Clouds Media kuwa mbadala wa TBC ni sahihi?

mkirua una lako jambo, hapo ishu sio kuisikiliza ishu ni kuijadili humu kila uchao
yapo ya msingi zaidi kuzungumzia na sio kujadili clouds hapa.

mtoa mada bora uende ktk webpage yao andika hizo mada zako utaelezwa kwa nini wadosi wanaitumia clouds

Lokissa sina jambo lolote bali ninachokiona humu kila kukicha kuna ama Clouds au Kibonde...then kuna comment kuwa ni Radio ya wafu..Kama umefuatilia mijadala mingi inayohusu clouds kuna pia wito kuwa wana JF tusisikilize hiyo Radio na niliwahi kuuliza mara kibao what is wrong btn Clouds na Some of JF members?? Hapo sasa hakuna wa kutoa jibu....

Conclusion yangu ni kuwa tunapretend kuwa hatuitaki wala hatuisikilizi kumbe ni our favorite station!! Kama ni kweli hatuisikilizi mada kila siku za nini humu?? Ni wazi kuwa hatuwezi kujuwa kinachosemwa na clauds kama hatuwasikilizi.....
 
clouds wasingemfuata asingezungumzia huu mgomo???

NI haki yetu kama watanzania kusikia kauli ya serikal juu ya mgomo wa walimu.clouds wamefanya jambo jema sana kuturahsisha kusikia kauli ya serkali japo hazijaniridhisha.kwhyo cloudz inafanya kazi yake vyema hasa powerbrkfast hii inamaanisha tb wamelala japo nasikia alikuepo leo wazr wa utumish wa uma.
 
Hii radio ina matatizo nadhani hata kodi sijui kama inalipa ipasavyo ok siku itasema na imeajiri makada tu wa ccm hakuna kipindi cha maana kuanzia asubuh hadi usiku KITU NI RADIO FREE AFRICA AU HATA EA RADIO NAFUU
 
Youth has almost become an ideology in itself kutokana na wingi wao (70% plus), na ili kuwafikia hawa, CCM inafanya whatever it takes, including kuwafuata walipo e.g. Clouds.
 
Mwishoni mwa miaka ya 2010 tbc ilianza kupotea kwa wateja hasa baada ya kujikita kwenye uccm na kuponda upinzania hasa ktk kila kipindi kilichokuwa kinaruka hewani.

Wadau walijaribu kuwaonya na kuwambia wasipende kuwa upande mmoja wa shilingi maana shilingi ina pande mbili wakapuuza kwa vijembe na mbwembwe nyingi.

Leo hii tbc ambayo ndio kituo tv ya taifa kimepwaya na kimepoteza dira na mwelekeo kwani hata wale watu wa vijijini nao mpaka sasa wamekipa kisogo,tuliwapigia kelele wakati wakipendelea uCCM na tukapaza kwa wananchi kususia tbc na hatimaye kweli mwitikio ukawa mkubwa na kikasusiwa mpaka sasa sidhani kama kinaingiza faida yoyote,bahati yake ni kuwa kinapata ruzuku lkn kama kingekuwa cha mtu binafsi mpaka sasa angekuwa ameshafilisika.

Kwa sasa naona kuna hawa Clouds media nao sasa hivi wameshika hatamu kwa kujipendekeza kwenye serikali ya CCM na magufuli, kwa sasa ndio kituo kinacho kiki kwa kupigiwa simu na magu na wamejiona sasa kama wao ni kituo cha serikali maana siku hizi ndicho kinarusha ziara za kiserikali, hawa wanaingia mkenge ambao baadae utawagharimu sana maana wanapitia njia zile zile walizopitia TBC.

Kwa mnaofuatilia mtakumbuka ndugu kafulila aliwahi kutolewa kwenye kipindi ambacho kilikuwa tayari kimeandaliwa lkn sijui kwa hofu ya kuchukiwa na magu wakaona wakatishe.

Clouds media inatumika kama mbadala wa kuwapoteza ITV na ipp media ambao hawakuwa na upendeleo wa upande wowote hivyo kuwachukiza maccm ambao wanataka kumiliki na kuviendesha vituo vyote vya habari.

ITV nao kwa kutojijua sasa wamejisahai na wao wameanza egemea upande wa serikali ya ccm bila kujua kwamba wanaingizwa shimoni ili nao wajipendekeze harafu wakose umaarufu na hatimaye clouds media ishike hatamu.

Ndugu zangu sasa ni muda wa kuanza kuisusia clouds media mpaka ijirekebishe maana wameegemea kwenye uccm zaidi kwa sasa.

Swelana.
 
Unataka kutuaminisha kuwa TBC wana vipindi vizuri sana, muonekano mzuri sana kuliko chanel nyingine ila wananchi wameisusa kisa wanaipendelea ccm? Unapotoka kabisa, kama kuipendelea ccm ndio kufa hao clouds wameshindwa vip kufa tangu 2015 walipoipendelea ccm?

Hebu TBC waje na muonekano mzuri na vipindi vizuri tuone kama watakupotea, nani aangalie chanel yenye muonekano wa zamani na vipindi vya mwaka 47 wakati kuna chanel nyinyine zenye muonekano mzuri,vipindi vinavyogusa jamii kubwa, watangazaji wenye mvuto kwa watazamaji, matukio yenye mvuto kwa watazamaji wengi.

Mchawi wa TBC usijidanganye kuwa ni watu kuwaambia wananchi bali ni ubunifu wao wenyewe.
Clouds wamejipanga kufanya biashara na sio kumfurahisha kila mtu na chama chake, kama wanajua wengi wanataka burudani katika muda fulan watahangaika naye wapate wanachokitaka, kama ni ziara za makonda wenzako wamecheza kibiashara kwani walijua hata wapinzani watataka kujua Makonda karopoka nini leo.

Kama unafatilia sakata la Clouds na upinzani limeanza lini basi usijihangaishe kabisa hao ni wafanyabiashara wazuri tu, waukize wenzako wa hip hop waliongizwa mkenge na sugu leo wako wapi na clouds iko wapi.

Sio kila anayeipenda ccm anaweza kupotea kizembe , Diamond waliyemsusia yuko wapi sasa hivi ukilinganisha na wale wengine? Biashara ni akili na sio kumridhisha kila mtu. Clouds wana uwezo wa kubadilika kutokana na muda, siku ukawa ikawa na maslahi kwao watajipeleka ila kama hakuna watatafuta kwingine.
 
Nina muda mrefu sana kuangalia clouds. Bu the way hawana chochote zaidi ya umbea na kumtukuza m. Tu. Kufu
 
Hujui unachokiongea,clouds media ni malimbukeni,wana uccm sana ndio maana magu kawapenda.
Sasa wewe jidanganye kwamba tbc imekufa kwa sababu ya ubunifu,tbc inakufa kwa sababu ya ubinafsi wa uccm hilo liko wazi,
Kipindi wanashadadia uccm sisi wapenda haki tulihamasisha wasusiwe na matokeo yake umeyaona wamechoka hali mbaya.
Clouds media nao wasubiri uhamasishaji unakuja hatutaki watu wanaokuwa wanafiki kwenye media,tutahamasishana na watapotea,ngoja tubuni njia nzuri ya kuhamasishana,tunza maneno yangu kabla ya 2020 utaniambia.

Swelana.
 
Hata kama ni mm siwez kupoteza mda kwenda kuhojiwa na media ambayo husikilizwa na watu wawili!
NI FURSA KWA MEDIA ZA UMA KUACHA URASIMU NA KUJUANA KTK KUAJIRI!
MANA MEDIA INATENGENEZWA NA WATU SASA ZA UMA WANAAJIRI SI KWAKUANGALIA VIPAJI, UTASHI, ELIMU WALA NN BALI NI KUJUANA WW UNATEGEMEA NN.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom