishai-download trial version ya siku 30, ambazo tayari zilisha-expire. na nikijaribu mara ya pili inagoma mpaka niinunue. na gharama yake ni USD 87.99.
 
Nashukuru, kunipa hiyo link, tatizo langu ni jinsi ya kuinunua ili niweze kuitumia kwa muda mrefu nitakao. Programu nilishai-download trial version ya siku 30, ambazo tayari zilisha-expire. na nikijaribu mara ya pili inagoma mpaka niinunue. na gharama yake ni USD 87.99.
Niliyoweka hapo sijawahi kuitumia. Hata hivyo, ni matarajio yangu kwamba utaweza kuitumia kwa zaidi ya siku 30.

Nimeeleza kidogo (post no. 443) kuwataka watu wachukue tahadhari pale wanapo-install software za namna hii from unknown sources.
 
Kama una CRDB Visa Card, na ulikuwa unafikiria kuitumia kwenye internet, basi usithubutu kutia sahihi kuiwezesha kutumika mtandaoni (ila kama tu unajua unachokifanya).

CRDB wametoa card mpya zenye nembo ya visa, ambayo wanatangaza kwamba unaweza kununulia vitu mtandaoni. Inaonekana kama ni bonge la wazo mpaka pale utakapogundua jinsi gani zisivyo salama hata kiduchu.

Mtu yeyote mwenye namba ya kadi yako, pamoja na vile vinamba vitatu vya "usalama" vilivyo nyuma, anaweza kuitumia hiyo kadi yako kwenye mtandao bila tatizo lolote. Kwa hiyo ukiitumia kwenye tovuti ambayo si salama, basi ni kama umegawa namba yako kwa watu wengine kujihudumia.

Pia ukiisahau kadi yako mezani, na mtu/rafiki yako/mtoto wako mtukutu/mpenzi wako/secretary wako akapata mda wa kunakili pembeni hizo namba zako, basi pia inakuwa imekula kwako.

Kama ulikuwa unafikiria ile pin yako, basi sahau maana haina kazi kwenye mtandao.

Address Verification
Unaweza ukawa unajiuliza mbona kuna watumiaji wengi tu wa credit cards duniani na wasiwe na wasiwasi hivyo?

Moja ya njia ambayo huwa inatumika kupunguza wizi wa kutumia kadi za wengine ni kufanya uhakiki wa anuani. Kiasi kwamba mtu akiweka oda ya kitu basi oda yake itakubaliwa na kadi kutumika ikiwa tu anuani ya ambapo vitu vya kwenye oda hiyo vitatumwa ni sawa na anuani ya mwenye kadi.

Kwa CRDB hii feature wameifinya, kiasi kwamba mtu yeyote duniani anaweza kutumia kadi yako na kununua na kutuma vitu vyake sehemu yoyote duniani anavyotaka.

Paypal
Kutumia site kama www.paypal.com inaweza kusaidia kuondoa uwezekano wa mtu kukuibia namba za kadi yako online.

Kujiunga kadi yako na paypal sio tatizo, tatizo ni jinsi ya paypal kuihakiki kwamba kweli ni ya kwako.

Paypal wanachofanya ni kukuchaji fedha kidogo (wastani wa 2,000TZS), halafa katika muamala huo wanaweka namba ya siri fulani. Sasa wewe inabidi uangalie statement yako kutoka benki, uione hiyo namba, halafu uwape paypal. Assumption hapo ni kwamba hakuna mtu mwingine anaweza kuona statement yako zaidi ya wewe.

Sasa ndani ya paypal unaweza ukakamilisha taratibu. Ukija CRDB ili kupata tu details za hiyo transaction, jasho litakutoka. Inaweza ukadhani ni kitu simple tu kupata details za transaction (hata mimi nilifikiria hivyo), lakini amini usiamini utashangazwa :) ... Nimefanya si chini ya trip 10 kwenda CRDB kwa ishu hiii, usihesabu simu, na nimetoka kupiga nyingine sasa hivi ... lol ...

Ningetakiwa niwe nimeshakata tamaa ila tu nataka tu nifuatilie mpaka mwisho waniambie inawezekana au haiwezekani.

Ila kama huu ndio utaratibu, sioni ni jinsi gani wataweza kuwahudumia wateja hata 100 tu wanaotaka kujiunga na paypal. Achilia mbali kwamba hawa watu 100 inabidi wapige kwata CRDB more that 10 times, halafu wawe wanapiga simu mara kwa mara kuwakumbushia CRDB case zao. Na mara nyingi watu unaoongea nao CRDB hata hawaelewi unazungumzia nini.

Makubaliano yako na CRDB ni soo
Ili kuiruhusu kadi yako kutumika online, itabidi utie saini makubaliano yako na CRDB, ambayo yanavipengele ambavyo vinaiondolea CRDB jukumu lolote la kukuhakikishia usalama wako unpotumia kadi yako kwenye mtandao. Kwa hiyo ukiwa online na kadi yako, jua you are on your own.

Kwa watumiaji wengine duniani kuna taratibu za jinsi ya mtu kupinga kuchajiwa transaction ambazo hujazifanya wewe. Na kuna taratibu za jinsi gani utarudishiwa pesa zako.

Mpkataba wa CRDB hauoneshi kama kuna kitu kama hicho. Kwa hiyo mtu akipata details za kadi yako, siku zote itakuwa inakula upande wako.

Kwa hiyo baada ya kuutia saini tu nimehakikisha kadi yangu haiondoki machoni pangu, na pia nahakikisha akaunti hiyo ya CRDB haina vijisenti vingi ... mpaka ntakapomaliza hii exercise. :)

Hitimisho
Sasa hivi unaweza kutumia kadi yako ya CRDB kwenye mtandao, lakini you do it at your own risk, tena risk kubwa tu.

Kinachonitisha ni kwamba kama kadi yako imewezeshwa kutumika kwenye internet, mtu hana haja ya kukuibia kadi nzima kwa sababu utashtuka, utaripoti, na kadi itafungwa. Anachotakiwa kufanya ni kupata namba za kadi zilizopo mbele, na vile vijinamba vitatu vilivyopo nyuma ya kadi, na inakula upande wako kimya kimya.

Kama umeiwezesha kadi yako kutumika kwenye mtandao, na kama vijinsenti vyako kwenye akaunti yako sio vidogo, na kama huwezi kuitunza details za kadi kiasi hicho, ni vyema ungewaambia waizibe isitumike kwenye mtandao ... or u may have to learn the hard way.

Mkuu,

Ahsante kwa maelezo yako ambayo kidogo yamenipa mwanga kuona kwamba bado Tanzania hakuna mfumo wa maana wa ulipaji fwedha mtandaoni au electronic payment system kama unavyojulikana.

Kwa sisi tulio nje ya Tanzania si tu kwamba tumezoea mfumo huu, bali pia hata aina zingine za malipo kama mobile payments, digital payments, e-cash na e-cheques.

Wafanyabiashara wote duniani wakiwemo mabenki ambao hutumia electronic payment system katika internet wanaitwa merchants na wako liable kwa wale watoaji wa kadi hizo zenye nembo ya VISA na MASTERCARD.

Mara nyingi wakishindwa kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa basi hutumia third parties kama PayPal na kadhalika ambao kumalizia taratibu zote za malipo kwenye internet kwa niaba ya mteja, hawa wanaitwa Payment Service Providers.

CVN (card verification number)

"Merchants" wote wakiwemo CRDB ni lazima wazingatie kanuni na taratibu zote za kuhakikisha kwamba malipo yanayofanywa na mwenye kadi ni kutoka kwake yeye mwenye kadi.

Hii ni pamoja na kuweka security protocal ( hapa kuna mambo mengi kama CGI au (common gateway interface) na hatua zingine za kuhakikisha kadi inatoka mahala sahihi vikiwemo certificate of authorization na mfumo wa PKI au public key infrastructure ambao unatoa kinga kwa kila transaction inayofanyika kwenye internet.

Ikiwa CRDB bado hawajafanya hivi basi huu ni ujinga wa hali ya juu.

Njia ya pekee kwa sasa ambayo ni salama ni kwa watu kutumia PayPal kwa any transaction.

Halafu mkuu umeongelea juu ya kufananisha anuani ya mteja anaefanya transaction online kama inafanana na anuani ambayo imo katika kadi ya mteja. Kama CRDB wameminya kama unavyosema huu ni uvunjwaji wa kanuni za kibenki na kibiashara labda kama mpaka sasa Tanzania hatuna public address systems ambapo mtu anaweza kupata mzigo wake baada ya kuununua.

Public address system ni rahisi sana kuiunda endapo pana nia ya kufanya hivyo na uundwaji wake unaweza kuchukuliwa simple tu kwa kuangalia motherboard ya computer jinsi ilivyoundwa, na hii ndio utapata system nzuri ya kutuma na kupokea barua na mizigo.
 
Last edited:
Kutumia card ya CRDB kwenye mtandao ni wazo zuri. Na CRDB inabidi wapongezwe kwa hatu hiyo.

Ninachosema hapa ni kwamba CRDB wamejitoa kwenye tatizo lolote litakalotokea kwa matumizi ya kadi yako. Kitu ambacho ni tofauti na kwa wenzetu kwa jinsi ninavyofahamu mimi.

Hiyo inafanya matumizi ya hii card yawe na risk zaidi. Yaani hata kama kosa ni lakwao bado hakuna wa kukusaidia.

Kwa mfano ukinunua kitu online halafu kwa bahati mbaya anayekuuzia akatoa fedha zaidi ya zile alizotakiwa kutoa. Halafu kwa bahati mbaya akawa anasuasua kukurudishia fedha zako. Hapo utakuwa huna jinsi ila kukubali umeliwa kimachomacho. Lakini kwa wenzetu kuna taratibu za kupinga transaction ambayo si sawa au si halali, na mwenye kadi waweza kurudishiwa pesa ambazo hukutakiwa kukatwa. Kwa CRDB inaonekana hakuna kitu kama hicho.

Sisemi kwamba CRDB wanatakiwa waweke utaratibu kama huo. Ila nasema wewe mtumiaji ujue hali ilivyo, usije ukang'atwa siku ndio ukaanza kutoa macho na kuwa mkali na CRDB.
Nakubaliana, technolojia hii bado haitusaidii.
 
Duuh...hii taarifa muhimu sana kwangu maana nilianza mchakato wa kujisajili na tayari nilishaanza kuweka dau kwenye mnada wa ebay. Yaani hii nchi kila sehemu ubabaishaji hata tunakoweka amana zetu nako hovyo asa tuende wapi?? Sio siri nchi inachosha kweli hii yaani kama tupo vikumbulu ama kimazichana bwana. Ahsante mdau kwa taarifa
 
Ndugu Manitoba na wanajamii FOrums wengine.

Msiogope kutumia VISA Electron debit card.

Jawabu: Jisajili paypal.com na utaweza kununua huduma kwenye internet bila namba za kadi yako kujulikana
 
Ndugu Manitoba na wanajamii FOrums wengine.

Msiogope kutumia VISA Electron debit card.

Jawabu: Jisajili paypal.com na utaweza kununua huduma kwenye internet bila namba za kadi yako kujulikana

Sadakta!

Ndio tunachowaambia watu hapa, unless unajua unachokifanya, jaribu kuepuka kutumia kadi yako moja-kwa moja. Na paypal inaweza kusaidia kufanya hivyo.

Mimi mwenyewe nimeiweka hiyo kadi papal, natumia paypal badala ya kutmia kadi moja kwa moja.
 
Mimi mwenyewe nimeiweka hiyo kadi papal, natumia paypal badala ya kutmia kadi moja kwa moja.
Hili ndilo wazo ninalokusudia kulifanya. Asante kwa ushauri wako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom