Community Secondary and college: A not for profit education provider.

kotinkarwak

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
376
114
Kwenye ukumbi huu, kumekuwa na maongezi kuhusu kuporomoka kwa elimu na pia kupanda kwa michango ya shule (fees) kwa wazazi. Ufaulu unaopatikana kwenye shule za binafsi wengine wanaamini kuwa ni changa la macho kwani kuna shule zingine zinaweza kuhusishwa na udanganyifu kwenye matokeo ya mitihani ili kuongeza idadi ya wanafunzi kwenye shule zao.
Katika kuwaza njia mbadala wa kutoa elimu, je inawezekana kuendesha shule hapa TZ kwa njia ya non-profit? Na kuna misaada ipi halmashauri inaweza kutoa katika kuanzisha shule kama hii, je viwanja vinavyotengwa kwa matumizi ya wote vipo na vinaweza kutumika?
Swali lingine ni hiyo gharama ya kutoa elimu. Kwa wanaoendesha shule either za serikali au binafsi, mnaweza kutoa maoni yenu kuhusu mahitaji muhimu katika kuendesha shule.

Nawakilisha...
KK
 
Back
Top Bottom