Congo DRC: Waasi wa Mai Mai wawateka madereva 8 wa Tanzania, wanataka $ 4,000 kwa kila Dereva

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
lori.jpg

Magari yaliyochomwa moto

Maimai1.jpg

Mai Mai rebel soldiers

Tumezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics Mzee Azim Dewji amethibitisha taarifa hizi na tayari tumezungumza na balozi wa Tanzania DRC pamoja na wizara ya mambo ya nje tayari serikali inashughulikia swala hili. Jumla ya gari zilizotekwa ni 12 kati ya hizo gari 8 za Tanzania na 4 za Kenya.

Gari 4 za Tanzania zimechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete kilometer 30 kutoka mji wa Namoya.

Tunawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao wasitishe safari ili kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Tutazidi kuwapatia update information.



KUNA TAARIFA KUWA waasi wa Mai Mai wamewateka madereva wa Tanzania watano na kuchoma baadhi ya magari. Wanadai usd 4000 kwa kila Dereva amasivyo watawapiga risasi. Wametoa deadline ya majeshi kuondoka pia.

Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

ACT Wazalendo yaitaka serikali itoe tamko kutekwa kwa watanzania DRC

TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI ITOE TAMKO KUTEKWA KWA WATANZANIA NCHINI CONGO

CHAMA Cha ACT Wazalendo, kimepokea kwa mstuko taarifa ya kutekwa kwa Magari 12 ya kusafirisha Mizigo yaliyokuwa safarini nchini Congo

Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha wamiliki wa Malori Tanzania(TATOA) iliyomnukuu mmoja wa wamiliki wa malori hayo Azim Dewji wa Kampuni ya Simba Logistic ,imeeleza kuwa kati ya magari hayo 12 magari manane(8) ni za kitanzania na yaliyobaki ni kutoka Kenya na kwamba gari nne za Kitanzania tayari zimechomwa moto huku madereva wakiwa wamechukuliwa na waasi

Kwamba tukio hilo limetokea sehemu inayoitwa Kasebebena na Matete ambayo ni kilometa 30 kutoka mji wa Namoya huku madereva wawili wa kitanzania walioshikiliwa mateka wakifanikiwa kutoroka

Kwa nafasi yetu ya Chama ambayo moja ya malengo makuu ni kuhakikisha watanzania wanakuwa salama popote waendapo, tunaitaka serikali ya jamhuri ya Muuungano wa Tanzania itoe taarifa rasmi juu ya tukio hili na iseme inachuka hatua gani kuhakikisha watanzania wanarudi salama

Pia tunaitaka serikali kuwahakikishia ulinzi watanzania wote walio katika nchi mbali mbali zinazokabiliwa na migogoro ya ndani kabla ya madhara makubwa hayajawakuta katika maeneo hayo

John Patric Mbozu

Katibu Mambo ya Nje

ACT Wazalendo.

15 septemba 2016

KAULI YA SERIKALI YA TANZANIA:



Serikali imesema kuwa inashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhakikisha kuwa madereva wanaoendesha magari aina ya malori ambao wametekwa nyara jana na waasi wa kikundi cha Maimai katika eneo la Namoyo jimbo la Kivu kusini katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanapatikana wakiwa salama.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuwakoa watanzania waliotekwa nyara.

“Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Kongo inaendelea kufanya kila jitihada kuhakikisha madereva hao wanaachiwa huru haraka iwezekanavyo na kurudishwa nchini wakiwa salama”

“Waasi hao wa Maimai wametoa masaa 24 hadi kufikia leo wawe wamelipwa kiasi cha Dola 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia huru na kutishia kuwadhuru endapo hawatapata fedha hizo, hivyo basi Serikali imeendelea kuwa na mazungumzo na Serikali ya Kongo ili kupata ufumbuzi wa suala hili” alisema Kasiga

Aliongeza kuwa malori yaliyotekwa nyara ni 12 kati ya hayo nane ni mali ya mfanyabiashara wa kitanzania Bw. Azim Dewji na mengine ni mali za wafanyabiashara kutoka nchini Kenya.

Aidha, Serikali imewataka watanzania kufahamu hali ya usalama wa nchi wanazokwenda ili kujikinga na matatizo mbalimbali yanayoweza kuwapata wakiwa katika nchi hizo.

Mjadala zaidi soma=>Watanzania waliokuwa wametekwa Congo waokolewa
 
Yule mkuu mmoja wa jeshi alishawahi kusema "saddism is inevitable" sasa hapa ndio mahala pake pakusaidia raia na sio ukatili kwa wasio makatili..
 
Back
Top Bottom