Could Tanzanian Gov. stop 1994 Rwandan genocide?

Masanja,

hivi akitokea Daktari bingwa toka Kenya,Uganda,au Rwanda akasema anaomba apangiwe kazi hospitali ya mkoa wa lindi unafikiri Tanzania watamrudisha kwao?

hivi kwa matatizo ya population ya Rwanda unaamini kwamba kila mwenye nia ya kuhamia huko sasa anayo ruhusu kupitia hilo tamko la Kagame?
 
Kifupi ni kwamba Tanzania tungeweza kabisa kusimamisha Genocide lakini tulifumba macho na kuwa watazamaji.. reason behind ndio kama hivyo walivyosema wasomi na wenye kuelewa huko nyuma...
Binafsi hivi vyote ni visingizio tu na hata misaada huko nyuma, Tanzania ilikuwa ikisaidia nchi nyingine kwa sababu ya kumwondoa Mkoloni na vibaraka wake -wale wote wenye kukumbatia ukoloni. Yaani Nyerere alikuwa hawezi kupumua vizuri akisikia kiongozi fulani anashirikiana na kaburu...
Idd Amin bahati mbaya picha zilikuwa haziwivi na Nyerere na pengine naweza sema kosa kubwa la Idd amin ni pale alipoivamia Tanzania kisha akaendelea kuleta mikwara kwa Mzanaki...
Tungeweza kabisa kusimamisha genocide bila ruksa ya mtu yeyote kama tungetaka kufanya hivyo kwani yule mkuu wa kikosi cha UN alikwisha piga la mgambo kuomba msaada,Tulisikia vizuri lakini tuliweka pamba masikioni.. trust me vita ile imetu cost zaidi kiuchumi na kifikra kuliko msaada wetu kusaidia Mozambique.
 
Mkandara, heshima yako mkubwa, naomba utuelezee zaidi kuhusu hilo juu highlighted. Ahsante.

SteveD.
 
GAME THEORY,

Naomba utufafanulie kama Tanzania ingeweza kuzuia mauaji yaliyotokea Congo.
 
SteveD,
Kifupi leo hii ni wachache wanaokumbuka adha tulizopata Musumbiji lakini wanakumbuka hizi za Rwanda kama mweka hoja alivyosema huku chozi likimtoka - KIFIKRA.
Kuhusu kiuchumi, kumbuka tu kwamba ni tatizo la Rwanda lilizaa tatizo la Burundi na Congo. Kisha matokeo yake Tanzania tukawa nchi inayoongoza duniani kuwa na kambi zenye watu wengi DUNIANI over a million refugees at one time..
Kwa muda mrefu sasa na hata baada ya genocide ile tumeshindwa kabisa kusimamisha biashara vizuri kati yetu na nchi hizo. na ndio maana hata reli iliposimama haikuwa big deal kwani impact ya vita ile ilikwisha ondoa kabisa biashara ya mizigo kati ya nchi hizi. nadhani unakumbuka zamani kabla ya vita jinsi convoy la magari yalivyokuwa yakipandisha kwenda Uganda, Rwanda, Congo na Burundi...Baada ya genocide huwezi kukatisha ni lazima kupitia Zambia, na wafanya biashara wadogo wadogo wote walikuwa wakivamiwa na majambazi kila siku. Risk ya kuendesha biashara kati yetu na nchi hizo ni kubwa sana kiasi kwamba wafanya biashara wengi wamesimama hadi leo hii tunavyozungumza. Ukitazama Msumbiji hatukuwa na biashara nao kubwa zaidi ya misaada ya kivita.
 
WAUNGWANA, TUTATUMIA SABABU ZA KILA AINA KWA NINI HATUKUWASAIDIA MAJIRANI ZETU KIPINDI WALIPOKUWA WANAHITAJI MSAADA WETU, lakini ukweli unabaki pale pale, we as NEIGHBOURS (ACHA HIZO THEORIES ZA INTERNATIONAL COMMUNITY na kutupia mpira UN as if UN can do anything against the wishes of its members...) we failed Rwanda na inabidi tuone aibu kama Bob alivyoandika hapo juu.

Jiulize leo Rwanda ndo anaongoza juhudi za kulinda amani Darfur! Of all countries. I tell you, Africa kwa sasa tunahitaji viongozi kama akina Kagame wenye light touch ya udikteta na vision za kuikomboa Africa! The guy is succeeding wakati sisi wengine ni kumcriticize tuuu bila kuangalia mazuri anayoyafanya!

La muhimu, tujifunze namna ya kuyakabili matatizo kama haya siku za mbeleni. Lakini nitakuwa mnafiki nisiposema kwamba sisi Waafrica hatujifunzi lolote, maana watu wanapukutika Darfur, Somalia, Eritrea, Chad...na the best Africa can do we are bickering and arguing on the right statistics za wanaokufa!!!!!!!!!!!
 
Somo la GT ni zuri lakini liko tu theorectical for a normal person to comprehend. Kwenye swala la Rwanda kuna conspiracy theories nyingi sana, but what I can say

Mzee maelezo niliyoyatoa hayana theory bali ni facts according to info zilizokuwepo on the ground

Nakubaliana nawe kuwa JF watu bado hawako ready kudigest mambo ndio maana najaribu kupeleka mada nyingi kwenye centrre stage ambako ndiko tutajadiliana based on info zilizopo
. Utaona sikujaribu kuelezea kisa cha mgogoro wa Rwanda bali nilijibu swali nililoulizwa kama Tanzania ingeweza kuzuia yale mauaji na nadhani its about time tukafanya mijadala kwa style hiyo badala ya kungangania conspiracies kwani huwezi kuingiza conspiracies kwenye approaches to international relations

Dua you mean kwamba Tanzania hatujaendelea kiuchumi kwa sababu tulitumia raslimali zetu kuwakomboa wengine especially majirani? kama Zimbabwe, Uganda, SA nk? Or Iam missing a point?

Harafu nadhani WITH DUE RESPECT approach yako kwenye foreign policy yetu ni very minimalist! Mzee hakuna anayeishi kisiwani ati! Huwezi kusema eti Tanzania tuliamua kumuachia Mseveni kwa sababu tulitaka kurekebisha uchumi wetu? upi huo? Comrade labda ufafanue zaidi, leo Membe akiadopt mawazo yako, our foreign policy will be a TRAGEDY! Ohh I hope it is not-yet! Otherwise from your comments naona ni ile ile usual over negative indoctrination ya watutsi katika ukanda wa maziwa makuu!

Mkuu whether we like it or not, Rwanda and Burundi are our NEIGHBOURS so is Malawi, Kenya, Uganda, DRC etc we have to live with them na tupendane, na step ya kwanza ni kuwaleta kwenye East Africa Community! Tunaweza tusipende na kulaumu waliofanya huo uamuzi, lakini the bigger picture is umaskini ndo unasababisha yote haya. Leo Kagame kaondoa work permit kwa mtu yeyote anayetoka East Africa anayetaka kufanya kazi Rwanda.....Hiyo ni challenge, harafu tukiona jamaa wanaendelea ndo hapo tunaanza protectionism! My Compatriots Tanzanians TUAMKE tuache visingizio. We either compete or compete! kuwapiga vita haitasaidia chochote! Ndo maana mi nasema kila mara, hii sumu tuliyomwagiwa dhidi ya watutsi ni mbaya sana! Alot needs to be done by us.

Hivi ni wapi niliposema Tanzania hatujaendelea kiuchumi? Well wengi hawakusaidia ukombozi kusini mwa Afrika, je, ni santa gani alikuwa anatupatia vitendea kazi pamoja na kuwahifadhi sio wakimbizi tu hata viongozi wao.

Unaposema my approach ni minimalist ya kwako ambayo ni broad iko wapi? What influence do you have if any to the UN charter etc. Sijasema tuishi kama kisiwa haya ni maneno ambayo pengine umekariri na unafikiri unaweza kuyatumia yasipotakiwa.

Issue Tanzania ingeweza kuzuia mauaji ya Rwanda? Sijasema Tanzania tulimwachia M7 bali Tanzania tulikuwa katika another direction ya mambo katika kipindi kile (Fuatilia yaliyokuwa yanatokea Dar, Arusha, Mwanza wakati ule). Unafikiri ni nani aliyekuwa anawazuia wawakilishi wa Kagame wakati ule wasishiriki aktika mazungumzo? Kama hufahamu kitu ni bora kukaa kimya kuliko kuvamia maswala ambayo huyafahamu.

Unaongelea Membe kushape our foreign policy hivi kwa mawazo yako unafikiri Membe ndiye anayeamua Foreign policy ya Tanzania? Pole mkuu naona bado una matongotongo. Unasema usual negative indoctrination ya watusi pengine hiyo ni ya kwako na sioni wapi ambapo kwenye comments zangu ipo.

Mkuu kama una beef ingine iweke hapa kuliko kuruka ruka bila substantive accusation. Tanzania sio kazi yetu kuwasaidia kila Tom, Dick and Harry na swala la genocide wakulaumiwa ni M7 na Kagame pamoja na foreign masters wao sio sisi.

Tanzania hatuna sababu ya kuwachukia lakini tunawataka wale wakimbizi wote warudi kwao na wakitaka waje kihalali sio kutegemea pesa ya walipa kodi WTZ. Kwenye kujiamulia mambo yetu ya ndani hatutaki tuamuliwe na nchi yoyote ile iwe Rwanda au Kenya etc. the buck stops with us na hatuna kisingizio chochote kwa hilo. Hiyo sumu ya Watutsi unayo peke yako us as a sovereign state tutajiamulia mambo yetu.
 
Mwanaharakati ameuliza a straightforward question: kwanini Tanzania haikufanya chochote kuzuia mauaji yale ya Rwanda 1994?

Hizi habari za sijui UN, US, Pentagon, UNAMIR na sijui nani kafanya hivi na vile zinatokea wapi jamani? Mimi naona tunajitafutia visingizio tu... tukubali tu kuwa tuliona kujiingiza huko Rwanda hakuna maslahi (si kwa nchi yetu wala kwa viongozi wetu), mbona Idi Amini tulimuandama mpaka Kampala tukamtoa. Gadafi alipopeleka msaada kwa Idi Amin tukawapa kichapo vilevile hatukusubiri cha UN, US, UNAMIR wala nini... kujificha nyuma ya Strategic studies rahisi sana.

Si kweli kuwa Tanzania haikufanya chochote. Tanzania iliandaa mikutano ya ngazi za juu kusuluhisha migogoro na genocide ilitokea wakati pale ndege zilichokua marais wa Rwanda na Burundi ilipotunguliwa.

Na vile vile Tanzania ilifungua mipaka yake kwa wakimbizi kuja Tanzania na kupatiwa ulinzi wa ulioakikisha usalama wao. Kama Tanzania ingefunga mipaka, kuna uwezekano mkubwa idadi ingekuwa kubwa zaidi.

Kitu ambacho Tanzania haikufanya ni kupeleka majeshi ya uvamizi. Lakini hiyo sio lawama ya Tanzania. Ni lawama ya jumuia ya kimataifa. Majeshi ya umoja wa mataifa yalikuwepo kule tayari na jumuia ya kimataifa ilihamua kuyaondoa.

Vilevile majeshi yetu yasingesaidia kitu kwani wahusika walikuwa na agenda zao ambazo sisi hatuzielewi.

Na wale wanaosema Afrika ni lazima wajiamulie matatizo yao wako sahihi lakini ni mara ngapi Tanzania imekuwa mstari wa mbele na inatoka na madeni katika migogoro ya Afrika?

Ndio Tanzania ilimtoa Iddi Amin lakini kulikuwa na mikataba ya Tanzania kuilinda Uganda na kufidiwa gharama zake. Hizo gharama hazikulipwa.

Na mtu aliyetoa lawama kubwa kuwa Tanzania haikupeleka majeshi alikuwa JK Nyerere. Kwa bahati nzuri alipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kusuluhisha mgogoro wa Burundi. Nafasi yake kama mwenyekiti haikuzaa matunda makubwa kwa sababu wa-Tutsi walisema kuwa Nyerere was pro-Hutu.
 
WAUNGWANA, TUTATUMIA SABABU ZA KILA AINA KWA NINI HATUKUWASAIDIA MAJIRANI ZETU KIPINDI WALIPOKUWA WANAHITAJI MSAADA WETU, lakini ukweli unabaki pale pale, we as NEIGHBOURS (ACHA HIZO THEORIES ZA INTERNATIONAL COMMUNITY na kutupia mpira UN as if UN can do anything against the wishes of its members...) we failed Rwanda na inabidi tuone aibu kama Bob alivyoandika hapo juu.

Jiulize leo Rwanda ndo anaongoza juhudi za kulinda amani Darfur! Of all countries. I tell you, Africa kwa sasa tunahitaji viongozi kama akina Kagame wenye light touch ya udikteta na vision za kuikomboa Africa! The guy is succeeding wakati sisi wengine ni kumcriticize tuuu bila kuangalia mazuri anayoyafanya!

La muhimu, tujifunze namna ya kuyakabili matatizo kama haya siku za mbeleni. Lakini nitakuwa mnafiki nisiposema kwamba sisi Waafrica hatujifunzi lolote, maana watu wanapukutika Darfur, Somalia, Eritrea, Chad...na the best Africa can do we are bickering and arguing on the right statistics za wanaokufa!!!!!!!!!!!

Hatuna haja ya kutoa sababu kwa yoyote, majirani zetu wanaotegemea msaada kutoka Tanzania tulisema basi kila mtu abebe msalaba wake. Whats wrong with that? If Rwanda feels they can afford to send their troops to Darfur, that's their choice not ours and I don't think there is anything wrong with that. Kupanga ni kuchagua. Hatuwezi kukomesha mauaji kila mahali Afrika acha na wengine wajitahidi.
 
Mwanaharakati ameuliza a straightforward question: kwanini Tanzania haikufanya chochote kuzuia mauaji yale ya Rwanda 1994?

Hizi habari za sijui UN, US, Pentagon, UNAMIR na sijui nani kafanya hivi na vile zinatokea wapi jamani? Mimi naona tunajitafutia visingizio tu... tukubali tu kuwa tuliona kujiingiza huko Rwanda hakuna maslahi (si kwa nchi yetu wala kwa viongozi wetu), mbona Idi Amini tulimuandama mpaka Kampala tukamtoa. Gadafi alipopeleka msaada kwa Idi Amin tukawapa kichapo vilevile hatukusubiri cha UN, US, UNAMIR wala nini... kujificha nyuma ya Strategic studies rahisi sana.

Huwezi kujadili mambo ya International relations based on assumptions, conspiracy theories na guessing. Swali liloulizwa ni je TZ tungeweza kuzuia yale mauaji na majibu niliyotoa yanatokana na data na facts zilivyokuwa

Mzee hili jnii somo pekee linalojitegemea ambalo linaitwa Humanitarian interventioon na huwezi kujadili kuhusu GI ilivyofeli in Rwanda bila kuzungumzia UNAMIR na kwa nini ilifeli kule

umeraise interesting point about TANZANIA lakini huwezi kuzungumzia Tanzanias invasion of UGANDA bila kuzungumzia hizo international systems kama UN ambazo wewe hutaki kabisa kuziongelea

Tanzania iliivamia Uganda kwa kutumia ARTICLE 51 of the UN charter na the same applied to Vietnam ambao 1979 waliivamia CAMBODIA kwa kucite hiyo hiyo article 51 of the UN charter sasa I am not sure kama uko tayari kujadili haya mambo based on International laws au vipi . Kma uko tayari lete argument then nami nitaangalia kama kuna counter argument
 
..mbona tumepeleka majeshi Liberia na tumeahidi kusaidia mafunzo Somalia?

..hivi kila wanachofanya Rwanda basi na sisi Tanzania lazima tuige?

..mbona tayari tuna askari wanalinda amani Lebanon? mbona hakuna anayeuliza kama Rwanda wako huko?

..siungi mkono askari wetu kwenda eneo lolote lile nje ya mipaka ambako maisha yao yatakuwa hatarini.

..kama ni kupoteza askari basi tuwapotezi kwa kulinda mipaka yetu.
 
Mwakilishi
NI kweli hakukuwa na maslahi yoyote, labda kama tungekuwa na sababu tungesingizia humanitarian interest. Kuna Phrase moja wanatumia wamarekani inanifurahisha sana, "you are damn if you do you, are damn if you don't" hapo ndipo tulipofikia Tanzania. Kwa hiyo hatukuwa na sababu yoyote ya kutafuta sifa kwa kutumia pesa na kuhatarisha maisha ya askari wetu.
Ile ya Uganda mimi siwezi kusema sana kwa sababu nilikuwa bado mdogo sikujua yaliyotokea, lakini hata hivyo nadhani ulikuwa ni ujinga tu, tusingemchokoza nduli kwa kum-host Obote yasingetokea yaliyotokea, au tusiruhusu ardhi yetu itumike kuisimbua Uganda yote yale yasingetukuta, labda hii ni issue tofauti.

Afadhari naona kuna mtu anayeangalia maslahi ya Tanzania kwanza.
Jumuia za kimataifa zimejaa wanafiki, Tanzania ingepeleka majeshi yake kule ingepewa ahadi lakini isingelipwa gharama zake.

Tanzania isipeleke jeshi la kulinda amani kabla cheki haijakatwa.
 
Hivi clause ya OAU kuhusu non-interference inasemaje? Nafikiri kimsingi ilichangia mataifa mengine kuingilia bila kufuata a lot of red tape.Ndiyo maana Tanzania ikaweka effort katika mazungumzo.

Good question
OAU wanao member states ambao ni members na signatories wa UN charter. Majibu ya swali lako yako kwenye ARTICLE 51 of the UNITED NATIONS CHARTER
 
..mbona tumepeleka majeshi Liberia na tumeahidi kusaidia mafunzo Somalia?

..hivi kila wanachofanya Rwanda basi na sisi Tanzania lazima tuige?

..mbona tayari tuna askari wanalinda amani Lebanon? mbona hakuna anayeuliza kama Rwanda wako huko?

..siungi mkono askari wetu kwenda eneo lolote lile nje ya mipaka ambako maisha yao yatakuwa hatarini.

..kama ni kupoteza askari basi tuwapotezi kwa kulinda mipaka yetu.

Na wanasahau katika miaka ya 90, tulipeleka majeshi Siera Leone na bado gharama hazijalipwa.
 
Jamani,
Nadhani hamfahamu impact ya vita hata kidogo na huo msalaba sijui utaubeba vipi ikiwa wewe mwenyewe una njaa kutokana na jirani yako hana muda na uwezo wa kununua mali yako. wakati huo huo nakubaliana nanyi mnaposema kuwa hatupati malipo ya kazi yetu.
Ni maisha ya kawaida ya Mtanzania (mwafrica) kuwa kila mtu na mzigo wake na ndio maana utakuta mtu tajiri ndugu zake hawana kitu. Kibaya zaidi ni kwamba hata akiwasaidia wao watahakikisha wanampeleka chini.... Yaani kazi kweli kweli.
 
By the way siyo jukumu la BERNARD MEMBE kushape Tanzanias foreign policy kwani hilo lazima litoke kwa hao ma strategist wetu (ambao hatuna ) na kama issue ni kufanya mabadiliko then itabidi hili liiiguse kila sekta ya serikali na kwa kuanza wangeanza kupunguza lile jeshi lililojaa pale foreign na kubakisha tumu ndogo ambayo itakuwa effective huku wakisubiri kupata directives za jinsi gani ya kuelekeza Foreign Policy yetu
 
Jamani,
Nadhani hamfahamu impact ya vita hata kidogo na huo msalaba sijui utaubeba vipi ikiwa wewe mwenyewe una njaa kutokana na jirani yako hana muda na uwezo wa kununua mali yako. wakati huo huo nakubaliana nanyi mnaposema kuwa hatupati malipo ya kazi yetu.
Ni maisha ya kawaida ya Mtanzania (mwafrica) kuwa kila mtu na mzigo wake na ndio maana utakuta mtu tajiri ndugu zake hawana kitu. Kibaya zaidi ni kwamba hata akiwasaidia wao watahakikisha wanampeleka chini.... Yaani kazi kweli kweli.

Lakini issue hapa ni hiyo intervention na legalities ambazo zinaizunguka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom