Katika kipindi cha 45 minutes cha ITV leo jioni , mtoa mada alikuwa CD Msuya, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, enzi ya Mwalimu.
Kwa hakika amenikosha sana.
Bado ana data na current za kiuchumi-inaelekea nafuatilia sana current events
Hana papara wala jazba kujibu maswali, na alikuwa composed.
Lakini zaidi ya yote ameiasa nchi mambo makuu yafuatayp
Kwa jinsi alivyokuwa akijieleza kwa ufasaha, tofauti kubwa imeonekana , ukilinganisha na "Mawaziri vijana" wetu waliopo sasa.
- kuwawezesha wakulima kutukia mbegu bora, utaalam bora wakilimo, na mechanization
- ameishauri serikali kupunguza matumizi(kuachana na mashangingi)
- kuongeza uzalishaji mali-katika kilimo n.k. ili kuongeza pato la taifa nahatimaye kupunguza kuporiomoka kwa shilingi yetu
Walioona tupeni maoni, good or bad.
Hata mimi nilimuona na mazungumzo yake yalikuwa na mantiki sana.Isipokuwa,si alikuwa waziri mkuu ,alifanya nini,nothing.Hawa watu ni wababaishaji tu.Wanaona uozo wanapotoka madarakani,lakini wanapokuwa madarakani wanakuwa vipofu kabisa.Sijui nani anawapa limbwata.Sumaye,Mkapa,Warioba wote siku hizi wanaona uozo tulio nao, lakini walikuwa hawaoni kabisa,kazi kweli kweli.