kimei kavunja mpaka ndoa ya tully sasa
Tukiwasema kama hivi watajirekebisha, hizi ndizo benki zetu za ndani hivyo tujione tunawajibu wa kuwakemea wanapofanya ndivyo sivyo, kukimbia (kubadili) benki sio suluhisho la kudumu nadhani ni matatizo madogo madogo pengine kama branch manager alionja miguu ya huyo mtoto, na kuwa mtoto hana maadili mema tangu huko kwao alikotoka linaweza kuwa tatizo la mtu binafsi zaidi kuliko tatizo la benki.
Wakati mwingine tukiona kero zinazidi unaonana na kiongozi wake na kutoa malalamiko yako kwamba hukutendewa unavyo paswa kama mteja, ndio maana watu hao (supervisors) wapo na wanalipwa kwa hilo.
Pale mlimani city Branch, kuna dada mmoja mrefu, mweusi na sura yake mbaya kama yangu, anadeal na business acounts. Kwa kweli Mungu anisamehe each time I go there huwa sitaki hata kumwona kwa jinsi anavyonyanyapaa wateja wenye majina madogo. This bank is stinking, tatizo kwa hapa TZ, karibu benki zote zina tatizo la aina moja, huduma na kujali wateja ni zero.
siwapigii debe. SCB wako juu kwa bank zetu za tz. nimewahi kubank na bank zote za tz na nikapiga chini zote nikabaki na barclayz na standard chartered na nataka tosa barclays japo nahudumiwa nikiwa nimeketi nibaki na scb yangu. ninao tangu 2003 sasa na hawajaniboa hata.
labda SCB ya leo, ya jana na ya juzi na nyuma ni shida tupu, wengi tulihamisha amana zetu huko. tatizo la nmabenki yetu ni customer service, utakuta benk ina watumishi 20 front desk lakini wanaweza kuhudumia wateja vizuri ni wawili tu. Sasa ikitokea una bahati ya kukutana na hao wawili kila unapokwenda ku-banki, utaisifia tu ilhali ukweli ni tofauti.
SCB ndo bank gani wajameni?tujuzane na mi nikafungue huko..
CRDB nimefunga account juzi tu kwa hasira ..poor customer service..afu huyu anakujibu hivi akija mwingine anajibu vile
afu bila haya wananambia hatuna jinsi ya kukusidia kama unataka kufunga funga..
nilishangaa sana..
Hii bank huwa naambiwa ni one of the best and efficient banks in Tanganyika, in short ndo bank nzuri ya kwanza ya kizalendo kwa huduma tanganyika sasa kama hao staff wao wameanza kuleta marangi basi itaanguka muda si mrefu/ at least kupungukiwa wateja hasa wa mjini!
...Nimekuwa napata tabu na hii benki inayofanya vizuri kwasasa kwenye Banking Industry.Kuna kero juu ya Staff wake hasa wa kike,mfano wewe ni mteja na upo dirishani kwa Teller unakuta vinanyanyua simu nakuanza kuchat mbele yako....Leo nimeenda CRDB Dodoma Branch kwa ajili ya kufatilia kadi yangu ya ATM,chakushangaza wameniacha nimesimama zaidi ya nusu saa,nilipowaambia mbona sipati huduma wanasema tulikuwa tunawaudumia waheshimiwa yaani wabunge....Kwa kweli nilipandwa na hasira sana...yaani ubunge wao unanihusu nini mimi? Niliwaifanya kazi NMB miaka fulani akaja mbunge mmoja wa viti maalumu toka Iringa akitaka nikamchukulie hela ndani maana anawai,kwakweli nilimwambia wazi sikufahamu naomba upange foleni...........CRDB mnakera jamani....
Hii nimeipenda kwani huyo changu ni lazima siku nyingine atakuwa makini huwezi kuwa unafanya vitu viwili kwa wakati mmoja na ukategemea concetration itakuwa the same, amekoma!Branch za DSM ndio usiseme.
Jamaa yangu karibuni alienda kutoa hela, sister duuhh aliyekuwa akihudumia huku akilonga na hawara zake akajikuta amempa million 3 badala ya million1.5 (badala ya kutoa bunda tatu za laki tano yeye katoa tatu za million moja moja ). Jamaa alipogundua alichukua akaomba kumuona branch mger lkn kama kawa haikuwezekana. Basi jamaa kwa hasira kaondoka zake. Baada ya siku tatu kaenda tena yule binti akamfuata akisema nilikupa pesa zaidi last time, jamaa akakana kwani hawana ushahidi walikuwa wanagamble tu.
So CRDB msipoangalia siyo tu mtapoteza wateja bali pia pesa zenu..
Nbc is the best bank and if u wish to get the best an high quality product just inverst on it.