Crazy things you did in secondary school

Nakumbuka cku yakwanza naingia shule flani form1 nilibana mavi kwa siku kama 3 hiv kisa ctaki kwenda chooni vyoo vichafu utoto wa Mama mwingi. Cku kama ya 4 niko assemble kilichonitokea Mungu mwenyewe anajua. Ngoja niishie apa

Hahaha hahaha bro nn kilikukuta au muscles zili relax zen mzigo ukashuka wenyew.....
 
Dah ilikua form 2 nilisema kwa cube members wangu kuna kiatu cha jamaa mmoja Wa form six kinanuka ,wakaenda kunisemea ,kumbe jamaa alikua mtabe na anaheshimika kindakindaki ,muda Wa jioni unaingia kaanza kunitafuta dormitory ,nlienda kulala juu ya mti mpaka asubuhi nikanyoosha kwa headmaster kwa usalama wangu ,asubuhi naona jamaa anakuja kwenye office ya headmaster huku anapiga mluzi halafu katabasamu.

Headmaster mwenyewe anazima fegi kwa jamaa akaniombea msamaha ,kweli jamaa akawa kaka wangu Wa shule hakuna aliyenionea Tena ,sema ndio hivyo kumfulia, anakupa sh 50 umletee mkate, soda na change ibaki ,ukiletewa nido sijui na blueband unanyoosha moja kwa moja kwake
 
St. Anthony's Sec. Mbagala kuna jamaa walifanya mashindano kutembea UCHI wa MNYAMA mshindi apate Tsh. 20,000/= (watu walichanga) jamaa ili kufika mwisho akapewa hiyo pesa na baadae jioni akafukuzwa shule.
 
St. Anthony's Sec. Mbagala kuna jamaa walifanya mashindano kutembea UCHI wa MNYAMA mshindi apate Tsh. 20,000/= (watu walichanga) jamaa ili kufika mwisho akapewa hiyo pesa na baadae jioni akafukuzwa shule.

hahahahahahaha 20,000 imemponza
 
Mlivaa chupi ya VIP zina mistari horizontal kawaida ya chupi Hizi zinabanaga Sana na zinakatika katikati, sa nlikua Nacheza mpira, si unajua zamani timu moja lazima Ivue shati..? sa ile VIP bhana ikakatika, si ikaanza kupanda juu? Kuja kustuka Ipo tumboni halafu Madem walicheka saaana daaah!!!


Hahahaaaaaaaaaaaa
 
nakumbuka nikiwa la std 7, afu ndo nilikuwa kati ya top 5 wanaotegemewa kubeba bendera ya shule.

Tukafanya mitihani, nikapata inglish 16% walimu walipagawa wakaniita ofisini wananishambulia wanataka kunichapa. Ile kuniuliza nimepatwa na nini.

Nikawajibu, Nimerogwa.

Ilibidi waniache maana nilikuwa nalia kama mfiwa.




yu made my day
 
Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!

Mkuu siku ya Kande na Wali Nyama, utajua "wamisishaji" maana tunavaa makoti marefu yenye mifuko ndani alafu tunaingia nalo Dinning.

Tunabeba malboro kwaajili ya kupakia Kande na Wali kutoka kwenye sahani Za wengine....Duh hahahaha.....those old days jamani....
 
tulikuwa tuna mtindo wa kudoji vipnd unapga msuli bwenn sasa kuna cku ticha akaja bwenn 2likwa na mwanangu 2napga msuli ile tcha kufungua mlango mm nkaingia chin ya uvungu wa ktanda dah c nkaingia nusu viatu vikaonekana tena sikuvaa soks miguu imepaukaa ticha alpoiona miguu ikabdi acheke to wakt huo mm cjui kama kama ameniona nkawa nasema kmoyo moyo kilugha lelo ndero..yaan leo ndio leo

Hahahaaaaa, ikawaje sasa!?
Hukupoke kichapo?
 
duuh mara sec hiyo iwe siku ya nyama afu wewe ndo mgawaji unawahi sana kabla wenzako hawajafika unapiga 3 za fasta unatulia. zikipelea mnawekeana bifu na aliekosa
 
Zile dansi za kunatana ziliniadhiri mzee mzima. Baada ya ukame mrefu wakaja mabinti kutoka Weruweru.Nikampata binti mrembo anaitwa Amina. Baada ya kunatana kwa muda kukiwa na kagiza kidogo, taa zikawashwa.

Nilipatwa na uvimbe kwenye suruali yangu nikashindwa kurudi kwenda kukaa. Nikavunga kuingiza mikono mifukoni. Picha ilishaungua ikabidi nipewe pole.
 
Haijapita hata miezi miwili hii issue ilinitokea live high school huko rombo.

ilikuwa jpili nikaamka zangu fresh tu bila mbwembwe zozote tukawa dormitory na boyz wenzangu tunapiga piga story tunasubiria uji ndo tuende kanisani.

kwenye saa mbili hivi kuna mshikaji akaja akaniita akaniambia kuna binti wa form 6 anakuita yupo jirani na dormitory kwao bila mbwembwe nikaenda nilivyomwona kumbe najuana naye ni binti ambaye tulikuwa mabest toka ni toke,kiufupi nilikuwa nimezoeana naye sana tu utani kwa sana basi nikamfata akaniambia alichoniitia, badala ya kuondoka tukaanza piga piga picha story za kawaida tu si unajua wanafunzi tena.

mara headmaster akapita na gari kumbe alituona bhna niliamini hvyo baada ya kupita nusu saa aliporudi akatukuta pale pale nikiwa na huyu dada akasimamisha gari akaniita akanitazama kwanzaaa coz nilikuwa nimevaa jezi za chadema kisha akaniuliza wewe ni mwanafunzi wa hapa nkamjibu ndiyo akaniuliza unamwambia nini huyo binti hapo nimesha panic kiroho juu nkamwambia tunapiga story za kawaida fyuuuuuuuuuuuu mzee aka mind akashuka kwenye gari nikala vibao vya kutosha kuna lirungu nilikuwa nimeshika akalichukua akanilaza chini akanipiga nalo mpaka likavunjika.

akanichukua na binti mpk ofisini kwake akaagiza fimbo bhana mwanaume nkainamishwa kwa mara ya kwanza tangu niinge advance level nikala 3 za maana.ikafata zamu ya binti kuchapwa binti akataka achapwe kalio nkaona sio kabisa nkamzuia headmaster nkamwambia mwachee dada huyu ni mgonjwaa.

headmaster akaniuliza umejuaje wewe ni matron????nkakosa cha kujibu ila binti akachapwa za mkono tukamwachia namba za wazazi tukingoja waitwe turudishwe home siku 21.

hiyo siku ya jpili ikaisha ilipofika jumatatu asubuhi kwenye morning parade headmaster akaja parade na walimu karibia wote wako 104 hivi.mzee akaanza kuwahadithia wanafunzi 1400 jinsi alivyonikuta na huyo binti kwamba alienda moshi na kurudi bado tunazungumza tu,mbaya zaidi akatupandisha assembly wanafunzi kutucheka tu.bahati mbaya hakuturudisha home wala hakupigia wazazi simu kesi ikaisha.

Yaani ule udhalilishaji unanicost mpaka nakufa kwanini wanafunz wa day walivyofika nyumban wakawahadithia wazazi wao basi siku nimetoroka nipo mtaani wazazi wakiniona tu ninanyooshewa vidole.
 
Hahahaaa, Mkuu mie nilisoma Mazengo nikiwa Mdogo sana huwezi kuamini.

Nimekuja kubarehe nikiwa Form 3 mwishoni. Nilikuwa najisikia aibu sana kuwa na kisauti cha Kike.

Kwa sababu hiyo, sikuweza kuacha Watoto kabisa pale Mazengo. Ila kuna Mwenzetu alimpa mimba Mtoto wa Mwalimu Magambo. Huyu Magambo alitokea Ifunda au Mtwara Sec na huko alikuwa akisifika kwa kupiga Wanafunzi.
Kijana alikuja kufukuzwa shule. Alikuwa mtu wa Iringa kama Sikosei.

Alikuwepo yule Mwalimu wa Umeme anaitwa Ndile kama sikosei, mtu wa Mbeya. Watoto wake Wazuriii halafu wamejazia Makalio ni balaa. Ila ilikuwepo imani kuwa ukilala nao tu, unapata Division 0. Mhhh, wengi waliogopa.

Wagogo na Kisauti chao " Mpishi, Chikulomba Malenga." Hapo Shedi linajibu "Malenga Msina..."

Sikonge na Ngonalugali - wazee wa Complex, mmnenikumbusha mbali sana. BTW wale watoto wenu mlowaacha pale kijijini Kikuyu sasa ni wakubwa, mnapeleka matumizi wakulu??
 
Back
Top Bottom