Cord: Wakenya sahauni kabisa pesa za Eurobond

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
5,508
9,091
4bk45eb498680b6ffd_620C350.jpg


Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD umewataka raia wan chi hiyo, kusahau fedha zilizotokana na mkopo wa Eurobond kwa kudai kuwa, ni suala lisilo na shaka kwamba fedha hizo zimeshapotea. Wakiongea hapo jana Alkhamisi na waandishi wa habari jijini Nairobi, viongozi wa muungano huo waliwataka Wakenya kutotarajia kupata tena fedha hizo walizosema ziliibwa. “Mkopo huo ulitolewa ugenini na kuibwa kuko huko. Badala yake serikali iliwasilisha deni nchini,” alisema Bw Kalonzo Musyoka aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya Raila Odinga na Moses Wetang'ula. Viongozi wa muungano huo wa upinzani nchini Kenya walifikia hatima hiyo baada ya Gavana Patrick Njoroge wa Benki Kuu (CBK) kukataa kukutana nao.

Katika taarifa aliyotoa juzi Jumatano na Dkt Njoroge alisema kuwa, habari waliyokuwa wakifuatilia viongozi hao wa upinzani ilikuwa haiwezi kutolewa nje kutokana na sheria inayosimamia sekta za benki nchini.
 
Ni vigumu sana hawa jamaa kuendelea, katiba nzuri sana mnayo lakini madudu ni mengi mno!.... WTZ katiba mbaya lakini angalau tumepata kiongozu mwenye uzalendo na nchi
 
hahahaha.....eti zilitengwa zikiwa ughaibuni zikaibwa huko huko....
 
Haina tofauti na $600M walizodalalia kina Shose Sinare na Sioi, nani anajua zilipoenda????
 
Back
Top Bottom