Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
- Thread starter
- #21
Hii ya kusema kwamba wazungu wanampinga Uhuru kwakuwa atawakwamisha ni mbinu ya jubilee kutafuta huruma ya wakenya kumchagua Uhuru.
Ni uhuru huyu huyu ambaye amejaza uwekezaji wake huko kwa wazungu sasa wamuogopee kitu gani? Wazungu hawataku kurisk kwa kuwekeza kwa mtuhumiwa wa ICC ambaye anaweza kuhukumiwa kifungo na hivyo wao wakashindwa kufanya biashara na uwekezaji kwa kushirikiana na serikali ya Kenya.
Kutokana na hilo wapambe wa Uhuru na jubilee wamekuwa wakieneza propaganda hiyo kama njia ya kuwahadaa wakenya wamchague na sitarajii kama hiyo propaganda itawasaidia kiasi cha kutosha.
Mwita Maranya Uhuru kawekeza Kenya siyo ulaya kama unavyodai na hao wazungu wanataka kuwekeza kenya kwa mazingira ambayo yatawanufaisha na siyo lazima wakenya wanufaike pia..............
ICC haina bao baada ya Uhuru kushinda uraisi na kesi zote zitahamishiwa Arusha kwenye East African Court of Justice na huko zitafutwa kwa sababu hakuna ushahidi wa kuwaunganisha watajwa..........
Ushahidi ambao ICC hadi leo inaukusanya na kutamba nao ni wa kuthibitisha vurugu na mauaji yalitokea lakini siyo ushiriki wa wahusika tajwa kwenye mauaji hayo.......................
Unapozungumzia Uhuru kufungwa lazima uuweke mezani ushahidi ulionao na huna....................................do him justice, at least there.