Clouds Media, hongera kwa kujipambanua

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,509
7,539
nimeona hiyo post ya '' clouds media wamwandalia birthday JK 2010''. sasa nimepata picha ya yale makengeza waliyonayo kwenye ishu zozote zinazomhusu huyo bwana. na ndipo nafahamu kwa nini wana ukaribu sana na TBC( nimeshawahi kuanzisha thread kuulizia hilo) jibu ni kuwa wote wanamtumikia bwana mmoja.swali ninalojiuliza JK/CCm wana hisa kiasi gani katika umiliki wake au labda mmiliki ni kada wa CCM?siwezi kumlaumu mmiliki kwa kufanya anachofanya na mali yake bali nampongeza kwa kufanya uamuzi sahihi wa kujipambanua.

Hata kuelekea b'day yake mtangazaji wa michezo(ndugu shafii) alisema atamzungumzia JK na mchango kama mwanamichezo, nilijuuliza kwa nini kipindi hiki, je haitakuwa aina fulani ya propaganda, niliamua kutosikiliza kipindi kile na mpaka leo sijasikiliza na sitarajii kusikiliza tena.

Pia Kuna wakati ndugu Kibonde alilaumiwa sana kwa unazi wake, binafsi siwalaumu waliokuwa wakimlaumu kwa sababu hawakufahamu undani wa redio hiyo lakini sasa naamini watakuwa wamefahamu hilo na sitegemei tena KIbonde au mtangazaji mwingine yoyote kulaumiwa kwa sababu wako pale kutekeleza matakwa ya mmiliki, kitu ambacho ni sawa na kumlaumu mtangazaji/mwandishi wa redio/gazet Uhuru ya Ccm au mwandishi wa magazeti ya RAkwa kutangaza/kuandika kile alichoamriwa kwani ndicho kinachompa riziki .

Ninachokiona sasa ni kuwa wamegundua propaganda ni rahisi kusikilizwa na wengi pale zinapotangazwa na redio ambazo itikadi yake haifahamiki vyema tofauti na kusikiliza redio Uhuru au gazeti Uhuru lisilouzika ambapo wanaofahamu hawasikilizi/hawanunui kabisa au wanaosikiliza wanasikiliza wakitaka kusikia ni propaganda gani mpya zinatangazwa.

Hivyo basi ukiamua kusikiliza isikilize lakini usimlaumu mtangazaji kwa sababu yuko kazini.
 
Back
Top Bottom