Crazy things you did in secondary school

Kusoma cookery ilikuwa dili, mapochopocho kibao siku ya practical na kukiwa na wageni mnaenda kupika mamisosi. Basi unafungasha na kwenda kuwagawia ndugu zako. Kwa vile ukimpa anaweza kukataa, unavizia hayupo unamwekea kwenye locker lake au popote pale al muradi mzigo aupate!

Nilipokuwa form 1, mama yangu wa shule alikuwa akinifanyia kila kitu, kutandika kitanda, kunifulia, kuninyooshea na kunitafutia maji ya chai. Ilikuwa raha sana. Namkumbuka na kumuheshimu hadi leo.


Are you serious?!
What were you supposed to do in return?
 
Are you serious?!
What were you supposed to do in return?


Kwenda kuiba nguo zake, na mimi nimfulie, nimnyooshee halafu nikaweke kitandani kwake akiwa hayupo. Lakini inakuwa kazi ngumu sana kumuibia mama yako nguo, anazificha kweli. Unachoweza ni kumvizia tu, lakini walikuwa makini kweli!

Hakuna mtu unayemuheshimu hapo shuleni kama mama yako na/au mwanao, ni dhambi kubwa sana kumkuta mama yako hajavaa nguo bafuni au akiwa navaa chumbani. Yaani anakuwa kama mama kweli (unamwamkia shikamoo).

Ukiumwa basi mapochopocho hayo kutoka kwa mama zako na ndugu zako wengine.
 
Hakuna mtu unayemuheshimu hapo shuleni kama mama yako na/au mwanao, ni dhambi kubwa sana kumkuta mama yako hajavaa nguo bafuni au akiwa navaa chumbani. Yaani anakuwa kama mama kweli (unamwamkia shikamoo). Ukiumwa basi mapochopocho hayo kutoka kwa mama zako na ndugu zako wengine.

Familia shuleni...that was real crazy..Now tell me Mama, do you ever think of 'family' re-union?:
 
Kwa wale tuliosoma Tabora Girls mnakumbuka mambo ya WARSAW NA BERLIN
tukitoka disco pale milambo wanaume tukiwa tunarudi tunawakuta wavulana wa TABORA BOYS ndo wanakula ugali wa usiku tunawazomea haoooo tumetoka kwa shemeji zenu basi usiku wanavaa kininja wanakuja Girls na fimbo na kutuchapa vibaya mno..............

Korogwe girls mpoooo???
Mnakumbuka enzi za maborbo ( Tanga Tech) vs Galanos .....ilikuwa mpambano kwelikweli!...
mabesti wetu walikuwa Galanos.... Tanga Tech nao wanashindania attention.... KG tunawasare tuu..maana chice for the boys was limited!
 
Korogwe girls mpoooo???
Mnakumbuka enzi za maborbo ( Tanga Tech) vs Galanos .....ilikuwa mpambano kwelikweli!...
mabesti wetu walikuwa Galanos.... Tanga Tech nao wanashindania attention.... KG tunawasare tuu..maana chice for the boys was limited!

Natamani nirudi fomu wani ili nifaidi mambo yaliyofichika. Sisi wengine tulitumwa na vijiji kwa hiyo wakati wengine wakisoma na ku-enjoy sisi ilikuwa ni book kwenda mbele.

Kumbukumbu zangu ni kusumbua walimu hasa wanapoingilia ratiba yangu ya kusoma. Na nilikuwa nimewabandikia ratiba kwenye mlango wangu ili wajue niko bize ama niko richabo. Si mchezo, nilitafuta sana u-newton nikaambulia malaria.
teh teh teh teh
 
Saturday was my special day nilipokuwa Old Moshi.

Nikishafua viguo vyangu inabidi nivisimamie hadi vikauke manake kuna warugaruga walikua wanaiba hadi chupi! Napanda kitandani napiga horizontal kiaina (kusomea kitandani) huku nikisubiri bati (kengele ya msosi), bati likiliita naenda na plate mbili coz mshkaji wangu mtoto wa mama wikiendi lazima aende kwao akanyonye, table leader akiniuliza namwambia "namchukulia mshkaji kenda town!" kiulaiiini najikombea double share japokuwa wengi walikuwa wanajua kuwa na 'forge'.

Baada ya kula najua siku hiyo Ushirika leo inacheza kwenye ligi kuu, siwezi kuikosa hii gemu kwa kuwa vijana walikuwa wanatisha (David Rogers, Venance Mwakalukwa, Often Martin, Martin Mahimbo, etc), nashuka zangu Shengena mbio kumuwahi mshkaji kilema kwenye wheelchair ili nipate kuingia bure uwanjani, mama wee! nakuta washkaji wameshamuwahi walee wanashuka korongoni, inabidi niende nikapande juu ya mti au ukuta, akipigwa bao mtu wakati polisi nao wanashangilia hapo ndo unaruka ndani!

Baada ya mpira ni lazima kutakuwa na harusi, mimi na masela wangu tunaenda kupiga misele kwenye kumbi za ushirka kuangalia uwezekano wa kuzamia, tukishindwa tunaenda zetu kwenye hall la wanachuo kuanagalia TV(KBC tu!), mara jamaa wanatutoa baru. Hatuna jinsi tunaingia kitandu kula mbege, mitumbo inajaa na mikojo kibao, tunaamua kwenda red house kumalizia na gongo ili tuwake vizuri!

Ukirudi school saa 4 usiku unaona washkaji wanashika pua tu, soon unagundua kuwa 'pamenuka', Mdudu mwenguvu amepiga roll call ya nguvu bila kutarajiwa na jumatatu darasani kutakuwa hapakaliki! Monitor ni mshkaji ananitonya usiwe na wasiwasi 'nilikutiki'!

Umbwe,
Siku moja na mamitungi yangu narudi school toka uswekeni, bwii na giza vikanifanya nisione kilichokuwa mbele yangu, kumbe lilikuwa ni jopo la maticha nao wametoka kuutwika! Si nikagongana na mmoja wao uso kwa uso? jamaa akaning'ang'ania na maticha wengine wote wakanirukia huku wakinilazimisha niseme mimi ni nani, I was quite famous and popular! Nikawa nafight niwatoke huku nikiongea kishwahili cha lafudhi ya kichaga na kujitetea kuwa mimi sio mwanafunzi! Nilikuwa nimevaa ki OPP nikawa nakisikia kinachanika taratibu jinsi songombingo linavyoendelea, nilifanikiwa kuponyoka na kuwaacha na kiOPP, nikatoka na moto mkubwa hadi school na ponapona yangu umeme ulikuwa umekatika, giza ndilo lililoniokoa siku hiyo otherwise ningetemwa school.
After one week napita kwenye nyumba za maticha nakaona kaflana kangu mlangoni kwa ticha mmoja anapigia deki, mii kimyaaaaa!

Katika shule zote nakumbuka jinsi ambavyo mabafu yalikuwa yakijaa baada ya debe (disco) kuisha usiku! Wee nanihii nakujua huogagi kabisa, kulikoni huku bafuni saa hizi usiku huu wa manane na kirevola chako mkononi? Blues zilikuwa zinatutesa sana na kutuchafulia suruali kwa kiwango kikubwa!
 
KanakaNsungu welcome back
Hamjawahi kwenda kucheza game Moshi Tech?
Hao jamaa wa ushirika umenikumbusha mbali unamkumbuka Willy Martin ,Mohd Husein
 
Wa Musoma Alliance 1975/78 mpooo? Mambo ya Nyoya, Pyiramid na Top Layer na jinsi tulivyokuwa tunawapelekesha watani wa jadi Mara Secondary kwenye football? Mnakumbukwa mwaka 1975 aliletwa binti mmoja pale kama majaribio ya kuifanya kuwa shule ya mchanganyiko. Eeebwana ee!

Ilikuwa patashika unifomu kuchanika jinsi kila mvulana alivyojitahidi kuwa Company ya yule Binti! unaambiwa kila akipita hivi alikuwa anafuatwa na ruundo la wavulana!

One thing, though! alisaidia sana mwaka huo wanafunzi kuwa at their best most of the time kuliko walivyokuwa wakivaa rafu rafu tu kabla!! I Miss those days!
 
KanakaNsungu welcome back
Hamjawahi kwenda kucheza game Moshi Tech?
Hao jamaa wa ushirika umenikumbusha mbali unamkumbuka Willy Martin ,Mohd Husein

Thanks man,
Willy Martin namkumbuka sana, si alikuja sajiliwa simba? Moshi tech napakumbuka sana, pale ndio ilikua kiwanja chetu kipindi cha UMISETA. Kuna kioja kimoja nakikumbuka hadi leo hii kilichotokea wakati tukiwa Moshi tech wakati wa UMISETA. Wakati wa kula yakaletwa mapoti ya ugali kwanza, wakati tunasubiri mboga, akaanza jamaa mmoja kudonoa ugali kama vile kuonja, mara mwingine akadonoa, mwingine kadonoa tonge kubwa kidogo, mara sereka likafumuka kila mtu akajikuta ameshika ugali wake mkononi, utamu ulikuwa pale mboga ilipoletwa na ilikuwa ni mchuzi, jamaa aliyebeba dish anatokea tu mlangoni watu wakamvamia, nyama ilikuwa haina mpango siku hiyo kwa kuwa kila mtu alikuwa anajitahidi tu angalau aloweke kipande chake cha ugali kwenye lile dishi la mchuzi!
 
Nakumbuka nikiwa Form 1, tulikuwa tunafanya mtihani wa kiingereza basi baada ya muda wa mtihani kuisha mwalimu akasema wote wekeni kalamu chini, mimi kuangalia nilikuwa nimejibu maswali kama matano tu kati ya kumi na tano , basi tulivyoambiwa kila mtu alete mbele karatasi tulizofanyia mtihani mimi niliificha ya kwangu sikuikusanya kabisa. Siku mwalimu anarudisha makaratasi ya mitihani kwa wanafunzi na mimi nikamdai kuwa mbona mimi sijapata mtihani wangu, basi mwalimu alienda ofisini alitafuta bila kupata baade ikabidi anipe tu maksi akaniandikia 78%.

teh teh..

Aisee wewe ni fisadi..
 
teh teh..

Aisee wewe ni fisadi..

tena ufisadi wake kauanzia mbaliiiii no wonder why baadhi ya viongozi wetu wanakua mafisadi wakubwa wakipewa dhamana kubwa kubwa serikalini hatuwezi jua wao vipaji vyao walianza vigundua lini kwa kufanya nini!

well hope uliyejipatia 78% hukuendeleza kipaji chako maana ni against sharia za Mungu
 
Tulichanganya sulphiric acid pamoja na chuma kwenye beaker na kumuwekea chini ya meza ya mwalimu tusiyempenda!
 
ilikuwa saa mbili asubuhi mwaka 1989 pale Tambaza boys, basi likatushusha muhimbili enzi hizo UDA, Tukawa kundi kubwa tunaelekea shule, kufika viwanja vya muhimbili walimu na wanafunzi wengine wako mstalini, mwalimu mmoja mnoko pamoja s.master wakatusimamisha wote wakitutenganisha na waliowahi.

tukaambiwa chuchuma chini anzeni kichurachura kuelekea shule ya msingi muhimbili then mnarudi mstalini Tambaza ukifika unapata bakora unaelekea class.

Sasa kilichotokea wakati tunaruka kichurachura jamaa mmoja akasema tukifika muhimbili primary hakuna kurudi nyuma kwenye bakora tunasimama wote na kuaanza mbio kulelekea muhimbili hospital,diamond jubilee na kwengineko town kama faya.

walimu walibaki midomo waza tukazurura posta ,library hasi kesho tukaje shule walimu hawamjui hata mmoja.

eeeh eeeh ilikuwa kali maanake,
 
Back
Top Bottom