Clouds FM yafagilia Walanguzi?

WATAZANIA TUMELOGWA, ALIYETULOGA ALISHAKUFA KWA HIYO HAKUNA DAWA YA MATATIZO YETU!

Kwanza nianze na hii signature kabla sijachambua ulichoandika hapo juu. Haya ya kuamini uchawi na warogi ndiyo yameharibu akili yako.
 
1. Mikataba ya migodi ni mibovu - Kweli inahitaji kazi, lakini kwanza tuielewe ili tusirudie makosa, pili tuhakikishe tuna capacity ya kuregulate hii sekta na kushiriki kikamilifu.
2. Tunapata ONLY 3% from revenue ya madini - Wrong, 3% ni value ya extraction na siyo revenue. Vile vile kuna njia nyingi za ku-track revenue inayobaki nchini siyo kodi na royalty pekee!

3. Migodi imetililisha sumu katika mito kama Tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa- Mpaka leo hamna vipimo vilivyoweza kuthibitisha madai ya vifo vya binadamu wala mifugo. Hizi habari za kupashana mtaani tuziacheni watanzania...No Research, No Right to Speak!. Wewe inkuingia akilini maiti za watu 44 na mifugo 700, amabao wote wamekufa ndani ya wiki 3 eti hazionekani? waliodai kuzika hawataki kuonyesha makaburi! Hii mipasho kuna siku itafanya watanzania wapigane kwa mambo ambayo hayapo.

4. Watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua. Porojo nyingine hizi hapa - Once again folks u have to do ur reseach, walinzi wa makapuni (haswa extractive industry) ambayo yako listed kwenye NYSE hawatumii silaha za moto, kutokana na makampuni hayo kuwa signatories waVoluntary Principles on Security & Human Rights. Kwa hivyo hawa mabwana wanatumia virungu, tear gas na 'rubber bullets'. wanaomimina hizo risasi ni FFU...acha projo!

Leo hii PJ na Power Breakfast, niseme Cluods FM wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu? Mimi ninampongeza PJ kwa kuwa na ujasiri we kwenda kujionea mwenyewe. Wengi wetu hapa tunajishibisha na material za internet na baadhi ya magazeti lakini hatuja kaa na kujaribu kufanya utafiti wa kina.

The range of what we THINK and DO is limited by what we fail to notice. And because we fail to notice that we FAIL to notice, there is little we can do to change; until we notice HOW failing to notice shapes our thoughts and deeds. Otherwise we will waste time pondering solutions for a unrelated problem. That is the risk we run by ranting without understanding the issue.

PJ, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana Barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Hao jamaa wanafanya PR ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo. Mimi na wewe PJ tutabaki hapa hapa TZ. Hiyo cheap PR unawapa haitafautiani na ile ya Richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!

Ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia Kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na Liyumba je?

Anashutumiwa kuiba Tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi? Sasa nikuulize PJ, hao jamaa zako wa Barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba BOT tuka invest katika migodi yetu? Kaka hizo investment PJ alikuwa anazungumzia ungeenda kujionea kwanza. Mining is the most capital intensive sekta, high risk alafu long term returns...ni balaa. Mgodi wa underground kama ule wa Kahama unahitaji $900 million kujenga, bado haujaingiza hesabu za exploration ambazo huwa haziwi recovered. Hapo huanzi kuzalisha mpaka baada ya miaka 2. Alafu baada ya shughuli kuanza you have to do capital re-investment ili kuweza kuendesha mgodi, bado haujazungumzia umeme, barabara, maji, wafanyakazi...sikukatishi tamaa lakini naomba ukasome kidogo kabla hauja-propose mambo ambayo hayaeleweki!

Huu ni ujinga watu kama PJ na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa.

Ombi langu kwako PJ na wana Clouds wenzako nikwamba, waTZ waleo sio mbumbumbu. Tunaelewa. Tunachambua na tunatafari. Huwezi tupumbaza kamwe.

Sekta ya madini Tanzania inayo matatizo mengi lakini siyo hayo ulioyataja hapo juu. Kumbuka kwamba unapozungumzia hii sekta serikali yako ilijiwekea malengo kwenye Vision 2025; ikasemaa kwa kufungua sekta ya large scale mining inatarijia ifikapo 2025, sekta hiyo itachangia asilimia isiyopungua 10% ya GDP - pato la taifa. Leo hii sekta hiyo inayumba ikichangia kati ya asilimia 2.4 mpaka 3! Lakini wakati huo huo ndiyo sekta inayokuwa kwa kasi kuliko sekta nyingine zote, including telecoms. Sasa hapo jiulize, how is that possible? The 'simple answer' ni kwamba serikali imekosa mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba sekta inakuwa na fwd and bwd linkages to the economy. Vile vile ukiangalia nchi ambazi zimetutangulia kwenye biashara hii utagundua wamevuna mapesa mengi zaidi kutokana na supply chain za migodi. Ndizo zilizopanua tax base, kuibua employment oppurtunities na kuwezesha kukua kwa middle class. Tusidanganyike na ongezeko la royalty na kodi, kwani hizi no siasa tupu. Mrahaba na kodi siyo sustainable, kwani zinakuwa limited na uwezo na performance wa hiyo sekta.

As they say, nothing is complete and thus nothing is exempt from criticism.
 
Hawa jamaa walikwenada kutembelea na kuja na habari hiyo pj aliyoitoa, lakini kama utachunguza habari aaliyoyasema pj yalikuwa kama maoni yake kwani yeye hakwenda kikazi zaidi ila alikwenda kama matembezi aidha ya kukarimiwa au binafsi ndo maana kamaulisikiliza haikuwa habari ya kiuchunguzi kiuchunguzi na iliegemea upande mmoja (barrick).

Lakini ukweliutabaki palepale mikataba yote ya madini ni ya wizi na wakulaumiwa ni serekali ya kisanii ya jamuhuri ya mungano wa tanzania
 
Clouds FM is a crass, low-brow hodgepodge of unappealing potty mouthed misfits, mid age crises combating social climbers brandishing a string of ever increasing shocking shallowness, grotesquely inappropriate chatty-chatty business, unscrupulous half truths, inconspicuously sponsored promotions, and a generally barely covered ill-caricaturing of the collective intelligence of the good people of Dar.

The failed slapstick is hazardous to your health, the toxic sugary dilettantism is at the very least cancerous, the idle dabbling is a waste of time and wattage.
 
Now, can you put this in simple English (lol)?
 
Nina hasira na mediocres wanaojipitisha kama radio station.

That is adequately simple English, au ulitaka niweke references za Quantum Mechanics na String Theory kui-simplify?
 
Nina hasira na mediocres wanaojipitisha kama radio station.

That is adequately simple English, au ulitaka niweke references za Quantum Mechanics na String Theory kui-simplify?
Watasoma tu na dictionary mkuu... Hahahaha
 
Nina hasira na mediocres wanaojipitisha kama radio station.

Redio zote hazina malengo na walengwa sawa. Kama vile ambavyo kuna akina Rush, Howard Stern, Jim Lehrer, n.k., kutakuwepo hao Clouds na akina PJ pia.

Ila kama you've had it up here and you feel you need to exhale, write or call them up and let them know how you feel....
 
Nakubali kwamba redio zote hazina malengo sawa, kwa hiyo kama Clouds wangebaki kwenye commentaries za michezo na kina Kibonde, au muziki na burudani wala nisingekuwa na cha kusema.Huhitaji kuumiza kichwa sana kuongelea art na entertainment, na largely haya ni mambo ya taste, kwa hiyo to each his own.

Lakini the minute wanapoingilia mijadala mizito ya juu ya kama Tanzania inahusika katika biashara ya silaha, au juu ya kwamba uchimbaji wa dhahabu unaisaidia Tanzania ama la, hapo ndipo inabidi tuseme ukweli.

I wont be surprised nikisikia hakuna mtu hata mmoja (kutoka Clouds) aliyeisoma kikamilifu ripoti ya UN kuhusu Eastern Congo, au kama hakuna hata mtangazaji hata mmoja anayejua kwamba Tanzania inachukua a paltry 3% royalty katika biashara ya kuchimba dhahabu.

Sasa unataka watu kama hawa wajipitishe kama wanaweza kutoa social-political commentary kuhusu Tanzania? Kuhusu UN?

Ndiyo maana hunisikii kupiga kelele kuhusu taste ya muziki ya Clouds FM, au obsession yao low-brow na michezo.

Lakini the minute wakiingia kwenye siasa lazima tuwa call out kwamba ni wachovu, hata wao wenyewe wanajua.
 
Sasa unataka watu kama hawa wajipitishe kama wanaweza kutoa social-political commentary kuhusu Tanzania? Kuhusu UN?

I guess inategemea watu wanawachukuliaje. Mtu makini hawezi kutegemea Clouds FM kama chanzo cha habari na uchambuzi makini na yakinifu. Lakini hii inategemea na mtu na mtu. Kwa hakika, si mimi. Sijui wengine.

Ndiyo maana hunisikii kupiga kelele kuhusu taste ya muziki ya Clouds FM, au obsession yao low-brow na michezo.?

Sijui kama wana program format lakini hii ya low brow, sports, and entertainment pengine huenda ndio inawafaa.

Lakini the minute wakiingia kwenye siasa lazima tuwa call out kwamba ni wachovu, hata wao wenyewe wanajua.

Itapendeza kama ukiwaandikia na kuwaeleza sentiments zako.
 
Nina hasira na mediocres wanaojipitisha kama radio station.

That is adequately simple English, au ulitaka niweke references za Quantum Mechanics na String Theory kui-simplify?

mkubwa hapo si ndo ungeua kabisa?? acha hasira inayokufanya utumie lugha ngumu na kutukosesha uhondo wa kukupata vilivyo...

anyway nimekusoma
 
Itapendeza kama ukiwaandikia na kuwaeleza sentiments zako.

Yaani kuwaandikia kutakuwa ni kama kuwa elevate. Kuna washua wanasaga Philly Inquirer na NY Post au hata Newsweek lakini huwezi kuona wanawaandikia hata siku moja.

After all, nakubaliana na point yako kwamba wana segment ya population kwa hiyo kuwaandikia wakati mimi si segment hiyo nitakuwa nachanganya. Ila naandika hapa kama washabiki wao wanasoma waweze kujua Clouds ni kanyaboya. Na kama wanaweza kuwatetea wawatete tuende toe-by-toe in the true Bluray tradition.
 
Twende mbele turudi nyuma, Clouds FM kama chombo chochote cha habari kinaendeshwa kibiashara na biashara yao ni pamoja na matangazo ya biashara.

Sioni ubaya kwa wao kutumia chombo chao kujiingizia kipato kwa kuwafagilia wateja wao, Je unajua ni kiasi gani wamelipwa kwa kazi hii? Mbona hata kina Matunge na waganga wa kienyeji hujitangaza kwenye vyombo vya habari. Kwani mjumbe hauwawi na Clouds si chama cha siasa, tutenganishe siasa na biashara.
 
Ahahahahahahahaaa..sidhani kama washabiki na wapenzi wake wako interested na majadiliano kama hayo....labda uwalaghai kwa kumtumia Tiger/ Cheetah Woods na indescretions zake
 
Twende mbele turudi nyuma, Clouds FM kama chombo chochote cha habari kinaendeshwa kibiashara na biashara yao ni pamoja na matangazo ya biashara.

Sioni ubaya kwa wao kutumia chombo chao kujiingizia kipato kwa kuwafagilia wateja wao, Je unajua ni kiasi gani wamelipwa kwa kazi hii? Mbona hata kina Matunge na waganga wa kienyeji hujitangaza kwenye vyombo vya habari. Kwani mjumbe hauwawi na Clouds si chama cha siasa, tutenganishe siasa na biashara.

Kwa hiyo wewe unaona huu ufisadi wa kuji-prostitute kwa makampuni ya uchimbaji dhahabu na kudanganya Watanzania for a fee kuwa ni biashara poa tu?

Unatetea ufisadi huu mchana kweupe?
 
Hastahili lawama yeye kama PJ, afterall ye ni mtu mdogo sana. Nakubaliana na mchangiaji mmoja aliyesema kwamba hana uwezo wa kupanga program ya kwenda kufanya mahojiano na yeyote bila order ya bosi wake.

Kukosekana kwa elimu ya uraia ni moja kati ya matatizo yanayo wanyima vijana wetu uzalendo. Mgao usio na uwiano wa pato la taifa linaweza kabisa kufanya watu wakasahau utaifa na kuendekeza njaa binafsi.

Maadili mabaya ya ki-uongozi wa taifa inapelekea watu kuona kwamba usaliti ndio unaolipa kuliko maadili mema.

Conclusion: PJ asilaumie, alaumiwe mwenye kituo ndie mwanzo wa yote haya.
 
Lawama zinaanza na PJ kwa kujivua nguo uwanjani (wakati mechi inaendelea).
 
Hastahili lawama yeye kama PJ, afterall ye ni mtu mdogo sana. Nakubaliana na mchangiaji mmoja aliyesema kwamba hana uwezo wa kupanga program ya kwenda kufanya mahojiano na yeyote bila order ya bosi wake.

Kukosekana kwa elimu ya uraia ni moja kati ya matatizo yanayo wanyima vijana wetu uzalendo. Mgao usio na uwiano wa pato la taifa linaweza kabisa kufanya watu wakasahau utaifa na kuendekeza njaa binafsi.

Maadili mabaya ya ki-uongozi wa taifa inapelekea watu kuona kwamba usaliti ndio unaolipa kuliko maadili mema.

Conclusion: PJ asilaumie, alaumiwe mwenye kituo ndie mwanzo wa yote haya.

Kwa nini asilaumiwe mtangazaji na mwenye redio ? Mpaka wasikilizaji wa redio hii wanaoiweka mjini na kuipa biashara?
 
Back
Top Bottom