Clouds FM; mbona hivyo?

Kimsingi mapumziko ni muhimu lakini inapokuja kwa swala kama hili la radio I think its better wakawa na planning nzuri. Vipindi vyao hasa pb vinahusu current issues.Wanapokuwa na likizo ya namna hii tunakosa mengi!
 
Tatizo letu hapa mkuu ni kwanini baadhi ya vipindi tu ndivyo havirushwi hewani??au unataka kutuambia kuwa hivyo vipindi visivyorushwa ndivyo tu watangazaji na waandaaji wake wamekwenda retreet???na hao wasiokwenda hiyo retreet hawapangi mambo ya mwaka unaofuatia au hao wenzao ndio wanawapangia???au imekaaje hii???

Nadhani wamesimamisha vipindi vile vyenye habari na maeneleo ya aina nyingine, wanaendelea na vipindi vilivyojaa muziki labda na mambo ya michezo. karibu wafanyakazi wote wapo kwente hiyo retreat. lakini kwa sababu raduio haijafungwa kabisa, lazima wawepo baadhi wa kuhakikisha wasikilizaji wanaisikia kile kinachorushwa
 
...acha tu wasiwe hewani, hata mpaka mwakani :(, ...Power breakfast ilikuwa highly rated enzi za Masoud Kipanya, Fina Mango, na huyo Gerrard Hando, sio sasa.

Hiyo ni kweli mwana power breakfast ya sasa hakuna kitu.Hivi masoud na fina wameacha kazi clouds au?
 
Mkuu usikariri!!!!
POWER BREAKFAST bado iko juu vibaya.
PJ, BABRA na GERALD HANDO wameziba vizuri sana gap la hao watu wako na kipindi kinazidi kunoga!!!!Na muhimu kinachijadiliwa hapa ni kitendo cha clouds kutorusha hewani baadhi ya vipindi kikiwemo hicho cha PB.
Watu wanapohoji kulikoni mbona PB hairushwi hewani ujue kuwa wanakikubali kipindi pamoja na wanaokiendesha vinginevyo wasingeulizia kulikoni?????


...ni uhuru wa maoni, haki yako kusoma au kupuuzia, '...i cannot understand it for you' :). Vile vile, Wanaoendesha kipindi cha Power Breakfast ni haki yao kwenda likizo, kama haki za mwajiri, na mwajiriwa zinavyosema. Hilo si jambo la ajabu katika Radio Stations, au hata Television Programmes, kama hawakukuaga au hukusikia wakisema wanasitisha kipindi hilo suala jingine.
 
mi naona wamejisahau kwa sababu wanajua watu wengi wanatune katika redio yao they have tto be careful wasije wakapoteza mwelekeo kwa wasikilizaji
Mimi huwa kuna vipindi ambavyo nafuatlia Clouds FM na nakiri ikifika muda huo huwa lazima niitafute clouds FM. Miongoni mwa vipindi hivyo ni POWER BREAK FAST, NJIA PANDA, na SPORTS.

KWa wiki mbili sasa nimekuwa nanshangazwa kwa kutosikia vipindi vya power breakfast cha Gerad Hando na Paul James wanapoeruzi magazeti na Sebastian Ndege na Njia panda.

Wadau tusaidiane, hivi watangazaji ndo tatizo au vipindi ndo vimekufa? Nakumbuka kuna wakati hata kipindi cha Sport cha usiku walikuwa wakituwekea miziki. Vipi Clouds FM? Au ndo iko safarini kufa?
 
Au Mod, Admin na Management ya JF nao wakaenda likizo, nadhani hata hii thread tusingeiona wala kuchangia !!

Kuna baadhi ya fani huwezi kwenda likizo....
Kwa kifupi mawingu wamechemka kwa kwenda likizo redio ni sehemu ambayo huwezi kusema kuanzia leo hakuna taarifa ya habari kisa Janeth Mwenda na Godwin Gondwe wako likizo.....ni kutokujua nini wanafanya mawingu wao wameshamake mkwanja kwenye matamasha ya jirambe basi sasa hivi wanakula raha...
 
Back
Top Bottom