coastal union ya tz yasajili mchezaji kutoka brazil

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,845
Timu ya soka ya coastal union imefanikiwa kumpata mchezaji kutoka brazil. mchezaji huyo atareport mda wowote akiwa na mke wake. mchezaji kasema anafurahi kubadili mazingira ya kazi yake. ntawapeni updates soon ikiwemo na picha. mia
 
KIUNGO wa kimataifa wa Brazil,
Deangelis Gabriel Barbosa (27)
aliyekuwa akisubiriwa kwa
hamu hatimaye amewasili jijini
Tanga na kupokewa kwa
shangwe na viongozi pamoja na
mashabiki wa Coast
Barbosa aliwasili Jumamosi jijini
Tanga akiwa na mkewe Zaira
Caroline na mtoto wao Lara
Barbosa na kutambulishwa
rasmi kwa waandishi wa habari
jana katika makao makuu ya
klabu hiyo yaliyopo barabara ya
12 .
Mbrazil huyo alisema amefurahi
kufika Tanzania mkoa wa Tanga
amefurahishwa na mapokezi
mazuri pamoja na kuahidi
kukata kiu ya mashabiki wa
klabu hiyo.
�Mimi na mke wangu
hatukutegemea kupata
mapokezi makubwa namna hii,
ninachoahidi ni kwamba
nitajitahidi kwa kiasi cha uwezo
wangu kuiletea mafanikio kwa
timu yangu ya Coastal Union,�
alisema Barbosa.
Akizungumza wakati
akimtambulisha, Makamu
Mwenyekiti wa Coastal Union,
Steven Mnguto alisema tayari
klabu yake ipo katika hatua za
mwisho za kukamilisha kibali
cha kumuwezesha kuchezea
Coastal Union.
�Barbosa amesaini mkataba wa
mwaka mmoja na ataanza
kuonekana uwanjani hivi
karibuni kwani tupo katika
hatua za mwisho za kukamilisha
vibali vya kumuwezesha
kufanya kazi nchini, lakini vibali
vingine kama ITC tumepata,�
alisema Mnguto.
Alieleza kufurahishwa na ujio wa
Barbosa na kusisitiza kuwa
amewasili wakati muafaka
kwani Coastal Union inamhitaji
kiungo mshambuliaji kama yeye.
Barbosa ametokea timu ya New
Road ya Nepal aliyojiunga nayo
mwaka 2010 pia amewahi
kucheza Paham Footbal Club,
Flamengo, Santa Cruz zote za
Brazil na Churchill Brothers ya
India, Maruinense pamoja na
Sport Club ya Jiji la Paulo Afonso
 
mbona hajatuletea salamu kutoka kwa Maximo?

Deangelis Gabriel Barbosa da Silva ametokea Paulo Alfonso, Bahia, pwani ya kaskazini ya Brasil, kwenye ligi ya kwao amechezea Cruzeiro na Flamengo.
Maximo alikuwa muuza matikikiti huko Porto Alegre, pwani ya kusini ya Brasil. Wala hawajuani...
 
Wivu wa kibarazani huo, kina Jama Mba ndo wanalijua soka bwana...

jamba ba alikuwa msafisha viatu wa wachezaji wa club canon yaounde yanga wakaingia kichwakichwa na kuonyeshwa tu picha alizopiga na wachezaji wa timu hiyo.nilikuwa nawaonya tu,si unajua hata maximo ni muuza matikiti tu huko porto alegre?
 
Timu ya soka ya coastal union imefanikiwa kumpata mchezaji kutoka brazil. mchezaji huyo atareport mda wowote akiwa na mke wake. mchezaji kasema anafurahi kubadili mazingira ya kazi yake. ntawapeni updates soon ikiwemo na picha. mia


Mchezaji kutoka Brazil...... kuna maswali mengi sana juu yake ambayo majibu yake hayataki haraka .... ...... U- Brazili wake sio hoja, hoja ni kwamba je anauwezo wakucheza mpira? tena mpira huu wa bongo? kule alikuwa naacheza klabu za mchangani au? maana hata kama kule alikuwa hachezi mpira na alikuwa anafanya kazi nyingine kama kuosha magari, shoe shine au mpokea wageni hotelini haijalishi kazi ni kazi bora mkono uende kinywani na watoto wapate chooooooo ... huo ubrazil wake hauna maana yoyote............. isipokuwa ....... tunataka kuona kilichomleta ... si unajua tumeona wachezaji wa Simba & Yanga walioatoka mataifa yanayojua mpira wakija hapa kwetu ni maluelue tu
 
KIUNGO wa kimataifa wa Brazil,
Deangelis Gabriel Barbosa (27)
aliyekuwa akisubiriwa kwa
hamu hatimaye amewasili jijini
Tanga na kupokewa kwa
shangwe na viongozi pamoja na
mashabiki wa Coast
Barbosa aliwasili Jumamosi jijini
Tanga akiwa na mkewe Zaira
Caroline na mtoto wao Lara
Barbosa na kutambulishwa
rasmi kwa waandishi wa habari
jana katika makao makuu ya
klabu hiyo yaliyopo barabara ya
12 .
Mbrazil huyo alisema amefurahi
kufika Tanzania mkoa wa Tanga
amefurahishwa na mapokezi
mazuri pamoja na kuahidi
kukata kiu ya mashabiki wa
klabu hiyo.
�Mimi na mke wangu
hatukutegemea kupata
mapokezi makubwa namna hii,
ninachoahidi ni kwamba
nitajitahidi kwa kiasi cha uwezo
wangu kuiletea mafanikio kwa
timu yangu ya Coastal Union,�
alisema Barbosa.
Akizungumza wakati
akimtambulisha, Makamu
Mwenyekiti wa Coastal Union,
Steven Mnguto alisema tayari
klabu yake ipo katika hatua za
mwisho za kukamilisha kibali
cha kumuwezesha kuchezea
Coastal Union.
�Barbosa amesaini mkataba wa
mwaka mmoja na ataanza
kuonekana uwanjani hivi
karibuni kwani tupo katika
hatua za mwisho za kukamilisha
vibali vya kumuwezesha
kufanya kazi nchini, lakini vibali
vingine kama ITC tumepata,�
alisema Mnguto.
Alieleza kufurahishwa na ujio wa
Barbosa na kusisitiza kuwa
amewasili wakati muafaka
kwani Coastal Union inamhitaji
kiungo mshambuliaji kama yeye.
Barbosa ametokea timu ya New
Road ya Nepal aliyojiunga nayo
mwaka 2010 pia amewahi
kucheza Paham Footbal Club,
Flamengo, Santa Cruz zote za
Brazil na Churchill Brothers ya
India, Maruinense pamoja na
Sport Club ya Jiji la Paulo Afonso

Dah halafu nilikuwa sijui kama makao makuu ya Coastal Union yamehamia mtaa wa mahasimu wao African Sport barabara ya 12.
 
jamba ba alikuwa msafisha viatu wa wachezaji wa club canon yaounde yanga wakaingia kichwakichwa na kuonyeshwa tu picha alizopiga na wachezaji wa timu hiyo.nilikuwa nawaonya tu,si unajua hata maximo ni muuza matikiti tu huko porto alegre?

Awe muuza miwa ama chips ama hata mchoma ndizi....who cares? tunachojali hata kama akiwa mchoma ndizi basi apige soka na kufunga mabao.
 
Yanga tunamtaka sisi, tutamsajili katika dirisha dogo. Mtoto hawezi kukaa na hiyo almasi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom