Clouds: Acheni kufagilia upuuzi - wewe Diva - Loveness Love unajiaibisha....

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Kuna Kipindi cha Clouds sasa hivi kinaendelea.Mada ni Mume wa mtu au girlfriend wa mume wa mtu ni mtamu!

Loveness Love - the Diva anafagilia sana na kusifia... ati maboyfriend ni wachafu wananuka midomo, hawaogi! Waume za watu wanaogeshwa na wake zao, wanapuliziwa mapafyumu.Wakija kwako wasafiiiiiiiii. Mume wa mtu akija kwako raha tupu..... anakuja kwa kazi moja tu anaondoka.Hakuonei wivu wala nini......

Sasa wanaongea na B12... kuhusu sex ... experiences zao nk.

Hivi siku hizi watu wamechunwa uso kama samaki hawaoni aibu kuongea mambo ya faragha bayana?Utadhani hawajazaliwa n mama na baba zao! Hivi kama ndio mwanao anaongea hivi, mzazi utajisikiaje? NASHINDWA HATA KUANDIKA UJINGA WANAOONGELEA.

Jamani mimi naona aibu kwa niaba yao!

Saa hizi ndio kwanza saa 4, watoto bado hawajalala ... kweli maadili yataacha kumomonyoka?

CLOUDS... ACHENI KUTUHARIBIA WATOTO WETU!!!!!!
 
Ana stress za kuachwa na Moracka msamehe bure
My next question would have been.. hivi huyu binti kama ana boyfriend anayemsikiliza saa hizi..itakuwaje?
kumbeee!!

HATA HIVYO HIYO SI EXCUSE YA KUTUMOMOMYOLEA MAADILI YA WATOTO.
 
Tushawazoea hao jamaa, achaneni nao ni makanjanja tu na unprofessional watangazaji. Hivi vigezo vinavyoyumika kuwaajili hawa jamaa wa mawinbi ni vipi? Nadhani kama cha shule kipo basi kinakuja mwishoni!
 
HAYA SASA..WAMEACHA YAO..wanawazungumzia wazazi wao kuwa walianza mapenzi kazini! MWISHO WATASIMULIA YASIYOSEMEKANA! Nyie subirini tu...
 
...........Mwenzenu mimi kwanza huyu Diva wala simuelewi akili zake, zamani nilikuwa napenda kusikiliza kipindi chake lakini siku hizi wala sina hata time nacho. Kwanza huyu binti akili zake sijui zipoje maana hata nikisema akili zake kama mtoto nitawakosea watoto kwa maana kuna watoto wana akili na maadili mazuri kuliko hata Diva..........hivyo sijui hata nimuweke kundi gani?

............Hivyo hawa waandishi/watangazaji wa habari wa siku hizi haswa hizi FM radio wana elimu kweli ya utangazaji wa habari? Wengi wao maadili zero kabisa, sijui hata kozi gani wanazosoma..........sijui ndio wanasoma miezi 6 basi mtu anakuwa kapata tayari kuwa mtangazaji.

Yaani sijui alipata malezi gani huyu huyu msichana maana hana maadili kabisaaaaaaaa!!!!!!!!!!Mie namuona akili zake kana kwamba ndio kwanza yupo kwenye stage za kubalehe.
 
sasa hivi kaongezea dimension kuwa mke wa mtu naye mtamu! na anajua hapo Clouds mmoja anayetembea na mke wa mtu!.... kweli akili zake hazimtoshi.
 
kwani wadau mjadala hautokuwa mzuri kama tukiongea udhaifu wa kipindi chenyewe badala ya mambo binafsi ya muhusika yaaani sijuwe kaachwa sijuwi vipi...haileti raha siyo!
 
haya..anamuongelea babu yake na kimada chake ..binti mchangaaa!
Jamani huyu mtoto!

ati anamuomba radhi kama anamsikiliza!
 
Kuna Kipindi cha Clouds sasa hivi kinaendelea.Mada ni Mume wa mtu au girlfriend wa mume wa mtu ni mtamu!

Loveness Love - the Diva anafagilia sana na kusifia... ati maboyfriend ni wachafu wananuka midomo, hawaogi! Waume za watu wanaogeshwa na wake zao, wanapuliziwa mapafyumu.Wakija kwako wasafiiiiiiiii. Mume wa mtu akija kwako raha tupu..... anakuja kwa kazi moja tu anaondoka.Hakuonei wivu wala nini......

Sasa wanaongea na B12... kuhusu sex ... experiences zao nk.

Hivi siku hizi watu wamechunwa uso kama samaki hawaoni aibu kuongea mambo ya faragha bayana?Utadhani hawajazaliwa n mama na baba zao! Hivi kama ndio mwanao anaongea hivi, mzazi utajisikiaje? NASHINDWA HATA KUANDIKA UJINGA WANAOONGELEA.

Jamani mimi naona aibu kwa niaba yao!

Saa hizi ndio kwanza saa 4, watoto bado hawajalala ... kweli maadili yataacha kumomonyoka?

CLOUDS... ACHENI KUTUHARIBIA WATOTO WETU!!!!!!

Mama kizazi chetu hiki neno "maadili" ni msamiati mgumu sana. Ni kama vile maadili yamepitwa na wakati..eti haya ndio matunda uhuru wa media na utandawazi.!!!!

Mimi Mzazi mwenzio kwa upande mmoja nina bahati kuwa vyombo vya habari kama BBC vinafuata maadili japo kabla ya 11pm. Kinyume na hapo najaribu kutumia technology kama kuweka Password (Parental Control) kwenye Channels ninazojua vina mambo kama ya kina Diva wa Clouds....ikishindikana kabisa basi natumia mbinu walizotumia wazazi wangu kubadilisha Channel au kuzima Television...tena nikizidiwa kabisa hivyo vitu wala hawataviona kabisa....kule sio lelemama, yataka moyo.
 
kwani wadau mjadala hautokuwa mzuri kama tukiongea udhaifu wa kipindi chenyewe badala ya mambo binafsi ya muhusika yaaani sijuwe kaachwa sijuwi vipi...haileti raha siyo!
..........Udhaifu wa kipindi unasababishwa na nani kama sio huyu mtangazaji? Wewe bana hebu soma vizuri thread na kuelewa.
 
Asante Pretty,
Nilishikwa uvivu kumjibu maana inaelekea haelewi hapa tunaongelea nini.Hapa tunaongea na live examples ya kinachojiri huko Clouds ili kama wanaingia humu basi wajirekebishe ... waone kuwa wanayoyaongea hayavutii kivile kama wanavyodhania.
 
sawa, sasa mambo ya yeye sijuwi kaachwa sijuwi vipi yana husu nini hapa?
 
Back
Top Bottom