Corrupt Generation 50-70 years

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,603
8,741
Jamani Watanzania wenzangu nisaidieni kwa mawazo yangu Generation ya 50-70 years ndiyo yakulaamu kwa umasikini wetu. Sithani kama Generation zingine zitakuwa corrupt na kutojali nchi kama hawa wazee je mnasemaje?
 
Hapana, sikubali kabisa.
Akina Masha hawajafikia hata hiyo miaka 50. Akina Lukaza ( spellling) Corruption haina age.
 
Kamundu tusitafute ubaya wa kizazi gani hapa. Tuyaonayo ni matunda ya kuchezea uhuru.

Assumptions tulizochukua baada ya uhuru ni mbaya. Unampa mtu madaraka na hakuna check and balance yoyote hile.

Wangapi hapa mkipewa Ugavana wa benki kuu bila kuwa na check and balance mtafanya kazi zenu vizuri?

Kwa cheo chako cha ujenerali wa jeshi unaona kilo 40 za nyama kwa wiki hazitoshi unataka kuchinja ng'ombe mmoja kila siku.
 
Kuna vijana corrupt pia lakini kwa kiasi kikubwa Generation ya corruption ni hiyo. Vilevile kama wanapinga basi waongee ni sisi vijana tu ndiyo tuna mwamko na uchungu wa kuonekana. Kma kuna wazee safi basi ongeeni na semeni mawazo yenu ni nini. Kama wewe ni Mtanzania wa miaka 50 na nchi yako inaliwa na usemi kitu, hupigi kelele na huonyeshi uchungu sisi tutafikiriaje?. Hawa jamaa wanasaini mikataba ya miaka 30 ya rushwa wanajua kazi ni kwetu si kwao! Jamani angalieni nchi yetu inapoenda, hadi raisi na spika wanapeta si nchi imekwisha hiyo
 
Thread hii ni discriminatory kwa namna fulani. Nina wasiwasi na intellectual capacity ya mwanzishaji wa thread hii. Nadhani ni mpiga debe wa wanasiasa wabagangaizaji wa TZ wanaodai kuwa wazee hawafai kusudi wapewe wao ili "watese." Huwezi kusema kuwa kuna genretaion fulani ni corrupt kuliko nyingine. Nyerere alikuwa ni Mzee wa kumzaa Lowasa lakini alimwambia Lowasa point blank kuwa wewe ni corrupt. Kwa mantiki ya mwanzisha mada hii, umri wa Nyerere ulikuwa unam-qualify yeye kuwa corrupt zaidi ya Lowasa. Hiyo haikliki kwenye maindi yangu kabisa.

Nina views pana kidogo kuhusu umri mtu na madaraka yake lakini siyo kwa mlengo wa mwanzisha mada hii. Nitaweka maoni yangu hapa kesho kwa vile sasa ni tuuu leit.
 
Kichuguu nakubaliana na wewe to a very high %! Corruption is an act of mind, not age! Hii blame game anayoileta huyu mwanzilishi wa thread haifai ktk jamii kwani kuna vijana wako corrupt sana kupita hata wazee kwenye hiyo range yake! kwa hiyo nafikiri hapa suala la kujadili sio generation ipi iko OK na ipo haiko OK ila ni kujadili how do we deal with whatever the situation we are in now because of some corrupt minds!
Tuangalie mbele zaidi ili tusipoteze umakini wetu kwa kujadili umri na vizazi.....
 
This guy might have a point. Ukiangalia kwa umbali utaona watu wengi ambao wako implicated au mentioned kwenye skendo kubwa kubwa wako kwenye age ya 45 and above. Kwa vile hakufafanua alikuwa anamaanisha nini ni vigumu kuanalyse point yake. Lakin kwa ujumla TZ watu wengi serikalini wanaanza kupata madaraka makubwa wakifika miaka 45 na at this stage ndiyo huwa grand corruption inaliwa na watu huwa wanakuwa protected kwa vile wanakuwa wameshajijengea network baada ya miaka 20+ kwenye serikali ya CCM.
 
je Generation hii itakumbukwa kwa nini??

Nyerere si mtu wa 50-70 years na Lowassa yuko kwenye group hii sasa point yako ni nini?

Generation ya nyerere kwa mawazo yangu ndiyo great generation yetu lakini hawa waliofata ni Generation Corrupt.Hakuna haja ya hasira na kupigana madongo tujadili kuelimishana.
 
inaelekea webmaster anafuta reply ili topic yangu iende chini, Mini nilifikiri hii website ni readers ndiyo wenye power, sijatukana wala kusema kitu kibaya ni ukweli tu. Labda kila topic iwe ya kashfa ndiyo webmaster ataiacha.
 
kwanza ni vyema kujua ni corruption ya kiwango gani? je unazungumzia grand corruption kama richmond, buzwagi,
bot nk. au corruption ya kiwango chochote.

kama mtu anavuta corruption hata kama ndogo
kutokana na nafasi yake ndogo serikalini ujue mtu huyo
ni corrupt tu na angepata nafasi kama ya buzwagi basi
napo angevuta tuu. kwa hiyo hoja ya umri na corruption
nadhani haina nguvu.

je ni nani aliyesema hapa jf wanaoingia ni wale chini
ya hiyo age group uliyoitaja? naamini wapo wachangiaji
wenye umri zaidi ya 50 wanaoingia hapa na kutoa michango
makini ya kupiga vita corruption.

aidha naamini wapo watu ambao japo hachangii hoja humu wanakuwa
source ya information zinazokuja humu.

hivi umeangalia hao wamiliki wa makampuni 22 yaliyotajwa bot
wanaumri gani? jee wale akina vithlani (sina hakika na spelling) wa mambo ya rada wana umri gani vile?
 
inaelekea webmaster anafuta reply ili topic yangu iende chini, Mini nilifikiri hii website ni readers ndiyo wenye power, sijatukana wala kusema kitu kibaya ni ukweli tu. Labda kila topic iwe ya kashfa ndiyo webmaster ataiacha.

kamundu, acha hizo bana wee, ukiwa member mwenye post zaidi ya 120 hivi sasa, sitegemei uje na kauli kama hii... mbona unatoa lawama sizizo msingi?! Kuna thread ngapi ambazo zina umuhimu katika maisha ya Watanzania lakini hazina response kubwa. Usilazimishe member kuchangia thread yako kwa vile tu wewe umeianzisha. Yaani mtu uananzisha topic nzuri halafu katikati yake una kuja na kauli kama hii... vipi tena mkuu?! daah, inakatisha moyo kwa kweli. By the way, haya ni maoni yangu mimi na si ya huyo webmaster uliyemlenga. Natumaini umenielewa. Ahsante.


SteveD.
 
Back
Top Bottom