mtozwaushuru
Member
- Sep 20, 2010
- 86
- 12
siyo wanataka kuchakachua ila hapo ndo wamechakachua mwisho wa uwezo wao kupunguza aibu yao. Naamini the gap was three times bigger before the mchakachuo exercise. We kazi ya cku mbili mchezo!
Hongeara Mbunge wangu Halima Mdee, nilikuwa nasubiri kwa hamu matokeo ya jimbo langu la Kawe
Jamani nitoeni ushamba hivyo malaria sugu ndo nini?
CUF wangehitaji umoja wa wapinzani wasingeipa CCM Ubunge wa Tarime maana CCM ni kura 28600+ na CHADEMA 27300+ na CUF na NCCR @ 7000+ hivyo CUF ndo wamewapa CCM ushindi.Toba !! Yamekuwa haya!!
Ndugu yangu, mbona pongezi zimetolewa saana? N aunajua nini? CUF haiamniki tena, maana hiyo imeshakuwa ni CCM B, wameamua kula na mafisadi.
Hivi huku bara cuf walikuwa na viti vya majimboni vingapi?? au ndo vile vya kuteuliwa unavyoviongelea???
Aisee hii Artemether injection imemsababishia ndugu yangu shida sana. Nakupataje unisaidie?Kimsingi katika mfumo wa Tiba Hakuna Kitu Kinachoitwa Malaria Sugu (Chronic Malaria) bali Kuna Malaria ( Kali)- Complicated Malaria ambayo kwa Mfano imehusisha Ubongo na pengine figo (Renal Failure).
Malaria siyo Chronic Disease kwani Huua kwa Haraka. Ili Ugonjwa uwe sugu...au Chronic maranyingi ni kwamba japo unaweza kuleta Madhara chini ya wiki 2 lakini angalau mtu anaweza kukaa nao kwa zaidi ya wiki 2 au pendine unajirudia rudia mfano Ugonjwa wa Masikio -Chronic Otitis Media.
Malaria kama nilivyosema yaweza kuwa ile ambayo haijachanganya sana (Uncomplicated Malaria) Au iliyochanganya na kuonyesha dalili za hatari kama kupoteza fahamu, Degedege (Hasa kwa Watoto),Kuchanganyikiwa n.k na hii inaitwa Complicated Malaria ...KWA HIYO HAKUNA MALARIA SUGU katika mfumo wa Magonjwa
Hata ukuiangalia Kijiografia Kuna Endemic Malaria areas-Yaani Sehemu ambapo kuna mbu wengi wa Malaria na kwamba watu wanaugua Malaria mara kwa Mara. 'Epidemic Malaria' siyo Common sana kwani kama Africa Malaria ni 'Endemic' toka nasomea mambo haya sijawahi kuona sehemu yenye 'Outbreak' or 'Epidemic' au kwa Kiswahili Mlipuko wa Ugonjwa Wa Malaria
Ukija Katika Dawa.. Wadudu wa Malaria (Plasmodium) wanaweza Kujenga Ukinzani/Usugu dhidi ya Dawa ya Malaria kama vile Fansider au Chloroquine kuna wadudu wengi wamejenga Ukinzani(Resistance) ..Lakini Plasmodium Kujenga ukinzani (Resistance) kwa dawa hatuwezi kusema ni MALARIA SUGU labda usema PLASMODIUM SUGU,kwa kuwa kinachoongelewa hapa ni Vimelea vya Malaria na siyo Malaria Yenyewe na Japo Plasmodium wanaweza kuonyesha resistance bado Kuna Dawa zinaweza kuwaua kwa mfano IV Quinine na Artemether Injection. Na Vimelea (Plasmodium) vya Malaria ni Tofauti sana na Ugonjwa wa Malaria.
Mfano mwingine ni UKIMWI na VVU. Virusi vya Ukimwi vinaweza kujenga ukinzani dhidi ya ARV lakini hauwezi kusema mtu ana UKIMWI Sugu!
Kwa hiyo mwana JF 'Malaria Sugu' kama anataka kujenga Maana ajiite 'Plasmodium Sugu'
Tuwasiliane kama Hujaelewa