[COLOR="#FF0000"][B]USANII WA SERIKALI KWENYE BEI YA MAFUTA[/B][/COLOR][COLOR="#00ccff"]

jambotemuv

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
224
62
Petroli bei chini
Na Sharon Sauwa
3rd August 2011B-pepeChapaMaoni Yapungua kwa Shilingi 201.37 kuanzia leo
Tozo za Ewura, TRA, Tiper Sumatra zakatwa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura), Harun Masebu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana juu ya kushuka kwa bei za mafuta.Serikali imeshusha bei ya mafuta na petroli, dizeli na mafuta ya taa kuanzia leo nchi nzima. Bei ya petroli imepungua kwa Sh. 202.37 (sawa na asilimia 9.17) kwa lita moja wakati dizeli imeshushwa kwa Sh. 173.49 (sawa na asilimia 8.31).

Aidha, bei ya mafuta ya taa imepungua kwa Sh. 181.37 sawa na (asilimia 8.70). Uamuzi huo ulitangazwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Alisema kushuka kwa bei hizo kumetokana na marekebisho yaliyofanywa kwenye tozo zilizokuwa zikitozwa na taasisi mbalimbali za serikali kulingana na majukumu waliyonayo kwenye mfumo wa biashara ya mafuta.

Masebu alisema tozo za taasisi mbalimbali zimerekebishwa kwa ujumla wake ambapo tozo katika petroli imepungua kutoka Sh. 54.03 kwa lita hadi 27.27 (sawa na asilimia 49.53) na dizeli kutoka Sh. 55.00 hadi Sh. 28.15 kwa lita (asilimia 48.80).

“Mafuta ya taa yamepungua kutoka Sh. 55.66 kwa lita hadi Sh. 24.50 (asilimia 55.98) kwa lita. Kwa wastani tozo za taasisi zimepungua kwa asilimia 51.44,” alisema Masebu.

Kwa mujibu wa Masebu, bei ya kikomo kwa mafuta ya petroli kuanzia Julai Mosi hadi sasa ilikuwa Sh. 2,206.16 na kwamba bei ya kikomo mara baada ya mchakato wa marekebisho hayo sasa ni Sh. 2,003.79.

Kwa upande wa dizeli, Masebu alisema bei ya kikomo ilikuwa ni Sh. 2,084.33 wakati bei ya sasa ya kikomo itakuwa ni Sh. 1,910.84.

Masebu alisema bei ya awali ya kikomo kwa mafuta ya taa ilikuwa ni Sh. 2,085.90 wakati bei ya sasa ni Sh. 1,904.53.
Kwa mujibu wa bei mpya, bei ya kikomo katika jiji la Dar es Salaam sasa itakuwa Sh. 2,004 kwa petroli, dizeli Sh. 1,911 na mafuta ya taa ni Sh. 1,905.[/COLOR]

Lalamiko kubwa lilikuwa mafuta ya taa yalipandishwa bei kuwa sawa na dizeli kwa kisingizio cha kuzuia wafanyabiashara wakorofi wanaoyachanganya kwenye dizeli na petroli. Walalahoi ndo wakabebeshwa mzigo wa kuzuia biashara haramu badala ya vyombo husika kufanya kazi yake kudhibiti ubora wa bidhaa. Kwa sasa bei zimeshushwa kwa wastani kwa Tsh 200 kwa kila aina ya mafuta ambapo ya taa yameshuka kwa Tsh 181.37 yakitofautiana na dizeli kwa chini ya Sh 6 tu. Huu si usanii ni nini? Ni wazi kuna kila nia ya kuwakamua walalahoi vile ndo watumiaji wakuu wa mafuta ya taa na hawana nishati mbadala. Ndo maisha bora haya?
 
Back
Top Bottom