Clouds FM yafagilia Walanguzi?

Kwa hiyo wewe unaona huu ufisadi wa kuji-prostitute kwa makampuni ya uchimbaji dhahabu na kudanganya Watanzania for a fee kuwa ni biashara poa tu?

Unatetea ufisadi huu mchana kweupe?

Kijana punguza speed. Ni nani hasa alikwambia mimi natetea ufisadi?, kama wewe una hasira zako na Clouds FM ni kivyakovyako, ila ukweli ni kwamba Clouds FM did nothing wrong. Ni kama vile vyombo vya habari vya US vinavyorusha ads mbalimbali kuhusu Obama's birth au health care reform distortions. Kama umeumia sana na wewe nunua air time ufanye counter PR yako kama wewe una uchungu sana na madini ya nchi yako. Siyo kuleta blah blah blah hapa tunataka facts. siyo ubabaishaji na distortions. kama lawama walaumu hao wachimba madini, Clouds wao ni wajumbe tu. Au umenyimwa tender ya kuwatangaza nini?. Maana "hamna hamna ndimo mlimwamo"
 
1. Mikataba ya migodi ni mibovu - Nani analaumiwe kwa mikataba mibovu? Barrick au serikali yako na Bunge lako ''tukufu''? Mikataba yao hata kama ni mibovu lakini iko kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 1998 iliyopitishwa na mbunge wako. Barrick hawakuingia Bungeni kupitisha sheria hiyo!

Barrick pia wanabeba lawama kwa kuingia mkataba mbovu na wa kinyonyaji na serikali ya Tanzania - what happened to corporate social responsibility?

2. Tunapata ONLY 3% from revenue ya madini - Nani wa kulaumiwa? Barrick au serikali yako? Na je wajua kwamba kampuni ya Alex Sterwart inalamba 1.7% out 3% tunayokusanya kwa kukagua mauzo ya dhahabu!? Nao huo si mkataba mbovu kati ya serikali yako na Alex Sterwart?

Barrick pia analaumiwa hapa kuwa kukubali mkataba ambao unaipatia kila kitu but 3%. Swali kwako Masaki, je wewe ukienda benki kuchukua pesa let's say 30,000 lakini mhudumu akakupatia 300,000 kwa makosa au ujinga, je utazichukua na usihesabiwe mwizi?

3. Migodi imetililisha sumu katika mito kama Tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa - Je serikali yako imechukua hatua gani katika kuwawajibisha wahusika wa hili>? Kama ushahidi upo kwanini wasifikishwe mahakamani?

NO swali ni kwamba, Barrick imefanya kama kampuni kuzuia hii sumu in the first place?

4. Watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua - Kama walikiuka sheria za ulinzi wa migodi ulitegemea nini? Kumbuka pale kuna dhahabu kwa hiyo ulinzi mkali wa kutumia silaha unaruhusiwa kwa mujibu wa sheria. Na je walikuwa raia wema au majambazi? Kama kuna ushahidi kwanini kesi hiyo isipelekwe mahakamani?

Wewe umejua vipi kuwa hawa walikiuka sheria? Au unatumia visingizio kama vya serikali ya kikaburu ya Afrika kusini kipindi kile cha ubaguzi (ua na kisha tafuta sababu ya kuua)?

Unatakiwa kumwomba radhi PJ kwa kumdhalilisha kiasi hiki. Sidhani kama yeye ni masikini kiasi cha ''kununuliwa'' kwa kupandishwa ndege, kupewa chakula na malazi ya mgodini ili kumsafisha mtu au taasisi iliyo ovu. Yeye ametoa maoni yake kulingana na aliyoyaona!

PJ aombwe msamaha kwa nini? Aambiwe ukweli (kuwa amechemsha) na kisha aombwe msamaha?

Huo ndio ukweli japo ni mchungu sana! Hakuna bepari yeyote duniani anayefanya kazi bila kutegemea faida kubwa. Msingi wa ubepari ni mtaji unaozaa faida. Suala la kuachiwa mashimo ni kuzungumza wewe na mbunge wako!

Hapa ndipo umejifunua jinsi ulivyo - house negro

- Hapa sasa ndipo unapothibitisha kwamba serikali yako imeoza na haiwezi kufanya chochote kwa sababu ya wizi na ubadhirifu wa mali ya umma. Tanesco hiyo hapo mbona inawashinda kuendesha? Mashirika ya umma mbona yaliwashinda kuendesha? ATCL, TRL mpaka kesho yamewashinda! Mgodi wa Mwadui mliampora mkoloni mbona umeshinda kuendesha? Hao wezi wa BoT si ndio hao hao wangekwenda kuiba huko migodini?

More of house negroeish

Hakika ninakuambia leo hii, mimi siwatetei Barrick au wachimbaji wengine hata kidogo. Ninachosema, bora wao wanaendesha uchimbaji huu kwa ufanisi na matunda yake tunayoaona kutokana na kodi, ajira na mirahaba wanayolipa. Jukumu hili ingeachiwa serikali yako ungeshangaa migodi imekufa, faidi haijulikani imekwenda wapi na hakuna wa kuwajibiswa! ''I see the glass half full while you see the glass half empty''

Ufanisi gani hapa unaozungumzia (mr/s house negro)?
 
Yaani Watu hawataki Kufanya utafiti wala kusikiliza Upande Wa Pili Hii...Nchi hii.Kila Mtu mjanja mjanja.
 
Kijana punguza speed. Ni nani hasa alikwambia mimi natetea ufisadi?, kama wewe una hasira zako na Clouds FM ni kivyakovyako, ila ukweli ni kwamba Clouds FM did nothing wrong. Ni kama vile vyombo vya habari vya US vinavyorusha ads mbalimbali kuhusu Obama's birth au health care reform distortions. Kama umeumia sana na wewe nunua air time ufanye counter PR yako kama wewe una uchungu sana na madini ya nchi yako. Siyo kuleta blah blah blah hapa tunataka facts. siyo ubabaishaji na distortions. kama lawama walaumu hao wachimba madini, Clouds wao ni wajumbe tu. Au umenyimwa tender ya kuwatangaza nini?. Maana "hamna hamna ndimo mlimwamo"

Duuh mkuu Hofstede hivi mbona sio viwango vyako, na wewe umekula mkwanja wa akina Teweli nini? hawa clouds ni vigeu geu, wakati hili sakata linaanza walimtuma yule kijana wao "bonge" akaleta habari kuwa hali sio shwari leo hii sijui wamepewa sh ngapi basi washageuka.
 
Kijana punguza speed. Ni nani hasa alikwambia mimi natetea ufisadi?, kama wewe una hasira zako na Clouds FM ni kivyakovyako, ila ukweli ni kwamba Clouds FM did nothing wrong. Ni kama vile vyombo vya habari vya US vinavyorusha ads mbalimbali kuhusu Obama's birth au health care reform distortions. Kama umeumia sana na wewe nunua air time ufanye counter PR yako kama wewe una uchungu sana na madini ya nchi yako. Siyo kuleta blah blah blah hapa tunataka facts. siyo ubabaishaji na distortions. kama lawama walaumu hao wachimba madini, Clouds wao ni wajumbe tu. Au umenyimwa tender ya kuwatangaza nini?. Maana "hamna hamna ndimo mlimwamo"

Unataka facts utaziweza facts wewe? Huku unatetea "ads mbalimbali kuhusu Obama's birth au health care reform distortions" huku unataka facts.

Chagua kimoja nijue naongea na mtu anayesimamia wapi, sio hata mwenyewe unataka kupanda punda wawili kwa wakati mmoja, huku unadai unataka facts, huku unatetea distortions.

Utapasuka msamba.

Kuna tofauti kati ya Bluray na VHS. Umepata kisoda kilichoandikwa "Jaribu Tena".
 
Kijana punguza speed. Ni nani hasa alikwambia mimi natetea ufisadi?, kama wewe una hasira zako na Clouds FM ni kivyakovyako, ila ukweli ni kwamba Clouds FM did nothing wrong. Ni kama vile vyombo vya habari vya US vinavyorusha ads mbalimbali kuhusu Obama's birth au health care reform distortions. Kama umeumia sana na wewe nunua air time ufanye counter PR yako kama wewe una uchungu sana na madini ya nchi yako. Siyo kuleta blah blah blah hapa tunataka facts. siyo ubabaishaji na distortions. kama lawama walaumu hao wachimba madini, Clouds wao ni wajumbe tu. Au umenyimwa tender ya kuwatangaza nini?. Maana "hamna hamna ndimo mlimwamo"

Kwa hiyo nikitengeneza TANGAZO na kuwapa na tangazo hilo linasema "Rais Kikwete ni FISADI BABA" watalitoa? Hii ikiwa na kulipia hela zote wanazotaka. Kama ni kweli basi semeni bei yake na JF tupeleke matangazo yetu.

Ili iwe na msingi mzuri, tuchukue ujumbe wa Dr. Slaa juu ya Mafisadi na uwekwe hewani na Clouds FM. Hapo tutaona kama kweli wanatangaza kila wanachopewa so longer wamelipwa au WATAGWAYA.

Danganya wengine huko kwenu ila hapa unachezea watu wengine ambao inawezekana hiyo Clouds FM wanaifahamu zaidi kuzidi wewe.
 
Kijana punguza speed. Ni nani hasa alikwambia mimi natetea ufisadi?, kama wewe una hasira zako na Clouds FM ni kivyakovyako, ila ukweli ni kwamba Clouds FM did nothing wrong. Ni kama vile vyombo vya habari vya US vinavyorusha ads mbalimbali kuhusu Obama's birth au health care reform distortions. Kama umeumia sana na wewe nunua air time ufanye counter PR yako kama wewe una uchungu sana na madini ya nchi yako. Siyo kuleta blah blah blah hapa tunataka facts. siyo ubabaishaji na distortions. kama lawama walaumu hao wachimba madini, Clouds wao ni wajumbe tu. Au umenyimwa tender ya kuwatangaza nini?. Maana "hamna hamna ndimo mlimwamo"

- Mkuu Hofstede, heshima mbele sana na saafi sana, sasa kumbe kuna watu wanaotaka kuingilia tena uhuru wa habari? Yaani turudi kule kule tulikotoka kwenye mikingamo na pwagu na pwaguzi!

- I mean huyu PJ ana utaalamu gani kuhusu madini mpaka m-thread mzima kumshambulia as if ni Rais wa Tanzania! Kulikoni wakuu? Huyu PJ ni waziri wa nini hasa mpaka kelele zote hizi? Tatizo la madini sio la PJ ni letu sote wananchi wa Tanzania, we have no clue kabisaa kuhusu madini, sasa tunategemea PJ ndiye aje kutuweka sawa kuhusu madini, what a joke!

- Hebu heshimuni vyombo vingine vya habari jamani, piganeni na hoja zake, lakini hizi sweeping statements za kufagilia ufisadi, bila facts wala evidence mtalimaliza hili taifa, maana itafika wakati wote tutakua mafisadi, jamani mnashuhsa hadhi ya hili neno fisadi!

Respect
.

FMEs!
 
Clouds FM yatusaliti!

The whole week PJ wa Power Breakfast (clouds FM) alikua anatembelea migodi ya Barrick. Akaja na bla bla bla kwamba wamepeleka maendeleo katika vijiji vilivyo zunguka migodi. Mie nimemuona yeye na waliemtuma kwamba ni wa puuzi. Sababu ni hizi:

.

- Mkuu hii habari ni ya kweli, kuna maendeleo makubwa sana ambayo yamefanywa na hizo kampuni as a part of the contract za kuchimba madini, wamejenga shule, wanatoa scholarships kwa vijana wa eneo hilo, wamejenga bara bara, hizi habari mimi nilikuwa wa kwanza kuzileta hapa kitambo kirefu kilichopita kwenye mjadala mmoja wa madini.

- Haya makampuni ni kweli yanatuibia taifa, lakini leo ukienda huko ukapita maeneo yanayozunguka machimbo utajuaje kwamba wanatuibia? Si lazima kwanza uingie kwenye vitabu na uwe mtaalamu wa hiyo fani, sasa PJ alisomea wapi hayo huo utaalamu wa kuweza kupitia vitabu vya hizo kampuni na kugundua kuwa ni waizi wa madini yetu?

- I mean hii mada inaonekana kuwa ni personal beef ambayo wengine hatuijui ila tunaburuzwa tu, either kuna a beef na wamiliki wa Clouds, au huyu PJ, lakini hoja ya PJ kufagilia Barrick so far sijaiona, unless kuna facts zingine zimeachwa, sasa ziwekeni hapa tuzichambue!

Respect.

FMEs!
 
FMES,
Maendeleo ya $200,000 a year ambazo fungu kubwa linaishia mifukoni mwa viongozi wa CCM nisingeweza kuyaita makubwa. Nenda Tarime uangalie hali halisi ilivyo. Hata huko Bulyankulu nasikia kuna wanafunzi waliahidiwa full scholarship na Barrick na dakika za mwisho Barrick wakajitoa. $200,000 a year kwa kampuni inayochota zaidi ya $billioni kwa mikataba iliyosainiwa wakati dhahabu ilikuwa ni $300 an ounce na leo ni $1200 an ounce na bado hawalipi kodi is a big joke.
 
Kwanza nianze na hii signature kabla sijachambua ulichoandika hapo juu. Haya ya kuamini uchawi na warogi ndiyo yameharibu akili yako.

Kulogwa ninakozungumzia mimi hapo ni ''literary''. Nadhani umenielewa sasa!
 
FMES,
Maendeleo ya $200,000 a year ambazo fungu kubwa linaishia mifukoni mwa viongozi wa CCM nisingeweza kuyaita makubwa. Nenda Tarime uangalie hali halisi ilivyo. Hata huko Bulyankulu nasikia kuna wanafunzi waliahidiwa full scholarship na Barrick na dakika za mwisho Barrick wakajitoa. $200,000 a year kwa kampuni inayochota zaidi ya $billioni kwa mikataba iliyosainiwa wakati dhahabu ilikuwa ni $300 an ounce na leo ni $1200 an ounce na bado hawalipi kodi is a big joke.

Hizo $ 200,000 ni kodi inayolipwa kwa halmashauri za wilaya ambako migodi hii iko. Lakini maendeleo yaliyofanywa na migodi hii ni pamoja na ujenzi wa shule za kisasa za sekondari na msingi kwa wananchi, nyumba za kisasa kwa wafanyakazi wote wanaofanya migodini zikiwa na umeme na maji na kisha wakakopeshwa na kukatwa pesa kidogo kidogo. Pia barabara zote zinazoelekea migodini hukarabatiwa na migodi hii.

Isitoshe, Bulyanhulu Gold Mine wamejenga soko la kisasa katika kijiji cha Kakola ambalo sasa hivi lina karibu mwaka mzima tangu likabidhiwe kwa uongozi wa kijiji bado halitumiki. Ukiuliza utaambiwa vikao vya madiwani havijakaa kuamua uendeshaji wa soko, au pengine wanasubiri siku JK akitembelea huko aende akalifungue. Hao ndio Watanzania mnaowatetea!

Tatizo hapa sio wawekezaji, tatizo ni serikali yenu. Nyie mlioko nje ya nchi huwa mnadhani mambo yamebadilika sana hapa nchini, lakini hakika nawaambia siku mkirudi mtasikitika sana kuona kwamba ''mind set'' ya Watanzania bado iko kwenye zama za kale za mawe....Hii ni kuanzia viongozi wao mpaka wapiga kura wenyewe!
 
Barrick pia analaumiwa hapa kuwa kukubali mkataba ambao unaipatia kila kitu but 3%. Swali kwako Masaki, je wewe ukienda benki kuchukua pesa let's say 30,000 lakini mhudumu akakupatia 300,000 kwa makosa au ujinga, je utazichukua na usihesabiwe mwizi?

That argument is completely irrelevant here. Ulitaka Barrick waiambie serikali kwamba hapana jamani, 3% ni kidogo sana, tunataka kulipa 20%? Ungekuwa wewe ndiye mwanahisa mkuu wa Barrick ungefanya hivyo?

Wewe umejua vipi kuwa hawa walikiuka sheria? Au unatumia visingizio kama vya serikali ya kikaburu ya Afrika kusini kipindi kile cha ubaguzi (ua na kisha tafuta sababu ya kuua)?

Ni nani atapiga risasi mtu asiye na hatia? Tanzainia haijafikia huko. Kwa taarifa yako kama kuna watu wanafuata sheria za nchi hapa Tanzania basi makampuni ya kutoka nje, hasa ya madini yanaongoza! Sio zile biashara za wahindi wenu wajanja wajanja waoiba fedha za umma za pale BoT halafu mnawachagua kuingia bungeni!

PJ aombwe msamaha kwa nini? Aambiwe ukweli (kuwa amechemsha) na kisha aombwe msamaha?

Amedhalilishwa, period. Hoja ingejengwa kwamba hana utaalamu wa kujua kiasi dhahabu inayochukuliwa, si kwamba eti alipewa chakula, malazi na kupandishwa ndege ya Barrick ili apotoshe ukweli. Huko ni kudhalilisha!

Hapa ndipo umejifunua jinsi ulivyo - house negro

Tatizo leni mkishakaa sana nje ya nchi basi mnadhani kila mtu anajua misamiati ya USA.....House Negro(!?) Ndio nini?
 
Mwafrika,

Unajiita mwafrika alafu unathubutu kumwiita Mtanzania mwenzio eti 'house negro'! We are Tanzanians, we do not field negros nor house negros! Kama wewe umekaa huko kwa muda mrefu kiasi kwamba unajiona mtumwa basi pole sana
 
clouds kwani mpaka leo hamjajua kua ni genge la wahuni, na sasa mafisadi wameamua kuwatumia kwa mantiki moja tu......radio hii husikilizwa na magenge ya jobless , wamama mitaani na simpleminded person aka bongoflavour mind aka kizazi cha dotcom,.
mafisadi wanajua wakiwin makundi haya basi hata mpige kelele vipi, watashinda kila kona kisiasa na kijamii.
ni mawazo yangu.
 
Mi nawahurumia ndugu zangu mnaopoteza muda wenu kusikiliza radio hii.
Kuna watu na akili zao timamu wakifanya mahojiano na mtu basi utakaa na kusikiliza.

Hebu kaa siku usikilize Radio deutsche welle usikie kina aboubakar lyongo, umil kher, mohamed abdulrahman, othman miraji, sekione kitojo na watangazaji na wachambuzi wenye elimu, ujuzi na uzoefu katika taaluma ya habari jinsi wanavyotangaza ama kufanya mahojiano na mtu.

Kisha uje usikie uharo wa hao clouds wanaotangaza huku wanajambisha, mara wapige kelele, mara waanze kutekenyana....

Ni uharo mtupu
 
clouds fm yatusaliti!

the whole week pj wa power breakfast (clouds fm) alikua anatembelea migodi ya barrick. Akaja na bla bla bla kwamba wamepeleka maendeleo katika vijiji vilivyo zunguka migodi. Mie nimemuona yeye na waliemtuma kwamba ni wa puuzi. Sababu ni hizi:

1. mikataba ya migodi ni mibovu
2. tunapata only 3% from revenue ya madini
3. migodi imetililisha sumu katika mito kama tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa
4. watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua.

leo hii pj na power breakfast, niseme cluods fm wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu?

pj, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Hao jamaa wanafanya pr ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo. Mimi na wewe pj tutabaki hapa hapa tz. Hiyo cheap pr unawapa haitafautiani na ile ya richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!

ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na liyumba je? Anashutumiwa kuiba tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi?

Sasa nikuulize pj, hao jamaa zako wa barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba bot tuka invest katika migodi yetu?

huu ni ujinga watu kama pj na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa.

ombi langu kwako pj na wana clouds wenzako nikwamba, watz waleo sio mbumbumbu. Tunaelewa. Tunachambua na tunatafari. Huwezi tupumbaza kamwe.

mjadala unaendelea.
safi sana yaani umenifurahisha sana tangu nilipomsikia pj anasema ule utumbo nilisitisha kusikiliza hiyo power breakfast ambayo kwa sasa imekuwa weak breakfast.

Huyo pj hajui kuwa there is no free lunch. Amehongwa na hao barrick halafu anakuja kutangaza utumbo wake katika radio, "hatudanganyiki"
 
FMES,
Maendeleo ya $200,000 a year ambazo fungu kubwa linaishia mifukoni mwa viongozi wa CCM nisingeweza kuyaita makubwa. Nenda Tarime uangalie hali halisi ilivyo. Hata huko Bulyankulu nasikia kuna wanafunzi waliahidiwa full scholarship na Barrick na dakika za mwisho Barrick wakajitoa. $200,000 a year kwa kampuni inayochota zaidi ya $billioni kwa mikataba iliyosainiwa wakati dhahabu ilikuwa ni $300 an ounce na leo ni $1200 an ounce na bado hawalipi kodi is a big joke.

- Mkuu Jasusi, hili sio kosa la Clouds na kutegemea PJ ajue haya yote unayosema ni asking for too much kutoka kwa a stimulator talker wa radio, yaani a DJ! it takes mtaalamu of something kujua unayosema mkuu PJ is not!

Respect.

FMES!
 
Hizo $ 200,000 ni kodi inayolipwa kwa halmashauri za wilaya ambako migodi hii iko. Lakini maendeleo yaliyofanywa na migodi hii ni pamoja na ujenzi wa shule za kisasa za sekondari na msingi kwa wananchi, nyumba za kisasa kwa wafanyakazi wote wanaofanya migodini zikiwa na umeme na maji na kisha wakakopeshwa na kukatwa pesa kidogo kidogo. Pia barabara zote zinazoelekea migodini hukarabatiwa na migodi hii.

Isitoshe, Bulyanhulu Gold Mine wamejenga soko la kisasa katika kijiji cha Kakola ambalo sasa hivi lina karibu mwaka mzima tangu likabidhiwe kwa uongozi wa kijiji bado halitumiki. Ukiuliza utaambiwa vikao vya madiwani havijakaa kuamua uendeshaji wa soko, au pengine wanasubiri siku JK akitembelea huko aende akalifungue. Hao ndio Watanzania mnaowatetea!

Tatizo hapa sio wawekezaji, tatizo ni serikali yenu. Nyie mlioko nje ya nchi huwa mnadhani mambo yamebadilika sana hapa nchini, lakini hakika nawaambia siku mkirudi mtasikitika sana kuona kwamba ''mind set'' ya Watanzania bado iko kwenye zama za kale za mawe....Hii ni kuanzia viongozi wao mpaka wapiga kura wenyewe!

- Sawa sawa tupo ukurasa mmoja hapa!

Respect.

FMEs!
 
Mi nawahurumia ndugu zangu mnaopoteza muda wenu kusikiliza radio hii.
Kuna watu na akili zao timamu wakifanya mahojiano na mtu basi utakaa na kusikiliza.

Hebu kaa siku usikilize Radio deutsche welle usikie kina aboubakar lyongo, umil kher, mohamed abdulrahman, othman miraji, sekione kitojo na watangazaji na wachambuzi wenye elimu, ujuzi na uzoefu katika taaluma ya habari jinsi wanavyotangaza ama kufanya mahojiano na mtu.

Kisha uje usikie uharo wa hao clouds wanaotangaza huku wanajambisha, mara wapige kelele, mara waanze kutekenyana....

Ni uharo mtupu

Kitu kingine jamani kuweni macho na hao vijana inavyoelekea wana ujanja janja fulani kwenye matangazo yao na watu fulani, wamekuwa wakipiga debe kampuni fulani ya kuagiza magari ya SBT Tanzania nimeangalia anuani yao sikuipata, ikabidi niandike email SBT Japan, basi jamaa wakanitahadhalisha kuwa makini kwani kibishara hawana ubia nao ila wanaawatambua kuwa kweli wapo wapo wakigangaa njaa yao tu, zaidi wakanishauri kama ni biashara basi ni bora nikawasiliana nao moja kwa moja bila hao wajamaa wanaotangazwa sana na Clouds,
 
nadhan la msingi kujiuliza uyo pj yeye anataluma gani kuweza kutoa analysis ya faida na hasara tunazopata as a result na hao barrick kua apa nchini, wana jf tunaomba cv ya pj plz?
pili wakati pj anaenda kutembelea barrick alikua amejiandaa kwa data za kutosha kabla hajafanya uo uchunguzi wa kutosha?
tatu nani alimtuma kwenda kufanya iyo study? wakati anatumwa alithaminishwa na nani kwamba yeye ni mtu sahihi?
mi nadhan hawa pj angebaki kuchambua mambo ya bongo fleva at least uko is where they belong!
 
Back
Top Bottom