Condom(s) wakati wa Safari

chloe.obrain

JF-Expert Member
Feb 25, 2010
391
20
habari zenu great thinkaz!!!

Jamani dada/mama aliyeolewa au anayeishi na mwanaume kama mume na mke naomba kuuliza, Je ni vema kumwekea mumeo Kinga i mean Condoms kwenye begi anaposafiri kwenda mbali either kikazi,kibiashara au vyovyote ilimradi atakuwa mbali nawe kwa muda???

Kwa kaka/baba aliyeoa au anayeishi na mwanamke kama mume na mke, utajisikiaje mkeo/huyo unayeishi naye akikuwekea condom kwenye begi wakati unasafiri and what will you tell her???

Tujadili jamani!!
 
Sitamwambia kitu, nitarudi nazo zote bila kuzitumia......
Ofkoz, nitanunua nyingine kwa matumizi yangu....ila hicho kitendo kinaongea kwa sauti kubwa sana!
 
Ni ngumu hiyo. Je jamaa akirudi kutoka safari na hana, si mtu unaweza kuchanganyikiwa?
Muhimu hata kukumbushiana kuhusu wajibu wa kila mmoja juu ya kulinda afya zao.
 
Kwani Hawezi kununua akizihitaji??, Hio ni kama kum encourage akacheze AWAY Match!!!!!!!!
 
.........Unamuwekea mumeo condoms kwenye begi ili iweje?Kwa mtazamo wangu itakuwa kama unahamasisha dhambi ya uzinzi na vile vile mumeo ataona kama humuamini hadi imefikia hatua ya kumuwekea condom kwenye begi lake.

Ni kitu ambacho hakileti maana kabisa eti nianze tu kumuwekea mume condom kwenye begi!!!mhhh kinyaaaaaaaaaaaa.
 
Sitamwambia kitu, nitarudi nazo zote bila kuzitumia......
Ofkoz, nitanunua nyingine kwa matumizi yangu....ila hicho kitendo kinaongea kwa sauti kubwa sana!

I thought ungedanganya kuwa hukuzihitaji kabisa............... hiyo ni point, unarudi nazo ili msikwazane
 
Mbona simple tu,ukirudi toka safari unarudi nazo nyingi zaidi tena aina tofauti akiuliza unamwambia zile alizokuwekea wakati unaondoka hazikutosha ikabidi uongeze nyingine.
 
Hizo cd unaziacha tu ili roho yake ifurahi...hazizuii kitu...ukitaka si utanunua tu zingine uzitumie???
 
habari zenu great thinkaz!!!

Jamani dada/mama aliyeolewa au anayeishi na mwanaume kama mume na mke naomba kuuliza, Je ni vema kumwekea mumeo Kinga i mean Condoms kwenye begi anaposafiri kwenda mbali either kikazi,kibiashara au vyovyote ilimradi atakuwa mbali nawe kwa muda???

Kwa kaka/baba aliyeoa au anayeishi na mwanamke kama mume na mke, utajisikiaje mkeo/huyo unayeishi naye akikuwekea condom kwenye begi wakati unasafiri and what will you tell her???

Tujadili jamani!!

Unaweza kumwekea lakini asizitumie. Kwa kifupi haisaidii hasa kama ameshazoea 'voda kwa voda'! Sana sana itazidi kuongeza mapsuko kwenye mahusiano yenu.

Kuna condom za kike siku hizi, vipi mumeo akikuwekea kwenye begi wakati unasafiri utajisikiaje?
 
Very simple akiniwekea wakati nakwenda safari labda nisizione nikazikute nimeshafika.Maana nikiziona na mimi nitamuachia za kike nione na yeye atajisikiaje na ole wake nirudi safari na kuulizia zilipo nisizikute hizo sarakasi za siku hiyo zitakosa mtazamaji.Na kwangu nitahakikisha ninarudi nazo zote kumuonyesha imani yangu kwake pamoja na kuwa mie bila mechi za ugenini wala sisikii raha katika maisha.
 
hapo pamekaa kimtego mtego vile!unamwekea ili iweje?ok akienda nazo na kurudi nazo bila kuzitumia utajiridhisha kuwa huwa hachezi mechi za ugenini??????? mbaya zaidi ukikagua vizuri kwenye begi unakuta nyingine zikiwa zimefunguliwa mean zilikuwa ziki2mika!itasound vp?

Usimwekee atajua pa kuzipata km atazihitaji!!!!!!!
 
Siwezi kumwekea Condoms kwenye Begi kwa kufanya hivyo nitakuwa nahamasisha uzinzi ....neva ever siwezi kufanya hivyo
 
Unaweza kumwekea lakini asizitumie. Kwa kifupi haisaidii hasa kama ameshazoea 'voda kwa voda'! Sana sana itazidi kuongeza mapsuko kwenye mahusiano yenu.

Kuna condom za kike siku hizi, vipi mumeo akikuwekea kwenye begi wakati unasafiri utajisikiaje?

Na pia unawez akumuwekea asiziguse ila kwa kujifanya mtakatifu sana atanunua nyingine na kubanjua kama kawa akirudi home zinakuwa kama ulivyoziweka unaamini mme hajakusaliti alivyokuwa safarini :confused2:
 
habari zenu great thinkaz!!!

Jamani dada/mama aliyeolewa au anayeishi na mwanaume kama mume na mke naomba kuuliza, Je ni vema kumwekea mumeo Kinga i mean Condoms kwenye begi anaposafiri kwenda mbali either kikazi,kibiashara au vyovyote ilimradi atakuwa mbali nawe kwa muda???

Kwa kaka/baba aliyeoa au anayeishi na mwanamke kama mume na mke, utajisikiaje mkeo/huyo unayeishi naye akikuwekea condom kwenye begi wakati unasafiri and what will you tell her???

Tujadili jamani!!
kwa nini msiongee hayo mambo na kumuonya asitoke nje ya ndoa? mie nikiwekewa kondomu nakugeuza kibao kuwa unanishawishi nitoke nje ya uhusiano
 
Tujiulize swali moja mpaka unafikia hatua ya kumuwekea mume wako condom kwenye begi unakuwa haumuamini? Au je kitendo cha kufanya hivyo ni kuwa you dont trust him anymore? Halafu kwa mwanamke ambaye hamuamini mumewe sidhani kama anaweza akachukua jukumu la kumpa condom on the top.

Nafikiri kama unamjali sana mumeo utampa ushauri huko anakoenda awe makini ingawa vile vile inaweza isisaidie kulingana na hulka ya mtu mwenyewe na ni jinsi gani anavyothamini ndoa yake, ningeshauri badala ya kumuwekea hizo condom basiaweke BIBLIA kama mkristu na QUARAN kama mwislamu.
 
Back
Top Bottom