Clouds FM wamburuza mahakamani Lady JayDee, kesi yapigwa kalenda hadi Mei 27...

babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,644
3,288
MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.

Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

Source:Global publishers
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1368446913692.jpg
    uploadfromtaptalk1368446913692.jpg
    33.8 KB · Views: 3,694
Sasa si mtwambie hiyo hati ya mashtaka inasemaje? Au ni siri?

Tiba
 
wamepata nafasi nyingine ya kupatia hela. hawa jamaa clouds ni zulumati sana. ndo maana jide kasema wana mamilion lakini wanatamani hata mia mbili zangu. kwa ufupi jide kawakamata pabaya. mia
 
Nyani Ngabu tangu lini na wewe umeanza bifu na dadangu Jide?

Sina bifu naye. Ni kwamba tu naona kanunua bifu ili kupromoti album yake mpya.

Sasa ili apate free publicity akaamua ku pick fight na Goliath, so to speak.

Kwa vile Clouds ni chama kubwa nadhani calculations zake ni kwamba umma utamuonea huruma, utakuwa upande wake, na kununua album yake mpya.

Her beef ain't genuine. It's phoney baloney coconut bacon.
 
wamepata nafasi nyingine ya kupatia hela. hawa jamaa clouds ni zulumati sana. ndo maana jide kasema wana mamilion lakini wanatamani hata mia mbili zangu. kwa ufupi jide kawakamata pabaya. mia

Dhulumati wamemdhulumu nani, wapi, lini, na nini?
 
Kwani swala lililopo mahakamani ni lipi la mdhulumiwa kumtaja mdhulumu wake hadharani ama? Naona wazee wa magorofani wanajipanga kudhurumu mpaka kiduchu cha wasanii
 
Nyani Ngabu tangu lini na wewe umeanza bifu na dadangu Jide?

Nasikia Nyani Ngabu ni mtumishi pale Clouds sijui hizi kama zitakuwa ni habari za kweli, kama zitakuwa ni habari za kweli indirectly lazima Jidy na Nyani ngabu wawe kwenye Bifu, kama unadhani hakuna uhusiano wowote jaribu kumsema vibaya Ruge au Joseph K mbele ya Kibonde utaona matokeo yake.
 
Last edited by a moderator:
Nilidhani ruge na kusaga walivyojibu hoja kwenye media yao yaliisha...kumbe wameamua kumpeleka jide mahakamani?...now naamini wana-nia ya dhati kummaliza jide kimuziki..now naamini jide pamoja na kulia kilio kilichopoteza mwelekeo bado anahitaji kusikilizwa ili mtaani tutoe haki "streets justice"...maana naona hawa mabwana wanataka kutumia pesa na vijisenti vyao hata ikiwezekana watoe uhai wa wapinzani wao ki-biashara kwa mgongo wa mahakama.... Possibly itakuwa ni business defamation case ambayo hukumu ni kulipa fidia kubwa kusafisha jina lao.

Jide..please wasiliana na sugu tuone vinega wanaingiaje hapa na kukutetea...mahakama watakuzuia kuliongelea bifu lako kwakuwa kesi ipo mahakamani then itakaa 2yrs na ikitoka unapigwa fine 2billion tshs then unafunga na mgahawa wako na machozi band then unarudi kijijini kwako kulima mihogo.

Damn....joe n ruge..y cant u let this girl go...what do u really want 4m her?...her life?????..telll me psee whatttttttt?...you are grown-ups now "thugs turned businessmen...what else do u need???
 
Back
Top Bottom