Clouds FM inaniibia

Pole sana ndugu yangu,siku hizi hela zinatafutwa kwa nguvu,kosa moja tu unafungwa magoli mengi!!!

Sugar wa ukweli, aisee nimepita hapa nilitaka kujua ni lini umefika JF. Nataka kutoa salaaam tu. Just salaaaaaam tu na jina lako zuri.

'.......trrrrr trrrrrrrr halooo Yo Yo haloo Yo Yo. Naona hapatikani.
 
Makampuni ya simu yanatumika vibaya, hasa katika siku za hivi karibuni. Ni mfumo wa kifisadi bado unaendelea. Leo hata wewe ukitaka hela kiulaini, unakwenda kwenye kampuni yoyote ya simu, unakubaliana kutumi mtandao wao kuwafikiwa watu kwa njia ya ujumbe. Wao ( Makampuni ya Simu) yanagharama zao za msg. Wewe unachotakiwa kufanya ni kukubaliana nao kulipa gharama za msg, say Sh. 60/=. Sasa wewe utawatoza wanaotaka huduma hiyo ya kijinga sh. 200/= au 300 au 500/= na nyingine hata 1000/=. Utawatumia ujumbe wa kuwahamasisha wajiunge na mpango wako wa kijinga hata bila kuwafafanulia hasara zinazoambatana na mpango huo. Na kwakuwa wengi wetu hatupendi sana kudadisi kabla ya kufanya chochote tunaishia kujiunga haraka haraka. Bahati mbaya zaidi, unapewa namna ya kujiunga. Hupewi maarifa ya kujitoa. Machungu ya kukatwa pesa yanapokelea ndio akili ya kujitoa inapokuja. Kwakuwa makampuni ya simu yanatengeneza faida, hayashtuki sana unapolalamikia kujitoa. USHAURI WANGU NI KUWA, NI VYEMA KUWA MWANGALIFU NA MPANGO WOWOTE UNAOTANGAZWA, KABLA YA KUJIUNGA HAKIKISHA UMEJUA NINI HASARA ZAKE. Binafsi sijawahi kujiunga kwa taarifa za habari, vichekesho, afya, biblia/korani, caller tune na mengine mengi ya kiwiziwizi yanayofanana nayo.
 
Sugar wa ukweli, aisee nimepita hapa nilitaka kujua ni lini umefika JF. Nataka kutoa salaaam tu. Just salaaaaaam tu na jina lako zuri.

'.......trrrrr trrrrrrrr halooo Yo Yo haloo Yo Yo. Naona hapatikani.

Mkuu usione vya elea ujue vimeundwa hivyo.
Vinawenyewe angalia usije ukadondokea pua.
 
Mdau Jile 79 we mwenyewe ulifanya makosa kujiunga na huduma kama hiyo eti sms neno kwenye namba uwe wa kwanza.Tena ina jingle lake zuuri mi huduma za namna hiyo huwa sijiungi na huduma kama hizo kwani ni wizi mtupu.Je hawajatoa namba ya kutuma kam unataka kujiondoa ili waache kukutumia kwani hiyo ni biashara hizo pesa unazokatwa zinabadilishwa kuwa fedha na wanashirikiana na voda.
 
Nnavyohisi ni kwamba clouds kuna wakati walitaka watu wajirejiste katika Club yao ili kuwa wa kwanza kupata habari mbalimbali za burudani na michezo.Wakimaanisha habari hizo hukufikia wewe kwanza kabla hata ya kusoma magazetini.Lakini ki ukweli ni kuwa wakati wanatoa habari hii hawakujumuisha kiasi cha garama utakapokua umejisajili na mwendelezo wa gharama wakati wa kupokea hizo jumbe mbalimbali.Nafikiri ndugu yangu na wewe pasipo ama kwa kujua ukajisajili na ndio hayo yanayokupata sasa.Pole sana mkuu
 
Jamaa alijiunga mwenyewe, sasa sijui analalamikia nini!!!???? Mibongo bwana wana kurupuka tu!!!
 
350000/- haiwezekani!!! mkuu huwa hatuchaji hivyo huwa inakuwa 287 plus 18% vat, ila pole sana mkuu
 
wahusika wamtandao ndio wanawajibika kukuelekeza namna ya kujitoa.hivyo kama wameshindwa kukusaidia huo ni udhaifu mkubwa kwa upande wao.kuwa makini wakati mwingine ndugu.
 
This is very common...mara unaambiwa tuma sms kwa namba fulani..duh sms yenyewe costs ten times more than the normal charges. hayo mambo yenu ya kusubscribe to this and that number ndio unaliwa pesa bure. babangu kasubscribe sijui entertainment news by mistake ..mambo ya wazee hayo anacheza cheza na simu mara kila siku anatumiwa news about movies, sijui which artists is performing where....ahahhahha sasa mzee maskini yuko mashambani hukooooo za movie hanazo.. and of course kila sms inakula pesa. they never tell u how to unsubscribe mpaka ufunge safari kwenda huko kwa customer care....calling them might not even work! pole lakini uliyataka mwenyewe!
 
Mkuu usione vya elea ujue vimeundwa hivyo.
Vinawenyewe angalia usije ukadondokea pua.

Tehe teheee... kweli kimeundwa. Ila nakuhakikishia Fideli80 mimi nikifanikiwa sitauza mechi kama wewe....haaa......
 
Kuna ujumbe wanatuma kupitia simu ya kiganjani ambayo huwa imetoka Clouds kwanza +15556.

Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikitumiwa hizi meseji bila kujua, baadae nikabaini kuwa kila nikitumiwa meseji moja nakatwa Tsh.350,000.

bro, kwa kawaida msg ya mwanzo kabisa watakayokutumia huwa inasema kujiunga ni bure lakini ukishajiunga siku zinazofuata huwa wanaanza kukukata pesa. UKIREPLY tu hiyo msg unakuwa tayari ushajiunga. zipo service nyingi tu za upuuzi za nmana hiyo mara sijui utajiri, mara HABARI, mara NDOTO ili mradi wapate kukuibia.
ili kujitoa andika msg yenye neno STOP, ONDOA au CANCEL kwenda kwenye namba hiyo hiyo wanayokutumia mfano 15*** nk
 
Acha kutafuta number za kupiga, wewe wafuate huko huko ofisini uwaulize KULIKONI?, nafikiria kuwa watakuwa na jibu zuri kuliko kuongea nao kwenye simu.

Kingine mi nadhani kuwa uliji-enroll kwenye automatic MSG/Notification ambazo wewe mwenyewe umesahau, na mpaka uweze kujua chanzo chako ndio utaweza ku-cancel enrollment other than that utaendelea kuliwa mpaka kuchee.

350/= kwa MSG sio mchezo,

B.
 
thanx!!!!!!!!!!!!!! ila bado sijajua cha kufanya.......
 
thanx!!!!!!!!!!!!!! ila bado sijajua cha kufanya.......

Simu ni yako, hawezi mtu kukuzuia kujaribu kubonyeza namba yoyote au kujiunga na huduma yoyote anytime. Cha msingi ni pale unapogundua umejiunga na service ya hovyo na huihitaji tena iwepo njia ya kujitoa. Nyingi ya hizi huduma hawaweki option ya kujitoa maana hawataki mtu atoke. But this is wrong.

Nashangaa operators wako kimya na swala hili na huku wakijua fika kwamba it's against their license operational requirements. Na TCRA wana kitengo mahsusi kazi yake ni kuhakikisha consumers wanatendewa haki au wanapata huduma bora from the operators.

Nakushauri nenda kwa operator (in this case Voda) open a formal complaint na wakupe evidence (something in writing for furthe follow up). Kisha nenda karipoti hiyo ishu TCRA (watahitaji hiyo evidence). TCRA itawafuatilia kisheria.

Pole! ni mlolongo mrefu lakini bila kufanya hivyo tutabaki tunalalamika tu na ishu haitakuwa solved. Ni wakati sasa watanzania tuanze kushupalia kudai haki zetu.

Mfano mwingine ni hizi promotional sms zinazotumwaga kwenye simu (has kutoka Tigo) wakitangaza mahuduma yao. Sio sahihi maana hatuja consent wote kupokea hizo sms. Nimesharipoti huko TCRA lakini bado naona wanasubiri wapate complaints nyingi zaidi (sijui?). Twendeni tukadai haki zetu. TCRA ipo kukutumikia lakini bado haijui(?) na sisi tumekuwa wapole mno (?). Tuamke sasa.

Wabongo watakuambia 'ah huo usumbufu wote wa nini, si ntatupa chip ninunue ingine?' - it's your choice! tusumbuke leo kwa manufaa ya vizazi vijavyo!
 
si unajua manyau nyau ndugu yangu.........nimechemsha kweli maana siwezi kutoka nahaha huku na kule.Itabidi nivist clouds center nipate jibu...
Duh uliingiaje hapo mpaka umekubali kuliwa kiasi hicho
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom