Elections 2010 Count down to election day!......

Asiyehudhuria mdahalo amejitupa nje mwenyewe bila ya zengwe

Hapo ndo penye tatizo namna ya kumtupa nje, kama kungekuwa na strong media hapo ingewezekana, nadhani wanaharakati wafanye juu chini na kushawishi wananchi kuwa ambaye hataki kutuambia ataongozaje nchi hafai yaani, asiyetaka kuulizwa maswali hafai anatumia ujanjaujanja ili afike madarakani haikubaliki. tunataka tuwaulize wagombea na kupima uelewa wao.
 
Hivi kama JK/CCM wamejitoa, vyama vingine hawawezi kufanya huu mdahalo? - Dr. Slaa, Prof. Lipumba na wale wengine hata majina yao siyajui...

Inawezekana udhaifu huu wa waandaaji wa mdahalo huu au udhaifu wa vyama vingine vya siasa katika kuhakikisha mdahalo unafanyika ndio unaowapa kiburi CCM kusema hawataki Mdahalo.
Mimi nina hakika kabisa wagombea wengine wanaweza kufanya mdahalo pasipo Kikwete kwa sababu ni ktk utaratibu mzuri wa kuelewa sifa na uwezo wa mgombea.

Hawa viongozi have to compete in a contest of popular vote ambayo huwalazimu wagombea ku demostrate their competence na vision zao kwa future ya nchi yetu. Ni sawa kabisa na ajira yeyote ile ambayo CV pekee haiwezi kuwa kigezo cha kupewa ajira isipokuwa kwa utaratibu wa interview umekuwa ukitoa picha halisi ya uwezo wa mwajiriwa kwa sababu target kubwa ya interview ni kumpata mtu anayeweza kuifanya kazi hiyo mbali na hadithi na maelezo marefu ya CV.

Hivyo matayarisho ya mdahalo yanatakiwa kuwa sehemu kubwa ya NEC kuhakikisha unakuwepo ili wananchi wapate fusra ya kutoa ridhaa yao kwa mtu wanayetaka kumpa ajira..Na hata kama JK hatahudhulia, bado wananchi watakuwa na nafasi ya kumchagua lingawaje ndio atakuwa kajipunguzia nafasi ya kupewa kura.

JK na CCM wanatafuta ridhaa yetu, wanatafuta ajira hivyo sii jukumu lao kutupa sisi masharti isipokuwa sisi ndio tunatakiwa kuwapa wao, na tuwahoji kabla ya kuwapa ridhaa zetu..Hii ndio primary consideration in the popular decision, not their pliability to the interests of the ruling party.
 
anything can happen katika mdahalo. mgombea unayedhani anaweza kufanya vizuri mambo yanaweza kumuendea kinyume na kufanya vibaya[/B].

Mkuu hapa nakubaliana na wewe kwa 100%. Na mstari huu ndio unao support na kuhitimisha yote niliyoyaeleza hapo awali. Kwa mtazamo wa ccm mdahalo hauna tija kwa ccm badala yake utakuwa unawachezesha kamali wapiga kura wake. Kwa sababu ANYTHING CAN HAPPEN, na CCM hawataki kuwa risk takers.

Faida ya mdahalo ni kwa wapinza tu na sio kwa CCM, na faida za mdahalo kwa wapinzani zitatokea tu endapo CCM ataingia mkenge wa kushiriki mdahalo. CCM wanajuwa fika kwamba wigo wa wapinzani unakuwa kila siku na hivyo mdahalo kwao sio miongoni mwa njia za kampeni ambazo zitakipa ushindi CCM. Na mwenye masikio na asikie!!
 
Hivi kama JK/CCM wamejitoa, vyama vingine hawawezi kufanya huu mdahalo? - Dr. Slaa, Prof. Lipumba na wale wengine hata majina yao siyajui..

Consultant, nilishajibu swali hili kwenye post yangu ndefu ya awali. Kiufupi ili mdahalo ulete maana wapinzani watahitaji reference point (CCM) kwenye mdahalo huu. Kwa mfano likitokea swala la kuzungumzia EPA pasipo CCM kwenye mdahalo wasikilizaji wa mdahalo ambao pia ni wapiga kura wa CCM wasiposikia kutoka mdomoni mwa JK wako LIKELY kupuuza kitakachoongelewa na wapinzani. Na hii itakuwa faida namba moja kwa CCM kutoshiriki mdahalo. Vile vile kutowapo kwa CCM kwenye mdahalo kutawapiganisha wapinzani kwenye maswala kadhaa, mfano CUF na Chadema wanaweza kutofautiana juu ya kutoa elimu na afya bure, mapigano ya wapinzani kwenye mdahalo yatakipa CCM faida namba mbili.
 
Back
Top Bottom