Countdown to SIMBA v YANGA showdown on 3rd October 2012

Status
Not open for further replies.
Wakati uongozi wa Yanga ukiitaka Wizara ya Nishati na madini kupitia Shirika lake lenye dhamana ya kusambaza umeme kuhakikisha hali ya umeme inakuwa katika ubora unaostahili leo jioni/usiku ili mtanange uweze kupigwa bila vikwazo wenzao wa upande wa 2 wameendelea kuja na sababu lukuki za utangulizi.
Baada ya kulalamikia Card nyekundu za kujitakia walizojipatia wachezaji wao wakidai kuwa walionewa sasa wamekuja na kali zaidi,kupitia Msemaji(ovyo) wao Ezekiel Kamwaga Simba imemlalamikia Mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mechi hiyo Mathew Akrama ya kwamba hawana imani naye,nanukuu...
“Tunajua sekretarieti ya TFF ndiyo huwa inahusika kupanga marefa, na ndiyo hii hii ambayo tunailalamikia haitutendei haki, sasa sisi tunamuomba mambo mawili makubwa Akrama, kwenye mechi ya Simba na Yanga; kuna watu huwa wanapoteza maisha wakifungwa. Kuna watu huwa wanapoteza fahamu, wanaweka rehani nyumba zao, mali zao kucheza kamari, na wanaliwa.kuna viongozi wengine wamewahi kutimuliwa madarakani kwa sababu ya kufungwa na Simba na Yanga.
Kwa hiyo, hii mechi ina mambo mengi sana, sasa sisi tunamuomba Akrama asiue watu, asifanye watu wakaliwa, asifanye watu wakapata mateso yasiyo na sababu"...mwisho wa kunukuu.
Binafsi napenda kumkumbusha kuwa kama mtu atazimia au kupoteza maisha kwa team 1 kati ya hizi 2 kufungwa ni yeye na mshtuko wake na systems za mwili wake ku'fail Mwamuzi kama Mwamuzi hana uwezo wa kuzuia hili kutokea kama ni lazima litokee,sawasawa na wale wanao'bet kwa kuweka rehani Mali zao.
Ninaona dalili za Viongozi wa Simba kutoiamini team yao ndani ya uwanja,ni kama vile wanaona nafasi yao ya kuifunga Yanga leo ni finyu sana na ndo maana wameamua kuja na mwendelezo wa sababu za utangulizi ili wanalolitilia shaka likitimia basi wapate cha kujitetea mbele ya mashabiki,wapenzi na wanachama wao, walianza na Card ya Okwi,wakaja na Card ya Maftah na sasa wameingia kwa Refa atakayechezesha mechi ya leo, what is this?
 
Kama kikosi chetu kitakuwa kama ninavyotarajia kwa maana ya Kaseja golini, Chollo kulia kushoto Ngalema kati Kapombe na Nyoso dimba la chini Kiemba, mbavu ya kulia Eddo boy, kushoto Ngasa, kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto halafu pale mbele anamaliza Boban na Sunzu basi uwezekano wa mnyama kushinda ni mkubwa, lakini ili mechi iwe nzuri Minziro inabidi amweke benchi ama Yondani ama Mbuyu ili pembeni wacheze kulia Abdul na kushoto joshua halafu mbele Msuva kulia na kushoto Kiiza hapo hata timu yako ikifungwa utaumia lakini utafurahi kuangalia soka.
 
Tukutane jioni watani ndio mpige kelele saa hizi bado mna deni la 5-0, mpaka mtakapotufunga hiyo jioni ndio kelele zenu zitakuwa na maana
 
Tukifungwa hatutakubali ksbb zifuatazo:-
1. Okwi wetu hajacheza
2. Maftah wetu naye ame'miss
3. Mwenyekiti wa Yanga ana hela sana

By,
Mshabiki halisi wa Mnyama a.k.a Simba.

In addition, refa naye ni Yanga damu hivyo maamuzi siyo sahihi.
 
simba walishinda ile 5-0 kwa njia wanayoijua wao na huu ni ukweli wanafahamu ,sasa leo wanaona waliotumia ile njia imefungwa pingu na hakuna njia ya ushindi kwa hiyo kuanzia mashabiki mpaka viongozi ni njia iliyobaki kuanza kutoa visingizio kibao ,nikianza list ukurasa huu utaisha.
 
Sioni kwenye kauli ya msemaji wa simba kuna shida gani ameweka wazi maelezo yake kwa faida ya timu zote mbili kwa kuwa kama kucheza kamari wanacheza mashabiki wa timu zote mbili na hayo mengine, hope point ya maelezo yake ni muamuzi kuchezesha mechi kwa weledi na nidhamu. So kama unafikiri simba wanatafuta sababu tungoje matokeo
 
Sijui Minziro akishirikiana na Mkuu wake Mholanzi Ernst Brandts watapangaje 11 wa kwanza leo,kwa mtazamo wangu hawa wangeanza:-

1. Yaw Berko
2. Mbuyi Twite
3. Oscar Joshua
4. Nadir Haroub "Canavaro"
5. Kelvin Yondani
6. Athuman Iddi "Chuji"
7. Simon Msuva
8. Haruna Niyonzima "Febregus"
9. Didier Kavumbagu
10. Said Bahanuzi
11.Hamis Kiiza "Diego"

Pangekuwa patamu.......pale nyuma pamoja na kwamba wameruhusu magoli ma'5 katika mechi 4 bado ninaamini hakuna team yenye beki line nzuri kama hii wakitulia kila mtu atawapenda.

Kuna watu wawili wa watani zetu nawaonea huruma sana wa kwanza ni Mrisho Ngassa...kama kwenye mechi ya leo atapangwa kushambulia kutokea kushoto(kama ambavyo amekuwa akitumika mechi za hivi karibuni) na kusababisha awe anakabana na Mbuyu Twite kuna hatihati zile shutuma za kuwa na mapenzi na Yanga zinaweza zikaibuka upya tena kwa nguvu kubwa kwani kuna kila dalili ya Twite aliyepania kuwaonyesha Simba kuwa yeye ni beki mahiri ukanda huu tena huku akicheza kwa maelekezo ya Kocha wake aliyekuwa naye APR atamfunika kabisa.

Wa'2 ninayemuonea huruma ni Paul Ngalema endapo atapangwa asimame beki ya kushoto,itakuwa ajabu sana kama mfupa alioukimbia Fisi,Mbwa aumudu(Maftah kakimbia,Ngalema ataweza kweli,sijui...nina uhakika kama hatajipanga vizuri leo pale atakapokuwa anakabana na Dogo Msuva beki huyu anaweza kujikuta dirisha dogo akitolewa kwa mkopo kwenda team nyingine,na ikitokea tu Ngalema kuzidiwa na kulazimika Nyoso kumsaidia basi kuna hatihati Yanga leo baada ya miaka kadhaa tukaambulia penalt katika mechi dhidi ya Simba kwasababu kwa jinsi uchezaji wa Msuva ulivyo akikabana na Nyoso tu kuna mawili card au penalt.

Pale kati Chuji na Niyonzima ndo stahili,ngoma ya wakubwa kama hii mtu kama Domayo labda aingie dakika za mwisho team ikiwa tayari inaongoza....pale mbele pamoja na kwamba hajafunga hata goli 1,kwenye mechi kubwa kama hii ndo unaweza ukauona uzuri wa Bahanuzi anayejaribu kurudisha kiwango chake alichokionyesha Kagame,lkn akizingua si vibaya akampisha Mzoefu Nizar ambaye anaweza kurudi kulia Msuva akaenda kushoto na Kiiza kurudi kati kusaidiana na Kavumbagu.

All in all huu ni mtazamo wangu tu,nafikiri kila mtu anajua kuwa mpira wa miguu una matokeo ya aina 3, kufunga/kufungwa/droo.

Nawasilisha.
 
Hakuna njia yoyote, YANGA walizidiwa mpira ndio maana wakapokea kichapo cha goli 5-0 kama wanamweza leo warudishe hizo goli 5
 
Mimi nafikiri Msemaji(ovyo) yule wa Simba alikuwa anatafuta namna atakavyoweza kumpelekea ujumbe Bwana Mathew Akrama kuwa anapaswa kuwapa penalt 3 leo kama yule mwenzake aliyeiingiza mechi ile kwenye list ya mechi zilizowahi kuamuliwa ki'ajabuajabu sana,sijui hata kafia wapi yule Mwamuzi?

Refa atachezesha mechi kati ya Simba na Yanga kwanini sasa iwe Viongozi wa Simba tu waanze kutoa malalamiko na maangalizo ya kumwaga kama siyo kutafuta sababu in advance.
 
Masuke

Mtani nimekushtukia unataka Yondani akae benchi ksbb unaielewa vizuri shughuli ya mchezaji wako wa zamani,pole Kaka Yondani hawezi kusubiri kwenye mechi inayohusisha magarasa yanayojaribu kurudisha imani kwa mashabiki wao kama Sunzu na Akuffor atasimama mkoba lazima na pale kati kwetu wamecheza sana Canavaro na Yondani(kumbuka kuanzia Kagame) sina tatizo na Juma Abdul kucheza kulia ksbb na yeye namuamini lkn hata Twite katika mechi 2 alizocheza kulia alicheza vizuri tu tena hata kupanda alikuwa anapanda.

Kwenu sasa.....

Kule mbele kushoto mnapotaka kumchezesha Ngassa mnamtafutia kuibuka kwa shutuma za unazi wake Yanga hasa kama atakabana na Twite aliyekula yamini,pale nyuma kushoto mnapotaka kumpanga Ngalema napenda niwajulishe African Lyon au JKT Ruvu sijui Ruvu Shooting wakae tayari kumpokea mchezaji wao kwa mkopo wakati wa dirisha dogo ksbb mbele ya Msuva akiwa kwenye kiwango chake ninachokielewa lazima atawatumbukia nyongo tu.
 
Last edited by a moderator:
utabir wako umeangalia vigezo gani?

Utabiri wake ume'base kwenye ile mechi ya mwisho,anaamini na katika mechi hii pia refa atawapa penalt 3 na ataua move zote za kina Kavumbagu kwa offside.
 
Tisha-TOTO

Mkuu mie nilionaga kwenye gazeti 1 eti nyota yangu siku hiyo inaonyesha ni siku nzuri kwangu, yani kuanzia kipato hadi mapenzi, sii nikaenda kupiga deiwaka, siku nzima hola nikarudi kwa mguu home, nilivyofika home nikakuta wife nae anafungasha eti hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.

So usiwaamini sana hao jamaa,hapa YANGA lazima ashinde tuu.
 
Last edited by a moderator:
Anselm;

Mkuu huu ndio mziki wa kumuua SIMBA wa maonyesho:
1.Yaw Berko.
2.Juma Abdul
3.Oscar Joshua
4.Cannavaro
5.Yondani
6.Twite
7.Chuji.
8.Niyonzima
9.Kiiza
10.Bahanuzi
11.Msuva
Bench:
1.Barthez
2.Nsajigwa
3.Mwasika
4.Nizar
5.Kavumbagu
6.Gumbo"fundi"
 
Last edited by a moderator:
Yanga bana! mazoezini mnacheza viduku alafu mnataka ushindi!!! Mapouda leo lazima yatolewe na majasho! Chezea Ngassa wewe!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom