Clouds FM: Katika hili mnastahili pongezi

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,506
2,409
Clouds FM wamejiunga na Red Alert na mkurugenzi wao Joseph Kusaga yuko studio anawapigia simu watu maarufu ili wachange na tayari ameshachangisha zaidi ya 5m. Wanachangisha pia kwa njia ya sms.
 
Leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast, watangazaji wa kipindi cha XXL wametangaza kwamba redio hiyo itasitisha kwa muda kupiga nyimbo za wanamuziki wa Tanzania ili kushawishi wanamuziki na watu wengine maarufu waweze kuchangia watu walioathirika na mafuriko ya Kilosa.

Radio hiyo ilieleza kwamba wamepanga kukusanya sh. 50 mil katika kipindi cha siku mbili au tatu kuanzia leo. Watangazaji B12 na DJ Fatty wameeleza kwamba mwanamuziki yoyote atakaye taka nyimbo yake ichezwe redioni atatakiwa kutuma meseji 10 ili kuchangia waanga wa mafuriko ya Kilosa. Si kutuma meseji tu, michango ya aina yoyote inapokelewa kama nguo, chakula, mablanketi na vitu vingine.

Katika hili Clouds FM wanastahili pongezi, naamini hii itaamsha moyo wa kusaidia matatizo yanayotokea kwenye jamii yetu ambapo ni nadra sana kwa wanamuziki wetu wa kibongo kujitokeza kusaidia.
 
vyanzo vyangu vya ndani vinanidokeza kuwa reception ya kampeni yao imekuwa kinyume kabisa na walivyotarajia. Guess wanawalaumu kina nani..?

Thanks God,hii ni habari njema kwangu! Acha sisi tuendelee na kampeni yetu.Haya mambo ya kucopy na kupaste aidea za wengine na kujifanya ni initiative zao (VODACOM) na zitawatokea puani.Watu wamewashitukia.
 
Watangazaji B12 na DJ Fatty wameeleza kwamba mwanamuziki yoyote atakaye taka nyimbo yake ichezwe redioni atatakiwa kutuma meseji 10 ili kuchangia waanga wa mafuriko ya Kilosa.
Kwa hiyo siku hizo kuto misaada ni kulazimishana....ukishamlazimisha mtu mi naona si msaada tena huo...!!
 
Clouds FM wamejiunga na Red Alert na mkurugenzi wao Joseph Kusaga yuko studio anawapigia simu watu maarufu ili wachange na tayari ameshachangisha zaidi ya 5m. Wanachangisha pia kwa njia ya sms.
Isije kuwa baada ya kuona mwitikio wa watu umekuwa ndivyo sivyo,inabidi watumie nguvu za ziada lol!
 
Clouds me naona wamefanikiwa sana kwenye hii fund raising yao na wanastahili kuungwa mkono. Unajua kuna watu wanachukua mrengo fulani hata kama mtu akifanya jema hawamkubali.

Baniani mbaya.....

Jamaa wamekuja na idea nzuri,lengo la kusaga lilikuwa achangishe 5m lakini mpaka anatoka studio kawapigia watu wa TCC, Teddy wa serengeti, Kimei wa CRDB, Isaac wa Easy Finance na kampuni yake mwenyewe ya Prime Times ambapo amechangisha jumla ya shilingi 7m.

Watanzania endeleeni kuwachangia hawa watu wenye matatizo kule kilosa.

Charity begins at home........
 
La kushangaza ni kwa nini wameamua ku-team up na VODACOM badala ya kujisimamia wao wenyewe kama wanavyofanya kwenye fiesta zao.
 
Hii ingekuwa Charity mkuu...ningetoa pongezi...lakini hii sio Charity..!!

Tanzania...hata ukiwa unalinda maslahi yako au unarudisha fadhila kwa wanaokupa kula bado unapewa sifa.
 
La kushangaza ni kwa nini wameamua ku-team up na VODACOM badala ya kujisimamia wao wenyewe kama wanavyofanya kwenye fiesta zao.

Nikupe HINT...dodosa bajeti ya Vodacom inayokwenda Clouds FM kwa ajili ya Marketing.

Lakini mimi na wewe ni bora tukubali...bora wahanga wapate misaada au sio?
 
Duh...ama kweli Tanzania...hata ukiwa unalinda maslahi yako au unarudisha fadhila kwa wanaokupa kula bado unapewa sifa.
Ndugu yangu,
Wapo wanaoshindwa kabisa kurudisha hata fadhila. Clouds na wasanii wa Tanzania wanastahili pongezi zetu sio sifa.
 
Hata kama ikiwakilishwa 70% ya michango yote kwa waathirika, binafsi nakubaliana na jitihada za clouds fm. tunahitaji watangazaji creative kama hao bila kujali kama kuna kitu wanafadi binafsi ama la.

Hongera clouds fm
 
Clouds me naona wamefanikiwa sana kwenye hii fund raising yao na wanastahili kuungwa mkono. Unajua kuna watu wanachukua mrengo fulani hata kama mtu akifanya jema hawamkubali.

Baniani mbaya.....

Jamaa wamekuja na idea nzuri,lengo la kusaga lilikuwa achangishe 5m lakini mpaka anatoka studio kawapigia watu wa TCC, Teddy wa serengeti, Kimei wa CRDB, Isaac wa Easy Finance na kampuni yake mwenyewe ya Prime Times ambapo amechangisha jumla ya shilingi 7m.

Watanzania endeleeni kuwachangia hawa watu wenye matatizo kule kilosa.

Charity begins at home........

Mh no comment.
 
La kushangaza ni kwa nini wameamua ku-team up na VODACOM badala ya kujisimamia wao wenyewe kama wanavyofanya kwenye fiesta zao.

Hapo mkuu ndiyo kwenye point isije kuwa hawa Voda wameona wamefulia hiyo RED ALERT wakaona wawaingize clouds through hii idea mpya.

Idea siyo mbaya lakini ilitakiwa clouds wawe wenyewe plus jamaa wa RED CROSS. Maana hawa Red cross ndiyo watoa misaada hasa na wanafika mpaka kusikofikika kiraisi.

Lakini nawapa pongezi hawa clouds maana jamaa wako creative lakini inabidi creativity yao waitumie vizuri kwani kuna watu wanaweza kuitumia kama mtaji wao. BIG UP CLOUDS LAKINI MUWE MAKINI...
 
Nikupe HINT...dodosa bajeti ya Vodacom inayokwenda Clouds FM kwa ajili ya Marketing.

Lakini mimi na wewe ni bora tukubali...bora wahanga wapate misaada au sio?
Mafuru/Kusaga connection? Ngoja wakusanye michango hii. Uzuri mmoja ni kwamba wanachangisha toka kwa wenye nazo.
 
Thanks God,hii ni habari njema kwangu! Acha sisi tuendelee na kampeni yetu.Haya mambo ya kucopy na kupaste aidea za wengine na kujifanya ni initiative zao (VODACOM) na zitawatokea puani.Watu wamewashitukia.

Vodacoma wana makosa gani tena mkuu? something wrong?
 
Hapo mkuu ndiyo kwenye point isije kuwa hawa Voda wameona wamefulia hiyo RED ALERT wakaona wawaingize clouds through hii idea mpya.

Idea siyo mbaya lakini ilitakiwa clouds wawe wenyewe plus jamaa wa RED CROSS. Maana hawa Red cross ndiyo watoa misaada hasa na wanafika mpaka kusikofikika kiraisi.

Lakini nawapa pongezi hawa clouds maana jamaa wako creative lakini inabidi creativity yao waitumie vizuri kwani kuna watu wanaweza kuitumia kama mtaji wao. BIG UP CLOUDS LAKINI MUWE MAKINI...

Hivi mbona kuna wengine comments zenu zina chefua? wale wanaojitahidi kuchangia mnasema wamefulia! ndiyo nimeuliza hapo juu labda kuna kitu sielewi ila sijaona kabisa mantiki ya kuwasema mlivyowasema, simply sijaona!!! I can only see childish comments zilizojaa chembechembe za umbea na ujinga!

I hope all these people were supposed to be encouraged nothing else!!

Marketing?? Vodacom can sustain without this issue ya Kilosa! lets encourage them, acheni idea za kuwa wana market, kwanini Zain wasimarket basi!!

watu wanakufa kuna watu wanasema marketing!!
 
Back
Top Bottom