Could Mahiga make a good president?

Kwasababu tatizo kubwa na kilio chetu kama watanzania kwa leo ni rushwa, rushwa na rushwa basi hili ni lazima tulielewe na tunapomwangalia nani tumpe uraisi ni vizuri tukaelewa ni kwa kiasi gani rushwa imelitafuna taifa mpaka sasa. Na huyu mtu ni lazima awe na hilo kichwani, na hata tukimwangalia sura yake iseme kweli kwamba katika nchi yetu tuna Kansa ya rushwa. Binafsi sioni huyu Mahige kama ataweza kulifanya hili, anakotoka kuanzia taasisi mpaka nchi ni kati ya maeneo ambayo yanaongoza kwa kwa kuchuma mali zetu, tumetoka kupewa vyandarua ili kupitisha masrahi yao na kuchuma vya kwetu, kama tulipiga kelele kuhusu hili tujiulize huyu katokea mlsngo upi? kuna taasisi hizi za kimataifa ambazo huwa zinaandaa vibaraka wa kufanikisha mambo yao na hawa watu huwa wanaandaliwa na mwisho huwa wanakabidhiwa kazi ya kutekeleza policy za wakubwa hawa, huyu atakuwa ni mtz mwenzetu lakini kiutendaji tayari ana affiliation kubwa na waajiri wake alipo,sasa katika kuielekeza nchi yetu kwenye kujitegemea na kuing'oa rushwa hasa katika kulinda Mali zetu dhidi ya misaada ya aina ya vyandarua tutakuwa tumeliwa. Nisingependa tuwe na imported leader kutuongoza, tusidanganywe na kufanya kazi UN, hawa wa hivi si wenzetu kimitizamo na kiajenda pia hatufanani nao kamwe.
 
Back
Top Bottom