Confessions of an unfaithful husband

Mke wangu mpendwa!
Nimekuwa nikiandamwa na msongo wa mawazo siku za karibuni kwa kuwa sasa nadhani nimefikia mwisho sina budi kukueleza aina ya mume uliyekubali kuwa naye hadi mungu atakapo tutenganisha. Najua wewe ni mpole na mvumilivu lakini ninayokwenda kuyasema ni mazito sana kwa moyo wa mwanadamu hivyo usinionee huruma kwa uamuzi utakao uchukua kwani tayari nimeukubali kabla sijaujua. Sijajua kosa ulilolifanya hadi kupewa adhabu ya mume kama mimi ila ninaamini aliyekuadhibu akiyasikia haya basi atakuandalia pepo yako mbinguni kwa kuwa umekwisha onja kiama hapa duniani, mke wangu:-

1. Yule mtoto wa shangazi yako ninayemsomesha sifanyi hayo kwa mapenzi yangu kwako bali ninaficha ubaya tunaokufanyia, nimekuwa na uhusiano usiofaa na binti huyu tangu alipovunja ungo, miaka nane iliyopita.
2. Msichana wa kazi uliyemfukuza kwa kuwa na ujauzito tukagombana sana na nilikuita majina yote mabaya ni kwa kuwa nilikuwa najaribu kumlinda kwa kuwa sikuwa na uhakika kama hiyo mimba hainihusu kwa kuwa nimetembea naye miezi ile miwili uliyokwenda mafunzo south africa.
3. Nyumba unayoisifia sana aliyopanga shoga yako Suzzy wa Sinza, ninalipia mimi kodi na nimekuwa na uhusiano wa siri na rafiki yako Suzzy tangu mkiwa pamoja chuo kikuu.
4. Ugomvi mara kwa mara ndani ya nyumba yetu mara zote huwa naupanga ili kuficha maovu yangu.
5. Mke wangu sijawaji kukumbuka birthday yako hata siku moja ila ninaambiwa na rafiki yako Suzzy.
6. Hata tabia ya kwenda Bar si kwa sababu ya kukutana na marafiki bali ni tabia yangu mbaya ya kupenda kuwashika shika makalio na matiti ma bar maid.
7. Kinachonipeleka salon kufanya scrub si usafi mke wangu bali ni tamaa ya kushikwa shikwa na kutekenywa na wasichana wadogo wa salon, hii ndio sababu mara zote unaponunu dawa za scrub nyumbani nazipoteza au nasingizia zinanitoa chunusi.
8. Mke wangu mimi sio shabiki kabisa wa mpira bali huwa nasingizia kupenda ili nilpate uhuru wa kutumia muda mwingi nje ya nyumbani.
9. Mke wangu yule personal trainer wa gym nilimuajiri pia kukuangalia, kukuchunguza na pia kukujaribu ili nipate visingizio vya kukuacha tangu miaka miwili iliyopita lakini sikufanikiwa na alichoniambia ndicho kimenifikisha kwenye ungamo hili.
10. Mke wangu pete yangu ya harusi haikupotea bali niliigawa kwa rafiki yako Suzzy siku ya pili baada ya ndoa kama ishara ya kuendela na pembe tatu yetu hii.

Najua sistahili kusamehewa na kwa hilo sitakupa mzigo tena kwani ninajua umekuwa ni zaidi ya mke kwangu bali ni mlezi, kiongozi na mlinzi wa nyumba yetu.
Ni mimi
Mumeo Mkosefu.

Kaka umenikumbusha wimbo wa Lady Jay Dee ft MwanaFA. Suruali zinanivuka kila nikiona binti.... (Hajui tulikoka Lady Jay Dee, ft MwanaFA)
 
loh nahisi hukufaa kuoa ulitakiwa ubaki mseja for the rest of your life ili ufanye yoote unayoyapenda ya kibazazi
 
Nadhani hata confession ni njia ya kumtia hasira mkewe ili adai talaka maana katafuta kila sababu kakosa so hii ni silaha yake ya mwisho.
 
Kuna wengi tu wanaofanya hayo ila hamna hata mmoja mwenye ubavu wa kutubu hata ashikiwe pisto au akamatwe live. Kuna mdada alikuwa amekodi kwa wazazi wangu kwa ajili ya biashara; mdada alikuwa na magari mawili tena ya maana. Sasa sijuhi shule ndogo unakuta yuko kijiweni anasimulia jinsi anavyotunzwa na mume wa mtu by then alikuwa na ujauzito. Sasa mimi nikamuuliza huyo mwanaume watoto wake si watakuwa wanalala njaa maana naona pesa yote inaishia kwako. Akanijibu the man has money; mkewe anatembelea benzi kwa hiyo wala si rahisi wife kumshtukia. Akaendelea kutamba kuwa hata safari za kikazi nje ya nchi most of the time anaenda na yeye na si wife, na hiyo biashara jamaa ndiye kamlazimisha afanye (because yeye kama yeye haoni kwa nini ateseke na kutafuta pesa huku jamaa anamwagia za kutosha). Yani roho huwa inaniuma utadhani namjua huyo wife. Ukiwa na mume mwenye pesa kazi; ukiolewa na masikini kazi.
 
Mke wangu mpendwa!
Nimekuwa nikiandamwa na msongo wa mawazo siku za karibuni kwa kuwa sasa nadhani nimefikia mwisho sina budi kukueleza aina ya mume uliyekubali kuwa naye hadi mungu atakapo tutenganisha. Najua wewe ni mpole na mvumilivu lakini ninayokwenda kuyasema ni mazito sana kwa moyo wa mwanadamu hivyo usinionee huruma kwa uamuzi utakao uchukua kwani tayari nimeukubali kabla sijaujua. Sijajua kosa ulilolifanya hadi kupewa adhabu ya mume kama mimi ila ninaamini aliyekuadhibu akiyasikia haya basi atakuandalia pepo yako mbinguni kwa kuwa umekwisha onja kiama hapa duniani, mke wangu:-

1. Yule mtoto wa shangazi yako ninayemsomesha sifanyi hayo kwa mapenzi yangu kwako bali ninaficha ubaya tunaokufanyia, nimekuwa na uhusiano usiofaa na binti huyu tangu alipovunja ungo, miaka nane iliyopita.
2. Msichana wa kazi uliyemfukuza kwa kuwa na ujauzito tukagombana sana na nilikuita majina yote mabaya ni kwa kuwa nilikuwa najaribu kumlinda kwa kuwa sikuwa na uhakika kama hiyo mimba hainihusu kwa kuwa nimetembea naye miezi ile miwili uliyokwenda mafunzo south africa.
3. Nyumba unayoisifia sana aliyopanga shoga yako Suzzy wa Sinza, ninalipia mimi kodi na nimekuwa na uhusiano wa siri na rafiki yako Suzzy tangu mkiwa pamoja chuo kikuu.
4. Ugomvi mara kwa mara ndani ya nyumba yetu mara zote huwa naupanga ili kuficha maovu yangu.
5. Mke wangu sijawaji kukumbuka birthday yako hata siku moja ila ninaambiwa na rafiki yako Suzzy.
6. Hata tabia ya kwenda Bar si kwa sababu ya kukutana na marafiki bali ni tabia yangu mbaya ya kupenda kuwashika shika makalio na matiti ma bar maid.
7. Kinachonipeleka salon kufanya scrub si usafi mke wangu bali ni tamaa ya kushikwa shikwa na kutekenywa na wasichana wadogo wa salon, hii ndio sababu mara zote unaponunu dawa za scrub nyumbani nazipoteza au nasingizia zinanitoa chunusi.
8. Mke wangu mimi sio shabiki kabisa wa mpira bali huwa nasingizia kupenda ili nilpate uhuru wa kutumia muda mwingi nje ya nyumbani.
9. Mke wangu yule personal trainer wa gym nilimuajiri pia kukuangalia, kukuchunguza na pia kukujaribu ili nipate visingizio vya kukuacha tangu miaka miwili iliyopita lakini sikufanikiwa na alichoniambia ndicho kimenifikisha kwenye ungamo hili.
10. Mke wangu pete yangu ya harusi haikupotea bali niliigawa kwa rafiki yako Suzzy siku ya pili baada ya ndoa kama ishara ya kuendela na pembe tatu yetu hii.

Najua sistahili kusamehewa na kwa hilo sitakupa mzigo tena kwani ninajua umekuwa ni zaidi ya mke kwangu bali ni mlezi, kiongozi na mlinzi wa nyumba yetu.
Ni mimi
Mumeo Mkosefu.

Mume wangu Mpendwa...

Cha ajabu nyie wanaume tuki kaa kimya mnafikiri hatujui nini kinatendeka... Mara zoote na mara nyingi ulikua unafanya hivo na nikawa navumilia sababu mimi personally hujawahi nifanyia visa vya moja kwa moja na apart from hayo makosa you are a good husband. Hata hivyo niliona bora tu nivumile maana hata mimi ni mkosefu kwako...

  1. Yule First born wetu ambae alizaliwa immature - hakua immature ile mimba ilitimiza miezi tisa ila tu nilificha kua tulipokutana nilikua na uja uzito tayari... Hivo mtoto umpendae kuliko woote na ni wa kiume pekee sio wako.
  2. Suzy namfahamu kabla yako... tabia yake ndio hio hio ya kuparamia waume za watu - hivo nilijua kabisa kua utaingia katika anga zake, nikaona ni bora uwe na mwanamke ambae nitaweza fuata nyendo zako kuliko nisiemjua, ndio sababu ya kusifia sifia ile nyumba nikiamini kua labda utasema kweli.... naona ukawa unakwepa.
  3. Naelewa mambo ya Saloon huko.... maana hata mimi wale vijana wananifanyia Pedicure na Manicure... hua wananifaa kwa mengi... after all ukitoka kwa Suzy huwezi kitu - huwezi nilaumu, maana wewe sio lijali kiasi hicho...
  4. Mimi hua sijali kabisa ukienda mpirani au bar... kweli ukishinda nyumbani ni mpaka tugombane, hivo ukija zako umechelewa ni furaha kwangu na hua najifanya nimechoka mno ili tu usiniguse, nakua sina hamu nawewe...
  5. Sie kwetu kakaa kwa mume ni heshima kweli.... huoni ninavo heshimiwa kwetu tukienda kuliko wale wenzangu ambao ndoa zimewashinda?? Basi wala usijali...
  6. Yule mtoto unasomesha nyumbani sio wa shangazi - sema kalelewa tu na shangazi ni siri ndani ya familia, nilipata mimba nikiwa na miaka kuminasita hivo shangazi akanipolea, akanipanja ufyele na kum adopt mtoto maana kipindi hicho ilikua aibu mno...
Hivo usijali kabisa mume wangu wewe ni mkosefu kama mimi pia... Hivo tuendelee kuvumiliana.

Mkeo Mkosefu...
 
Yule mtoto unasomesha nyumbani sio wa shangazi - sema kalelewa tu na shangazi ni siri ndani ya familia, nilipata mimba nikiwa na miaka kuminasita hivo shangazi akanipolea, akanipanja ufyele na kum adopt mtoto maana kipindi hicho ilikua aibu mno....
Hii kali kuliko zote, naweza kujinyonga kama mungu hakutaka kuning'oa kwa heart attack.
 
Ni mzaha uliojaa ukweli mtupu ndani yakehaya mabo yapo! mkaubali mkatae.........Mungu atupatie ujasiri wa kutubu...............
 
Ni mzaha uliojaa ukweli mtupu ndani yakehaya mabo yapo! mkaubali mkatae.........Mungu atupatie ujasiri wa kutubu...............

Matendo sio mzaha... mzaha ni kua waweza andika hio barua ukampelekea wife??? Kweli hata uni convice sikubali labda kama mpango ni kukuacha.
 
It takes grt courage to tell the one you ''call your wife'' those things. Anyway congs and i hope you are going to change aftr that. God be with you
 
duh hili ni zaidi ya pepo la ngono,bado nakufikiria,maana mke wako namsikitikia
 
duh hili ni zaidi ya pepo la ngono,

Kwa nini tuna msingizia pepo? mimi nakili huu wote ni udhaifu wangu binafsi na sitaki kumsingizia pepo, nitasubiri hatma yangu na nitaubeba msalaba wangu bila kumsingizia pepo.
 
Back
Top Bottom