Countdown ya CCM na hatima yao baada ya siku 90 leo

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Tumekuwa tukihesabu miezi wiki siku hatimaye masaa kutimia muda wa siku 90 waliopewa wanaodaiwa magamba ndani ya CCM wajipime na kujiondoa wenyewe ikibidi watalazimishwa kuondoka lakini hadi kufikia count 0hrs hakuna ayejiondoa au aliyewalazimisha kuondoka.

Je nini hatima ya wanaotakiwa kuondoka na wanaotaka wenzao kuondoka na hatima ya chama kwa ujumla.

Maoni yangu inawezekana kwa vile waliambiwa wajipime wenyewe labda wamejipima na kuona hakuna sababu ya wao kuondoka.

Vile vile kwa upande mwingine wanaowataka wenzao kuondoka labda nao wamejipima wakaona hawana sababu za msingi kuwataka wenzao kuondoka.

Nini mawazo yako.
 
mamvi ni jitu kubwa sana kuliko unavyoweza kudhani, hawana cha kumfanya yule, medhali wapo nae basi maraia tusubiri aendelee kupunguza kura zao 2015.
 
Walikuwa wanatingisha kibiriti tu wamekuta kimejaa sasa wanagwaya na kutafuta pakutokea. Wakishindwa kujivua gamba basi Lowassa, RA na Chenge ndio watakuwa the most powerful people kule kwa akina magamba na hivyo kuanza kutengeneza mtandao wao mwingine kuelekea 2015 ili kuhakikisha Lowassa anaingia Ikulu.
 
Kelele za Napelape ni kama za chura hazimzuii tembo kunywa maji mtoni, naona mapacha watatu wanapeta tuu kiulainiii huku CCM aka magamba ikifa taratibu kifo cha asili(Natural death)
 
nothing cha ajabu kwa hao jamaa tumeshawazoea na propaganda zao, saizi si unaona jinsi wanavyojitahidi kuwasafisha? yahani watz ni kusa kubwa kuendelea kuwapa madaraka wezi wakubwa hawa
 
Walikuwa wanatingisha kibiriti tu wamekuta kimejaa sasa wanagwaya na kutafuta pakutokea. Wakishindwa kujivua gamba basi Lowassa, RA na Chenge ndio watakuwa the most powerful people kule kwa akina magamba na hivyo kuanza kutengeneza mtandao wao mwingine kuelekea 2015 ili kuhakikisha Lowassa anaingia Ikulu.
Unataka kusema watarudi kama mbogo aliyejeruhiwa.
 
Nimeyatafakari yale maneno ya Nape......."Chama kikubwa kuliko serikali, na kuwa maamuzi ya au msimamo WA serikali kuhusu WATUHUMIWA wa RADA hautaathiri UAMUZI WA Chama kuwafukuza WATUHUMIWA hao KWENYE vikao vya MAAMUZI"
Kwanza kwanini maneno haya yasemwe na Nape na SI KIONGOZI mwengine yeyote CCM?
inamaana Nepi ndo kashikilia Chama na HIVYO anaongoza MPAKA serikali?
Mwisho maneno Yale NI saw a na KUSEMA CHAMA KIMERUDIA MTINDO WAKE WA KUSHIKA HATAMU/PATAMU......
 
watz ni sehemu ya kujifunzia uongo na kudanganya pasipo na ulazma..
My take: viongozi walio wengi ni waongo na wanataka umaarufu.
 
Hawa kina lowasa wanachonifurahisha ni ukimya wao kana kwamba hakuna kinachoongelewa juu yao. Ngojeni muone ccm wataibuka na mpya maana hawakuwataja kwa majina ukiachia nape ambaye mimi namwona kama mpiga porojo. Utashangaa wanawajibishwa wenyeviti wa mashina, who knows!
 
Dah nawaonea huruma kweli mnaotegemea hao mafisadi wafanywe chochote cha maana. Kweli Watanzania ni wepesi wa kusahau. Hawa watu hawaja fanywa kitu tokea 2007 mnategemea wafanywe nini leo hii? Ni ushahidi gani uliokosekana 2007 ambao ume patikana leo hii?Watanzania hamjachoka kudanganywa na kufanywa watoto wadogo? Watu gani wana tuhumiwa kwa ufisadi wanapewa siku 90 wahame chama badala ya kuwa chukulia hatua hapo hapo??? Dah kweli ni rahisi sana kuwa mwanasiasa Bongo.
 
Maoni yangu inawezekana kwa vile waliambiwa wajipime wenyewe labda wamejipima na kuona hakuna sababu ya wao kuondoka.Vile vile kwa upande mwingine wanaowataka wenzao kuondoka labda nao wamejipima wakaona hawana sababu za msingi kuwataka wenzao kuondoka.Nini mawazo yako.
Nafikiri kila kitu tayari umeshakisema hapo! Sijui unataka maoni gani tena
 
Ilitajwa in terms of scale, 90dys=90yrs guys. Oooh! Sorry, walikanusha kuwa hawakutoa siku tajwa.
 
Hawa jamaa walikurupuka kufanya uamuzi huu na hii wamelikoroga BM atalaumiwa sana kwa kutoa pendekezo hili kama anavyo laumiwa Bilal kwa kutoa pendezo la wagombea nafasi zote kupigiwa kura za maoni na wanachama wote Na hili litawagharimu hawawezi kuwatoa/kuwafukuza hata baada siku 120 it is impossible kama hamuani ona wanavyo safishwa taratibu juu ya rushwaya rada bungeni na subiri uone wamegundua kuwa wakiondoka hawa ndiyo mwisho wa chama and this is the reality chama ni hawa jamaa wapo wengi na si watatu tu follow the list of shame according to Dr Slaa
 
Back
Top Bottom