Clouds FM warusha kisa cha kushtua!!

Jamani, Kuna kipindi cha njia panda CLOUDS FM hiyo hiyo. Dr. Seba alikuwa na binti wa miaka 10 ameharibiwa na babu mmoja wa huko Mwananyamala kama sikosei na juu ya hivyo kaambukizwa UKIMWI. Babu hakamatiki jalada lilikuwa Oysterbay lakini inavyoelekea Babu huyo mzito kiaina flani, maana kesi haieleweki, hospitali nako ushirikiano ulikuwa haba, hiyo ni Muhimbili. Ningependa kujua ilifikia wapi maana SEBA alijaribu kuomba wenye taaluma zao, km Wanasheria, TGNP, Tamwa na jamii kusaidia kuona angalau kuna kitu kinafanywa juu ya hili.

TUNAELEKEA WAPI JAMANI???
 
i am speachles, hivi mwanao kafanyiwa kitendo kama hiki ,halafu mzazi unaongea sijui kama nini,hivi inakuwaje jamani, mimi mwili unanisisimka kila sehemu, lakini unasikia mzazi anasema mambo ya kipumbavu, wangekamata huyo aliyefanya hicho kitendo,polisi na wangeangalia kama hao wazazi wako sawa kupewa hao watoto wawalee. man inasikitisha jamani

Mimi sioni wazazi walichokosea, ukisikiliza kwa makini utaona kuwa katika mahojiano kuwa watu wa aina nne. Kwanza ni waandishi wa habari wa clouds, pili mtoto aliyenajisiwa, tatu mzazi wa mtoto na nne ni jamii au watu waliokerwa na tendo hili. Sasa kwa kuwa nchi yetu inaongozwa na sheria za nani ni nani katika kushughulikiwa, imeonekana kuwa mkosaji ni mtoto wa msimamizi wa sheria, hivyo wasimamizi wa sheria wanataka kuvuruga ushahidi wa mtoto wao alichofanya, upande mwingine wa wananchi wamekosa imani na kuamua kulizungumza kwenye jamii tujue kuwa nchi hii ina wenyewe na wenyewe si mimi na wewe bali ni wale walioshika dhamana ya kutenda haki kwa misingi ya sheria.

Ukweli ni kwamba sheria hawapi haki wazazi au jamii kumuhukumu mkosaji bali ni mahakama baada ya kupokea kesi toka polisi kuwa kuna uvunjaji wa sheria umefanyika. Wanachokiongelewa hao wazazi na jamii ni sawa kile ambacho kinatokea kila siku kwa vibaka kuachiwa na wananchi kutoa hukumu straight pasi kusikiliza upande wa pili. Hawa waathirika hawawezi kumuhukumu mtuhumiwa kwani itakula kwao. Kilichopo hapa ni jeshi la polisi kuchukua hatua stahiki bila kuangalia vinasaba vya mtuhumiwa.
 
Nasikia watoto waliofanyiwa unyama walitajwa najina, madarasa wanayosoma na majina ya wazazi wao sasa wamekuwa kituko na wanazomewa madarasani na shule wameacha kwenda. sheria ya vyombo vy ahabari inarushusu hilo?

Mambo ya kusikia achana nayo sikiliza hiyo story wewe mwenyewe,mimi nimeisikiliza kwa makini ni kweli kuwa inasikitisha tena sana.Majina ya victims,wazazi wao na shule zao hazijatajwa hilo nimehakikisha mwenyewe.Wengi wa victims wa aina hii hawasikilizwi kwa sababu hakuna chombo kinachosimamia malalamishi yao pale yanapopelekwa jeshi la polisi.

Kwa kweli utendaji wa Polisi bado hauridhishi na kwa kiasi kikubwa unawakatisha tamaa sana wananchi.Nashindwa hata kusema nini kifanyike kwa maana kesi kama hizi ni nyingi nyingi kweli kweli.

Labda kama tunaweza kuwahamasisha TAMWA,TAWLA na TGNP wafuatilie masuala haya na kushinikiza serikali iyafanyie kazi natumai hali itakua tofauti.

Naunga mkono wale wanaosema vyombo vya habari vishikie bango hili jambo ili lipate kujulikana kwa watu wengi zaidi ili kuwe na great public interest.Its this public intrest inayoweza kulisukuma jeshi la polisi kuwajibika ipasavyo ili wasisakamwe na wananchi.Na kwa kufanya hivyo victims wengine nao watajitokezana kupeleka malalamiko yao ili nayo yasikilizwe.
kwa kweli hali tuliyofikia sasa hivi Tanzania inasikitisha.
 
Mimi sioni wazazi walichokosea, ukisikiliza kwa makini utaona kuwa katika mahojiano kuwa watu wa aina nne. Kwanza ni waandishi wa habari wa clouds, pili mtoto aliyenajisiwa, tatu mzazi wa mtoto na nne ni jamii au watu waliokerwa na tendo hili. Sasa kwa kuwa nchi yetu inaongozwa na sheria za nani ni nani katika kushughulikiwa, imeonekana kuwa mkosaji ni mtoto wa msimamizi wa sheria, hivyo wasimamizi wa sheria wanataka kuvuruga ushahidi wa mtoto wao alichofanya, upande mwingine wa wananchi wamekosa imani na kuamua kulizungumza kwenye jamii tujue kuwa nchi hii ina wenyewe na wenyewe si mimi na wewe bali ni wale walioshika dhamana ya kutenda haki kwa misingi ya sheria.

Ukweli ni kwamba sheria hawapi haki wazazi au jamii kumuhukumu mkosaji bali ni mahakama baada ya kupokea kesi toka polisi kuwa kuna uvunjaji wa sheria umefanyika. Wanachokiongelewa hao wazazi na jamii ni sawa kile ambacho kinatokea kila siku kwa vibaka kuachiwa na wananchi kutoa hukumu straight pasi kusikiliza upande wa pili. Hawa waathirika hawawezi kumuhukumu mtuhumiwa kwani itakula kwao. Kilichopo hapa ni jeshi la polisi kuchukua hatua stahiki bila kuangalia vinasaba vya mtuhumiwa.

mkuu umesikia lakini ni nini huyo mzazi wa huyo fatuma anachosema, mwanzo anaongea kwa uchungu sana kisha ,anasema mambo ya kipumbavu tu, sijui mitando yote kesha haribu, sasa mimi baba ake nitapata ganji lini, ni kitu cha kuzungumza kweli.
 
Mi wala sijaelewa naona mnaongea kichina china, wamebakwa na nani wazazi wanajua?, polisi walimuachaje mbakaji, kulikuwa na maelewano yoyote baina ya wazazi na mbakaji na polisi?

Hiyo link haifanyi kazi leo. au hii PC imeathiriwa na mitikisiko ya mabomu ya Mbagala maana nipo karibu na hapo.
poles sana just click hiyo link........mimi nimepoteza hata moody ya kilakitu...ni unyama sana, mtoto wa miaka 10 unamuingiria nyuma na mbele kama mtu mzima?????hizi ni dalili gani????? huyu mtu ana roho kweli ya binadamu??? haya ni kama zile story za babu Seya........sio tu afungwe huyu ni wa kunyongwa kabisa...
 
mkuu umesikia lakini ni nini huyo mzazi wa huyo fatuma anachosema, mwanzo anaongea kwa uchungu sana kisha ,anasema mambo ya kipumbavu tu, sijui mitando yote kesha haribu, sasa mimi baba ake nitapata ganji lini, ni kitu cha kuzungumza kweli.

Sikiliza vizuri mkuu yule aliyesema jamaa kaharibu "mitandao yote utandao wa nyuma na utandao wa mbele, baba yake ntapata ganji lini?", ni mmoja wa wakereketwa aliyejivisha uhusika wa mzazi na si baba halisi wa Fatuma aliyeongea mwanzo kwa uchungu. Si unajua tena kwenye kundi la mamba kenge hawakosi, na hasa mtu akijua anarekodiwa atarushwa hewani basi inakuwa tabu tupu..., sema hata presenters wameichukulia issue katika sura mbili, taarifa yenye kuhuzunisha na burudani.
 
Last edited:
Wakuu,

Kwa upande wangu kama binaadamu mwenye hisia za kiutu na pia kama mzazi suala hili limeniumiza sana na hata kunipa wasiwasi juu ya usalama wa watoto wetu ambao mara nyingi huwa tunakuwa mbali nao wakati wa kazi na mishughuliko mingine.

In short, huu ni ukatili uliovuka mipaka. Pamoja na ukweli kuwa waendeshaji wa kipindi hiki walikosa kuzingatia vipengele kadhaa vya kimaadili katika ku-handle hili suala, hakika nawapongeza kwa juhudi zote walizozifanya na kutupatia taarifa hizi.

Sote tunajua ya kwamba si kila mwanahabari au mtangazaji anaweza kuwa na jitihada na ujasiri wa kufanya kama walivyofanya.

Naamini, hii ni challenge kwa uongozi wa Clouds FM kuchukua further steps za kuwanoa kiasi zaidi watangazaji wake juu ya taaluma na maaadili, na kwa hakika baada ya hapo, watangazaji hao watakuwa 1000 times better.

Mwisho kabisa, kwa wale ambao wangependa kuwasiliana na Polizi, ikiwa kutaka kujua hatima ya suala hili ama kwa taaarifa nyingine muhimu, tafadhali tumia namba zifuatazo:

Kwa SMS (msg) namba 0783034224 au kwa simu ya mdomo 0754-034224, 0787034224 , zote ni namba za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam.

Namba n yingine ni 0754 276217 na 0776880000. Hizi ni namba za mkuu wa upelelezi kanda maalum ya DSM.

NB: Kwa faida ya wengine wote ambao hawakuwa na namba hizi, tafadhali mzihifadhi kwa matumizi mengine ya baadae pale mtakapozihitaji.

Wasalaam
 
Sikiliza vizuri mkuu yule aliyesema jamaa kaharibu mitandao yote ya nyuma na mbele je yeye baba atapata wapi payback, ni mmoja wa wakereketwa aliyejivisha uhusika wa mzazi na si baba halisi wa Fatuma aliyeongea mwanzo kwa uchungu. Si unajua tena kwenye kundi la mamba kenge hawakosi, na hasa mtu akijua anarekodiwa atarushwa hewani basi inakuwa tabu tupu..., sema hata presenters wameichukulia issue katika sura mbili, taarifa yenye kuhuzunisha na burudani.

Kama umesikiliza vizuri, yule ndiye baba haswaa, na kuna mtu kwa nyuma alikuwa anaulizwa "unalia nini??", naamini waliokuwa kwenye background ni watu wa karibu sana na mtoto, na baba wa mmoja wao alihojiwa

anyway, lazima pia waboreshe ku-filter baadhi ya maneno ili tafsida iwepo
 
kwanza asante clouds kwa kurusha hii kesi

jamani nyinyi mnaofanya kazi kwenye redio, kweli clouds hawana editor wa vipindi vyao kweli???
kama editor yupo alikuwa anafanya kazi gani?
kwa nini editor ameacha hayo majina ya watoto na madarasa wanayosoma yakatoka??
kwa nini editor ameacha hayo maneno ambayo baba yake huyo mtoto amesema kwamba atapata wapi hela sasa hivi?????
yani clouds wametaja majina ya watoto na kusema wameoza?????
kama kuna mtu anawafahamu wahusika wa clouds wawaambie wa edit hii kitu watoe majina ya watoto na maneno ya baba yao ya kwamba atapata wapi pesa????
yani baba hana uchungu hata kidogo???
 
Ukisoma hii thread nzima utaona jinsi wabongo tulivyo na huruma za ghafla.

Ukweli ni kwamba kuna injustice nyingi sana katika jamii yetu ambazo zinaenda unnoticed kwa makusudi au bahati mbaya. Atleast hata Clouds wameweka hii habari mtandaoni...hata wa US, UK nk.. wamesikia ndo wengi hapa wanaonyesha kwamba "we are one" culprits should be punished accordingly.

Lakini hatujiulizi ni mangapi maovu makubwa katika jamii yetu yanayotendeka na tunayafumbia macho? Ofcourse hakuna kinachoweza kujustify huu unyama waliotendewa viumbe hawa..lakini as a larger community lazima tujiulize..tutaendelea kuishi kwa zimamoto mpaka lini? Tujiulize kwa nini utegemee polisi afanye kazi yake vyema..kwa mshahara na kipato ambacho hakikutoshi wewe kwa mlo wa siku mbili? Why?

Ninachoweza kuwaasa wabongo wenzangu..jamii yetu imeharibika..na imejaa unafiki..tunapenda kutatua matatizo pale yanapowagusa wakubwa au wenye uwezo. Ndo maana hata wananchi hawawaamini polisi wala mahakama..Hatuaminiani..

Kuna watoto wananyanyaswa..hata majumbani kwetu..tunawatumikisha kama mahouse girls...hawaendi shule..wanatulelea, kutufanyia usafi, kutupikia kwa ujira mdogo (wengine hawapewi..)....kesho wanakuwa makahaba..kujiuza..ndo tunakuwa wa kwanza kuwapigia kelele..eti maadili yanamomonyoka...Yet ulivyokuwa na nafasi ya kusaidia kulinda maadili ya huyo binti kwa kumpa support ya kisomo hukufanya hivyo..

In all, as a society tuangalie bigger picture..tatizo ni kubwa kuliko tunavyoliona..tukabili kiini cha tatizo..ingekuwa vipi sympathy na ghadhabu iliyoonyeshwa hapa ingekuwa similar kwa ile inayoonyeshwa kwa madudu yanayotendeka katika jamii yetu kila siku? Something could be different.

I hope waliofanya huu ubaradhuli watafikishwa mbele ya pilato.
 
mkuu link iko safi huenda mashine yako tu na net iko down sana.

My Internet connection is ultra-fast na PC yangu ni mpya na very modern, lakini hiyo link naona ina-upload tu muda wote wala haifunguki, for 5 minutes now!! Don't think it's gonna work. Can someone Youtube it?
 
Typical bongo!

Wengi humu wanasikitika, wanatoa kauli za "kulaani", wanalaumu wazazi...wanashusha tuhuma nzito dhidi ya watendaji wa serikali and on and on....But no body comes up with a concrete solutions...(perhaps Mwawado tuu aliyeomba kufuatilia..)....Ilmradi kila mtu anajua ni jukumu la mwingine kutatua hili tatizo.Rightly so..lakini hawawajibiki..sasa tufanyeje? Onyesha njia..ndo uwajibikaji wenyewe huo..Clouds wamefanya jukumu lao..pick it from there--if you are interested anyway..

Sasa jamani kwa mtindo huu tutafika?..wewe kama wewe sema utafanya nini...maana makosa yameshatendeka..its not enough "kusikia hasira na uchungu kwa vitendo vya kinyama"..so what???

It is high time we start giving REAL solutions to REAL problems. rhetoricals na viingereza vingi humu bila matendo ni bure!

Masanja,

Sasa wewe unatoa solution gani?...Or you ain't interested?
 
kwanza asante clouds kwa kurusha hii kesi

jamani nyinyi mnaofanya kazi kwenye redio, kweli clouds hawana editor wa vipindi vyao kweli???
kama editor yupo alikuwa anafanya kazi gani?
kwa nini editor ameacha hayo majina ya watoto na madarasa wanayosoma yakatoka??
kwa nini editor ameacha hayo maneno ambayo baba yake huyo mtoto amesema kwamba atapata wapi hela sasa hivi?????
yani clouds wametaja majina ya watoto na kusema wameoza?????
kama kuna mtu anawafahamu wahusika wa clouds wawaambie wa edit hii kitu watoe majina ya watoto na maneno ya baba yao ya kwamba atapata wapi pesa????
yani baba hana uchungu hata kidogo???
sasa this is crying over spilt milk....wameshataja majina ya hao watoto so the damage is done....ila its true...najua clouds did this with good intentions but without foresight.......kuna mtu anatakiwa kuwajibika as a result of this mishap.....walitakiwa watoe taarifa without so many details yaani majina etc........halafu na wazazi wa hao watoto at least the first parent i heard is NUTS! i don't think he understands the severity of the situation.....yaani my heart goes out to these girls.
 
My Internet connection is ultra-fast na PC yangu ni mpya na very modern, lakini hiyo link naona ina-upload tu muda wote wala haifunguki, for 5 minutes now!! Don't think it's gonna work. Can someone Youtube it?

Mbona solution vipanga tulishatoa huko nyuma, muwe mnasoma thread.Hakikisha browser yako ina Adobe Flash player utaweza kusikiliza murua.
 
The link is not working...I do have Adobe Flash player and still can not open it. Ina-upload tu muda wote wala haifunguki for about 10 mins now!
 
Back
Top Bottom