Elections 2010 CONFIRMED: Joseph Mbilinyi (CHADEMA) atangazwa rasmi Mbunge wa Mbeya mjini

Acheni uzembe, sasa huyu zero anaenda kufanyanini bungeni au kwakua ni mkristo? Waislam mnataka wasemaje

Hao unaowaona wajuzi bungeni ndio waliotuibia miaka yote hii. Kumbuka mfano uliotolewa wa msomi Dr. Balali. Sugu anawakilisha sauti ya vijana
 
Sasa huyu Mr. Zero bungeni akafanye nini?? Chadema hapo mlifuka ilitakiwa kuangalia mambo mengi kuteua mgombea. Au kisa bongo fleva??? Bunge shule vijana sio sehemu ya kwenda tu. Ok yetu macho ndo ninyi wenywewe mtakao mkana 2015.

Ndio hvyo Sugu kashinda tena kwa kishindo, imagine ni Mbeya mjini!! mtajibeba mlodhani atashindwa ...na kwa taarifa yenu kuwakilisha matatizo ya wanachi sio lazima uwe Profesa au Dk. Nyie naona mmetumwa humu kumsakama Sugu au mmekosea njia manake naona wageni humu JF, au mejiunga ili kumkosoa Sugu??...Bora SUgu mara mia kuliko hao wabunge wanaoenda kusinzia na kupitisha kila kitu bungeni... Dk Buriani na elimu yake mbona kashindwa vibaya?? Masha yupo wapi?? achilia mbali Mama Mongela aliyekuwa Bunge la Africa, wote hawakufanya chochote na ELIMU yao ndo maana wameshindwa. Tuungane kumsapoti Sugu na ikiwezekana nyie mnaoona hafai mpeni tips au vipi??Go Sugu
 
"whatch you mouth before spell out"]
Dogo acha kupiga watu mikwara,wewe ndio hujui ulinenalo.
 
Acheni uzembe, sasa huyu zero anaenda kufanyanini bungeni au kwakua ni mkristo? Waislam mnataka wasemaje

Acha uzembe wewe negative, mbona unakuwa na mawazo finyu kama nukta. watu kama nyi Hayati baba wa taifa aliwaita Nyoka. Kumbuka Udini, Rangi, Kabila ni sumu katika kujaji jambo. Badilika hayo mamba yalisha kataliwa toka enzi na enzi, wewe unayaona ya thamani leo? Think big mzeaa
 
shida iko wapi...kumpenda sana Nyerere kosa?
Obi nakuomba uondoe picha ya hayati baba wa Taifa nadhani kiungwana si busara kuiweka hapo. Zipo picha nyingi unaweza kutumia tafadhali tumia busara kuiondoa. Nadhani hata wana JF wengine wameliona hilo. Tumwache mzee wetu apumzike kwa amani.
 
Jimbo la Mbeya Mjini

UBUNGE: Joseph Mbilinyi (CHADEMA) - 46,411
Benson Mpesya (CCM) - 24,327.
nguvu ya Umma Imeongea.

Haya yametoka kutangazwa na Tume Mbeya

Tupulize vuvuzela ....... kama walivyokuwa kisema wao .......................... :director::violin:
 
Sasa huyu Mr. Zero bungeni akafanye nini?? Chadema hapo mlifuka ilitakiwa kuangalia mambo mengi kuteua mgombea. Au kisa bongo fleva??? Bunge shule vijana sio sehemu ya kwenda tu. Ok yetu macho ndo ninyi wenywewe mtakao mkana 2015.
Hii inaonyesha we ndo huna elimu kabisa. Katiba ya Tanzania imeweka sifa ya kuwa mbunge na watu wengi wanaelewa. Kama kwenda Bungeni ingekua elimu tungewakilishwa na Professors na Dr, wa pale mlimani. Kawawa alikua bungeni na hakuwa na elimu ya chuo na aliweza kuongoza kwa uadilifu. Tatizo lako ni kuwa elimu yako ndongo sana au kama una elimu basi una ulimbukeni mkubwa na elimu haikusaidii hata kidogo. Kama ingekua suala la elimu hao kina Mramba wana elimu nzuri tuu na si ndio hao wanaoiba kila siku na kufanya watu vijijini wakose madawa. Sokoine alikua na elimu gani?Acha ulimbukeni jaribu kwenda shule. Sugu anafaa sana kwenda bungeni kwa kuwa ana uzoefu na maisaha ya mtaani na atatoa changamoto nzuri tuu. Sugu ana elimu ya uraiani kubwa kuliko viongozi wenu wengi tuu wanaoenda kusinzia bungeni na kenenepesha matumbo
 
hivi huyo anaesema sugu hana shule,anajua profesa maji marefu wa korogwe ana elimu gani? Acheni upuuzi wa kudharau watu,wasomi nchi hii ndiyo waliokosa uzalendo sana.acha tuende njia tofauti sasa! hongera mh. joseph mbilinyi.
 
Kina Kibonde...na watangazaji wengine....wa Clouds...wasema chochote....walio fikiri maisha ni kuwabania geeks kama sugu sasa ngoja aingie bungeni...watamsoma...vyema....kulopoka lopoka kisa alikuwa HipHop artist sasa itabid mwamwite mheshimiwa.....Ndama hawa.
 
Sasa huyu Mr. Zero bungeni akafanye nini?? Chadema hapo mlifuka ilitakiwa kuangalia mambo mengi kuteua mgombea. Au kisa bongo fleva??? Bunge shule vijana sio sehemu ya kwenda tu. Ok yetu macho ndo ninyi wenywewe mtakao mkana 2015.

watoto wa mjengoni kitawauma saaaaaaaaana mwaka huuu mtaregister majina hapa jf mpaka muyamalize na bado sugu yupo juuuuuu kama vipi mpande mkazibeeeeeeeee THIS IS TOOOO BIG FO YOU weraaaaaaaaa weeeeeeeeeraaaaaaaaaaaaaaa
 
Sasa huyu Mr. Zero bungeni akafanye nini?? Chadema hapo mlifuka ilitakiwa kuangalia mambo mengi kuteua mgombea. Au kisa bongo fleva??? Bunge shule vijana sio sehemu ya kwenda tu. Ok yetu macho ndo ninyi wenywewe mtakao mkana 2015.

tunampenda huyo huyo 'zero' lakini ni muadilifu na mpiganaji. Anayeweza kutetea watu wake. Labda tumbadilishe na wewe BOGASI
 
Back
Top Bottom