ukubwa wa Clouds Fm utakuwa ndani kwako tu ..Kama tunavyojua ya kwamba Lady Jay dee komandoo hana mahusiano na redii clouds fm,sasa hali hiyo imefanya huyu dada hata nyimbo zake kutochezwa katika kituo hicho.
Kumbuka clouds washakuwa katika tafrani na wasanii kama Mapacha,Sugu,Rama dee n.k,lakini hao wote waliomba msamaha na walisamehewa na bado nyimbo zao hazichezwi pale wala hata interviews hawapewi wala nini! Sasa huyu dada nadhani anaona aibu kuomba radhi clouds fm kwa kuwa anajua hata akiomba msamaha bado hawatacheza nyimbo zake, kitendo cha Jide kugombana na clouds fm kimemfanya akose ushirikiano na wasanii wote wa tanzania na hico kujikuta hakuna msanii anaeomba kufanya collable na yeye.
Hii inatokana na kwamba wasanii wanaogopa endapo watamshirikisha hii maana yake nyimbo haitapigwa clouds fm na ndio redio kubwa Tanzania nzima,ukitaka wimbo wako uvume ni lazima udili na hawa majamaa,kazi ipo
Nyimbo isipopigwa clouds, haingizi hela au?
Mkuu sikubaliani na wewe msanii hata wimbo akiwa na wimbo mbovu akipelekwa kwa hao mawingu atasikika !!!!!...... hapana huo uongo .Ni kweli kuwa Clouds fm ina nguvu kubwa kwa wasanii na hii ni kwa sababu inasimamia tasnia nzima ya music na sio tu kupiga nyimbo kama wengine.
Wanafanya promo, wanaandaa matamasha na pia deal nyingi za mziki za nje na ndani zinapitia kwao, hivyo wakiamua kumpandisha msanii watampandisha hata awe mbovu.
Pamoja na hayo zipo njia nyingine nje ya wao na Jide ni mkongwe hivyo anaweza kufanya mambo kama kawaida na wadau wengine na akawa safi.
JIDE NI PAKA MZEE HAWEZI KUPOTEA NJIA
Rudia kusoma post yangu, nimeandika wakiamua na sio wakihongwaMkuu sikubaliani na wewe msanii hata wimbo akiwa na wimbo mbovu akipelekwa kwa hao mawingu atasikika !!!!!...... hapana huo uongo .
kuna jama zangu wawili wanamuziki wachanga wanatoka mbeya siku moja tulikuwa tunabishana kuhusu haya haya mambo ya muziki wakasema kwa Tz hao jamaa ni ndoo wachawi wa muziki wakiamua kitu ndoo wameamua kama wakikata wamekataa huwezi toka kamwe ....
Niliwabishia nikawaambia ukitoa wimbo mzuri lazima mashabiki wa ukubali kwanza ndoo wewe msanii ufahamike alafu uanze kula deal za matamasha ila ukitoa wimbo mbaya utahonga mpaka uchoke hausikiki hata kidogo, waliendelea kunibishia.
Nikaja kuachana na hao jama baada ya kuona ni wale wale wamekuwa brainwashed . Sasa ikafika zamu yao na wenyewe ni wasani inabidi waingie studio watoe wimbo wapeleke pale ...sikia kichekesho wale jamaa walipeleka wimbo pale mwaka 2012 waka honga wee mpaka wakachoka lakini wasikilizaji hawakuzipenda nyimbo zao. Baada ya kuona Ma dj na watangazaji wanawalia hela wakaamua kurudi kulima mbeya.
Tatizo wasani wa Tanzania hawajitambui sijui Elimu ila kuna baadhi wanajitambua kama Sugu , Nature , Prof J na Jide.Hao redio mawingu ndo wanaowanyonya hao wasanii wasiojitambua jide anajitambua ndiyo maana hataki shobo.
kweli mkuu mleta uzi tumemshtukia ni kipele wa clouds,thumbs up lady jd komando...NDI NDI NDIclouds bana wameona dada wa watu kakomaa na anafanya powa mnakuja kuchek upepo wa mashabiki bado tunaiman nae akomae mtegemea cha nduguye hufa masikini.
kuhusu hilo la kujitangaza kwa njia ya internet nawapongeza sana wana hiphop one the incredible, songa,Nikki mbishi na wengineo kwa kuitumia fursa hiyo vizuri.Mtoa mada umechelewa wapi? Siku hizi watu wanatumia Sana internet, kwahiyo hizi redio zipige zisipige muziki unawafikia watu popote walipo