Compaq minilaptop

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
11514-img0948s.jpg

Wakati uliopita, mmoja wetu aliweka hapa jamvini details za minilaptop na feedback kutoka kwa wadau zilikuwa za kukatisha tamaa. Hata hivyo nimekuwa nikitumia hii minilaptop sasa kwa muda na nimeiona kuwa ni kifaa rahisi kutumia kama laptop ya kawaida na ni nyepesi kubebeka. Kwa kifupi ina Win XP Home Edition, HD 160GB, 1 GB memory, wlan, webcamera, 3 usbports..n.k.

Tofauti na laptop kubwa za inch 15, hii haina cd/dvd drive. Kitu ambacho kinaweza kuwa na upungufu kwa wengine ni herufi ndogo katika monitor, lakini kama macho yako yanaona vizuri, unaweza kusoma bila wasiwasi. Maandishi yake ni kama yale kwenye smartphone au PDA. Kwa maelezo zaidi tembelea hapa.
 
Back
Top Bottom