Confirmed: No DECI Refunds

Kwakweli wahindi hawa wamechangia sana kutufanya wazawa masikini.lakini,walitumia UDHAIFU WA WASOMI WACHACHE WAZAWA,walioko madarakani.
 
Sina shaka Sophia Simba na George Mkuchika wamesoma hii na sana wamemuelewa Reginald Mengi alipozungumzia 'mafisadi papa'. Hapa hatuzungumzii wahindi bali mafisadi! Jamani Watz tutaendelea kuwachekea mafisadi hawa mpaka lini? Hivi tumekuwa mataahira kiasi hiki? Tunapaswa kuamka na kusema 'sasa imetosha'!
Big up sana,tukiongezeka tutatosha kuilinda nchi yetu.
 
Artist Sant sana kwa hoja kali
Nimeisoma naona hasira zimenipanda na ungeona ninavyotaipu hapa we acha tu.

Kama ushahidi wa kimazingira uko wazi hivi, dola inangoja nini kuchukua hatua?
Dola isha tekwa siku nyingi dugu Sanii, jua hiyo? Habana dola tena hapa; kiongozi moja moja dani ya fuko ya fisadi. Ona hiyo? Tafanya nini bana! Fisadi kisa nunua yeye ote!
 
Artist Sant sana kwa hoja kali
Nimeisoma naona hasira zimenipanda na ungeona ninavyotaipu hapa we acha tu.

Kama ushahidi wa kimazingira uko wazi hivi, dola inangoja nini kuchukua hatua?[/QUOTE]

Kuna dola hapa in the real sense? Hapa kuna genge la wahuni tu wanaokesha kuwaza namna ya kutuibia na kujitajirisha wao.
 
Kama ushahidi wa kimazingira uko wazi hivi, dola inangoja nini kuchukua hatua?

Kuna dola hapa in the real sense? Hapa kuna genge la wahuni tu wanaokesha kuwaza namna ya kutuibia na kujitajirisha wao.

Wananchi wapo? kwanini wasichukue hatua? mbona ipo wazi kwamba Serikali a.k.a dola haipo au imelala. Tukiendelea kusubiri dola kutakuchwa.
 
Akija hapa Fundi Mchundo na Pundamilia na kaka yao GT, mtapewa habari zenu kwa kuwashambulia WAHINDI.

Mie nikija pata nafasi waanze kabisa Kujiandaa kuwekwa ndani na atayewatoa, walahi yeye na familia yake wata................... (Mods watanilima barua nikimalizia).

Wahindi ni Vibaka tu na dawa yao ni ileile kama ya Vibaka wa mitaani. Siku moja yatatimia.
 
Artist Sant sana kwa hoja kali
Nimeisoma naona hasira zimenipanda na ungeona ninavyotaipu hapa we acha tu.

Kama ushahidi wa kimazingira uko wazi hivi, dola inangoja nini kuchukua hatua?[/QUOTE]

Kuna dola hapa in the real sense? Hapa kuna genge la wahuni tu wanaokesha kuwaza namna ya kutuibia na kujitajirisha wao.

Hili saksta la huyo Chavda nililisikia bungeni hiyo miaka ya 90s akafukuzwa nchini badala ya kufilisiwa na kushtakiwa pamoja na washirika wake leo hii kuna chavda aliyekuja nchini kwa mgongo wa subash kama muajiriwa wake na sasa ni contractor wa kujitegemea najaribu kuunganisha uhusiano wa hao wahindi wawili kitendo walicho kitendea nchi na kama chavda aliyeko tz ni huyohuyo anaezungumziwa we are not serious, serikali ni ya watu walewale waliomtimua Mrema anaetajwa kulivalia njuga sakata hilo pamoja na vitisho vya kuwashtaki wanao fichua maovu yao, hapo mna tegemea nini? Si shamba la bibi bwana.
 
Ndugu zanguni najua wengi tumeshaanza kushahu mapenzi na machungu ya DECI kwa yaliyotukuta hivyo basi leo hii nimeona tuendelee kupeana moyo kwamba pamoja na DECI kuchukua akili zetu na mali zetu tuendelee kuamini vile vile bado maisha yapo baada ya DECI

L a maana tuwe makini tena kwenye asasi kama hizi tusikimbilie pesa za kukaa chumbani....asiefanya kazi na asile hivyo tujitayarishe kwa maisha mapya ya kufanya kazi tuweze kupata kipato cha kila siku.....

Mungu atusaidie kufanikiwa katika maisha haya mapya.....
 
Mimi naona watu hawajakoma, kuna wengine bado wanaweka kwenye taasisi hizi za kuvuna, Juzi j'mosi nilikuwa kwenye benki moja kwenye desk la kujaza form nimekaa na dada mmoja na yeye anajaza ya kwake ya kudeposit, anadeposit shilingi laki mbili kwenye taasisi inaitwa Matoponi Network na yenyewe ni design ya desi nilishawahi kuisikia.

Kwa hiyo maisha baada ya desi ni desi nyingine nyingi za chini chini mpaka zigundulike watu wameishaliwa.
 
Wanachama upatu wa Deci wataka kukutanishwa na tume ya serikali
Mmoja wa mamia ya wanachama wa upatu uitwao Deci waliokutanika Dar es Salaam ii kushinikiza kukutana na kamati ya serikali inayofuatilia kisa cha ushirika wa kupanda na kuvuna mbegu (fedha), ambao shughuli zake zimesitishwa na serikali.
Fidelis Butahe na Simon Simalenga

WASHIRIKI wa mchezo wa upatu unaoendeshwa na taasisi ya Development of Entrepreneurship for Community Initiative (Deci), jana walicharuka na kuzingira ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo wakishinikiza wakutanishwe na tume iliyoundwa na serikali kuichunguza taasisi hiyo.

Serikali ilitangaza kusitisha shughuli zote za Deci, ikiwa ni pamoja na kuzuia akaunti zote na kuitaka iorodheshe upya majina ya washiriki wake kwa ajili ya kuwarejeshea fedha walizowekeza.

Lakini subira imeonekana haivuti heri kwa washiriki wa mchezo huo, maarufu kama "Kupanda na Kuvuna Mbegu" na tangu wiki iliyopita wamekuwa wakipanga kukutana kwenye ofisi za taasisi hiyo zilizo Mabibo jijini Dar es salaam kwa lengo la kushinikiza kuharakishwa kwa malipo yao.

Jana washiriki hao walijazana nje ya jengo la ofisi hiyo ambalo walidai kuwa limeshakabidhiwa kwa mmiliki wake kwa kile walichoeleza kuwa Deci imeshindwa kulipa fedha ya pango.

Mkusanyiko huo ulisababisha baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo kuamua kuzungumza na washiriki hao ili kuwatuliza.

Akizungumza kwa upole, mmoja wa wakurugenzi wa Deci, Dominick Kigendi alisema kuwa zoezi la kuichunguza taasisi hiyo ni zito kwa sababu taasisi hiyo ina washiriki 700,000 hivyo aliwataka washiriki kuwa wavumilivu mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.

“Wiki iliyopita walikuja washiriki na kuomba kujua hatima ya fedha zao, niliwaambia waandike majina na niliwaambia waje leo (jana) ili kupata majibu," alisema Kigendi.

"Sasa nawajibu kama ifuatavyo; uchunguzi bado unaendelea na si rahisi kutoa majibu kwa sasa.

“Serikali imewaomba muwe watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati uchunguzi unaendelea. Deci ipo karibu sana na tume iliyoundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi hivyo mambo yakikamilika taarifa mtazipata. Nawatakieni kila la kheri katika uvumilivu wenu.”

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Timoth ole Loitingy’e aliwaambia washiriki hao kuwa fedha zao zipo, lakini wataitaarifu serikali ifanye haraka katika uchunguzi huo ili kuondoa usumbufu kwa kuwa inaonekana wazi washiriki wamechoka kusubiri.

Hata hivyo, kauli ya Kigendi ilionekana kuwakera washiriki hao na kujaa jazba. Washiriki wawili waliopewa nafasi ya kuuliza maswali, walisema hivi sasa uvumilivu umewashinda na kusisitiza kuwa lolote linaweza kutokea.

“Tunachokitaka ni kukutanishwa na hiyo tume iliyoundwa kwa ajili ya kuichunguza Deci ili itueleze huo uchunguzi utakamilika lini na tutaanza kurejeshewa fedha zetu siku gani,” alisema Abdalah Said.

Naye Lucas John alisema kuwa serikali ilitakiwa kutoifungia Deci badala yake ingeiamuru kwanza iwarejeshee fedha washiriki.

Lakini, Kigendi alijibu hoja hizo kwa kueleza kuwa maswali waliyouliza yataandikwa na kusomwa kwenye vyombo vya habari, hivyo wahusika watayaona na kuyafanyia kazi.

“Maswali nimeyasikia lakini kuna vyombo vya habari hapa vitayaandika na yatasomwa na wahusika,” alisema Kagendi na kuingia ndani huku akiwaacha washiriki hao wakiwa bado hawajajua hatima yao.

Akizungumza na Mwananchi, mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na washiriki hao Deci kwa ajili ya kufuatilia kwa ukaribu urejeshwaji wa fedha zao, Mchungaji Isaack Kalenge alisema kuna siri nzito kati ya viongozi wa Deci na serikali.

Kalenge, ambaye aliwahi kukamatwa na polisi na baadaye kuachiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa akichochea vurugu, alisema kuwa viongozi wa Deci si wakweli akidai kuwa hawawaelezi ukweli washiriki.

“Unajua sisi tunazungumza karibu kila wiki na viongozi wa Deci, lakini tunachozungumza nao sio wanachokisema wanapokuwa wakizungumza na washiriki. Hilo linatupa wasiwasi sana, tukiamua kusema tunachozungumza nao, hapa patakuwa hapatoshi,” alisema Kalenge.

“Nadhani kuna kitu kinaendelea kati ya Deci na serikali... kuna mchezo unachezwa hapa, kulikuwa hakuna sababu ya kuzuia fedha za wananchi, kwanza hata hiyo tume iliyoundwa kuchunguza Deci hatuna imani nayo. Kinachofanyika hapa ni kupoteza muda tu.”

Alisema kuwa walikuwa wamepanga kuishitaki Deci, lakini uongozi wa taasisi hiyo uliwaomba kutolipeleka suala hilo mahakamani na badala yake wakae na kuzungumza ili kuweza kupata ufumbuzi wa suala lao.

“Nafiriki hawa jamaa hivi sasa wanaleta ‘usanii’, tutakaa na kujadili suala hili kwa pamoja kama kamati. Tukiafikiana tutakwenda mahakamani. Wanaonekana wanataka kupoteza muda tu kwa kujifanya wanazungumza na sisi kumbe kuna mipango wanayoipanga,” alisema Karenge.

Wiki iliyopita Waziri wa Fedha na Uchumi aliliambia Mwananchi kuwa kinachosubiriwa hivi sasa ni ripoti ya tume iliyoundwa kuichunguza taasisi hiyo ambayo inaongozwa na mkurugenzi wa makosa ya jinai, Robert Manumba.
 
SAKATA la Kampuni ya Upatu ya DECI limechukua sura mpya baada ya wanachama wake kuigeukia Serikali na kupanga maandamano makubwa kushinikiza kutoa hatima ya mbegu zao walizoahidiwa kuvuna mwanzoni mwa mwezi huu.

Hali hiyo iliibuka baada ya viongozi wa DECI kuwaeleza wanachama waliokusanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mabibo, Dar es Salaam jana kuwa kwa sasa hawana chochote cha kufanya kwani Serikali imeshikilia hatma ya fedha zao, hatua iliyosababisha hata mmiliki wa jengo la ofisi, kutakanyumba yake kutokana na DECI kushindwa kulipa pango.

Akizungumza na wanachama hao, Mkurugenzi wa DECI, Bw.Timoth Ole Loiting'ye, alisema hawana lolote la kuwaambia wanachama hao isipokuwa Serikali kupitia Tume iliyoundwa, ndiyo inawajibu wa kutafuta suluhisho kwani hata wao hawana fedha hata fedha za mafuta ya magari yao.

"Tumefurahi mmefika ili mjue kinachoendelea lakini sisi hatuna cha kuwaeleza bali tutafikisha taarifa zenu kwa wahusika ambao ni Tume iliyoundwa, Tume hii ina watu muhimu wakiwemo Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo, IGP Said Mwema na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT),alieleza Bw.Loiting'ye

Baada ya maelezo hayo, wanachama hao walionesha kukerwa na hatua hiyo ya Serikali kuzidi kuwaacha gizani hadi sasa, kinyume na taarifa zilizotolewa awali kwamba mbegu hizo zingeanza kurudishwa mapema mwezi huu.

Walitoa maneno makali kuilamu Serikali kwamba badala ya kutatua tatizo lao, imegeuka na kuwakandamiza na kuwa kikwazo kupata fedha zao.

"Kwanini wanachama tusikutane na hiyo Tume iliyoundwa badala yake wanatufanyia ubabaishaji, hii amani inayoonekana hapa itavunjika muda wowote kuanzia sasa, sisi hatuondoki hapa mpaka kieleweke kwani mambo yetu mengi yamesimama kwa sababu ya huu ubabaishaji!" alilalamika mmoja wa wanachama hao.

Wanachama hao waliamua kubaki eneo la ofisi hizo kwa saa 3 baada ya viongozi kumaliza mkutano huo na baadaye kuamua kwenda kuandamana kwenda kwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila kutaka muongozo wa kuandaa maandamano makubwa kesho kushinikiza Serikali kuwalipa mbegu zao.

Mchungaji Mtikila amekuwa mstari wa mbele kutetea wateja hao kupata haki zao na hivi karibuni alihutubia mkutano wa wanachama hao kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam na kueleza kuwa kufungwa DECI ni uonevu.

Maandamano hayo yamepangwa kuanzia ofisi za DECI Mabibo hadi Wizara ya Fedha na Uchumi.

Aprili mwaka huu,Serikali ilitangaza kusitisha shughuli za DECI baada ya kubaini kuwa kampuni hiyo inaendeshwa kinyume cha sheria na kuwatahadharisha wanachama wake kutoendelea kuhatarisha mitaji yao.

Naye Edmund Mihale anaripoti kuwa Mbunge wa Handeni, Dkt. Abdallah Kigoda amesemakama DECI ingefanya utaratibu mzuri katika kuendesha shughuli zake, mabenki mengi nchini yangesahaulika na kufilisika kwa watu wengi kukimbia riba kubwa.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi ya Bunge jana, Dkt. Kigoda ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo ,alisema hali hiyo inatokana na riba kubwa inayotozwa kwenye mikopo huku wateja wateja wa benki hizo wakipata faida ndogo.

"Naomba nitoe mfano mdogo lakini najua hamtaupenda nasema kama DECI ingeandaa utaratibu mzuri, wananchi wa kipato cha chini wote wangekimbilia huko na mabenki yetu yangesahaulika" alisema Dkt. Kigoda.
 
Yawezekana mbegu zao karibu zote zilianguka njian,zingine kwenye miamba. ndio maana hawavuni.

Wajaribu kukutana na hiyo kamati pengine wanaweza kutifua hiyo miamba, wakamwagilia na hatimaye kuvuna. Kwa nchi yetu ilivyo sijui kama watavuna!!!
 
Wakazi wa Dar es Salaam ambao walipanda mbegu zao katika taasisi ya DECI Mabibo wakiwa wamekusanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo jana kutaka kujua hatma ya fedha zao.
 
Sasa jamani mbegu wapande DECI huko, kisha waje waanadamane kwenda wizarani, kwani huko ndo walikopanda? Serikali inatimiza tu wajibu wake.....kufanya hima sheria, basi. kama hawajaelewa, kiongozi wao ndo anawaambia mbegu zimeoza ivo!
 
Naona mvua haikunyesha na hawakuwa wanafanya irrigation. Sasa mbegu zote zimeoza.
 
Hii inanikumbusha kisa cha Abunuasi. Huyu mjamaa siku moja alikuwa na shughuli nyumbani kwake na aliazima sufuria kubwa kwa jirari yake. Baada ya shughuli aliirudisha ile sufuria na sufuria nyengine ndogo (kwa maana kwamba ni asante ama sufuria imezaa). Siku nyengine kukawa tena na shughuli nyumbani kwake na tena akaenda kuazima sufuria ile kubwa. Baada ya shughuli kwisha, hakuirudisha sufuria kwa mwenyewe.

Mwenye sufuria alipokuja kuiulizia Abunuasi akajibu kuwa sufuria imekufa. Mwenye sufuria akaja juu vipi sufuria inakufa? Abunuasi akamjibu mbona siku ile ilipozaa hukuniuliza?

Sasa DECI inanikumbusha ujanja wa wachache.
 
Sasa ndio kusema

- hela hawarudishi kabisa?
- mbona hata hio ripoti ya Tume haieleweki imesomewa Igunga au Kkantalamba?
- mbona wale wa Elimika Scheme nasikia walirudishiwa mbegu zao (za kwao, hazikuoza)!
-mwenye taarifa za malipo (marejesho) atueleze basi

Tumechoka kuona hitimisho.....!
 
Hizo pesa za DECI zitifaishwe na serikali ziingizwe kama miradi ya JAMII kwani hata zikigawiwa hazitatosha kwa kila mkulima kwa kadri anavyodai
Lijengwe bonge la shule liitwe DECI SECONDARY
 
Back
Top Bottom