Elections 2010 CONFIRMED: Vunjo ni ya Mrema Augustine!

Vunjo ni Mrema tena. si alimpigia debe rafikie Kikwete, wapinzani njaa kweli kweli. Mtikila yupo wapi
 
Vunjo ni Mrema tena. si alimpigia debe rafikie Kikwete, wapinzani njaa kweli kweli. Mtikila yupo wapi

Bado naamini kuwa Mrema ni mwanachama hai wa CCM. haiwezekani mwenyekiti wa Taifa wa chama kilichosimamisha mgombea ukampigia kampeni mgombea wa chama kingine. Ina maana yeye mwenyewe hajiungi mkono!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hakuna mpinzani, baada ya Maalim kukubali tende, tumegundua wote wanaganga njaa tuu.
 
Ni kweli Mtikila ziii kabisa. Hajasikika sana wakati wote wa kampeni. Labda anaandaa kesi nyingine ya kupeleka mahakamani..!
 
Maalim wenu kalishwa HALUWA toka Arabuni mwenyewe kakubali, usifanye mzaha na TENDE NA HALUWA toka Oman:smile-big::smile-big:
 
Vunjo ni Mrema tena. si alimpigia debe rafikie Kikwete, wapinzani njaa kweli kweli. Mtikila yupo wapi

Ingawa ni upinzani ila huyu jaama ninahisi ni CCM na amechoka kweli labda wamemuoneo huruma tu maana wala hakuwa na hoja ya maana
zaidi ya kuipigia debe CCM haswa kikwete
 
:evil: Lyatonga ashinda kwa kishindo.....kama enzi zake za miaka ya 1995....huyu jamaa bado hajafulia kabisa kisiasa!!!!
 
hakuna mpinzani, baada ya maalim kukubali tende, tumegundua wote wanaganga njaa tuu.

dalili zilionekana mapema. Alishasema "hata mkimchagua dr. Shein niko tayari kushirikiana naye". Alishajua kuwa saa inakimbilia kumi na mbili za jioni hivyo walau aambulie umakamu wa rais. Wahenga hawakukosea kuwa penye udhia penyeza rupia!
 
pamoja na ushindi huo, mrema kafulia tu. hana lolote jipya mle bungeni. isitoshe kwa mwenendo wake wa sasa, huyu jamaa anaingia bungeni kuiongezea nguvu ccm tu. hana lolote jipya.
 
Naamini kambi ya upinzani bungeni haitamkaribisha Mrema kujiunga nayo kwasababu ni Kibaraka na hata huko vunjo watakuwa wamempa kura za huruma kutokana na kudhoofika kwake.Sioni kama anaweza kumvutia mtu yoyote kwa sera na hoja kwasasa!
 
I would say CCM wameshinda kupitia Mrema. Na anaweza asiwe anahudhuria vikao vya bunge mara kwa mara, afya mgogoro sana.
 
Nadhani wengi hapa mnaandika kwa kudhani sio kwa kumjua Mrema. Kufanya kazi serekalini sio lazima uwe kibaraka. Unaposema hana jipya si kuelewi, kama unamjua, ameshakuja na mapya mangapi na hao wengine wana mapya gani. Tusifate mkumbo tuandike tuliyo na uhakika nayo.
 
Back
Top Bottom