Civilian shot dead by police after fierce exchange of words

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
A Michungwani resident, Said Malick, in Muheza, Tanga, was on March 26 shot dead by a police sergeant.

Apparently, Malick 'was not in sound mental health'. Read the whole story on the front page of The Gurdian Issue No. 447, Friday April 3, 2009.

With their guns they will finish us and once they do that, they will start killing themselves!
 
Nadhani hawa wanaopewa hizi bunduki hawajui maana yake! My Incident!!......

Jumamosi ya tarehe 21/03/2009 nilisafiri kwa gari binafsi kuelekea Arusha, sasa wakati narudi on the same date kufika maeneo ya Memorial (uwanja wa saba saba) kuna cheki pointi pale na nilisimamishwa na askari polisi aliyekuwa pale. kama kawaida alinidai kadi ya gari niukampatia,then akanidai na driving licence nikampatia pia, kisha akaniuliza gari ni la nani, nikamtajia jina ambalo liko kwenye kadi! yule bwana alitoa bunduki yake begani na kuniamuru kupaki gari pembeni zaidi ya barabara kwa madai kuwa kadi ya gari na leseni vina majina tofauti!! (maajabu) kidogo nilidhani anatania kumbe haikuwa hivyo;jamaa alikuwa siriasi huku kaishikilia bunduki yake sawa sawa...kibaya zaidi yule askari alikuwa hajui jina la mmiliki linaandikwa wapi kwenye kadi!! kwanza alidai jina nililokuwa namtajia ni tofauti na lile lililoko kweny kadi,pili leseni nayo ilikuwa na jina tofauti!!kichekesho zaidi ni kuwa yule askari (napata kichefuchefu kumwita hivyo) alikuwa anasoma kwenye muhuri wa advocate aliyeidhinisha ile kadi kwani ilikuwa ni kivuli(photocopy)! tuligombana kwa muda na alikuja mwenzie aliyekuwa kwenye ki-hyundai kilichokuwa kimepaki chini ya miti lakini hakuzungumza kitu! kwa kweli pale nilishikwa na hasira na ilibidi niliyekuwa naye kwenye gari amueleweshe yule jamaa ambaye kwanza alikuwa anayumba kwa ULEVI,na pili alikuwa hajui anatafuta nini!
swali langu
Hivi hakuna utaratibu wa kuwakagua wanaopewa silaha kabla ya kuzichukua?
Je! hakuna utaratibu wa kufanya ukaguzi kwa wale walioko kazini hasa wenye silaha

Kama hizi silaha wanaweza kupewa walevi kama yule aliyekuwa pale siku hii tutarajie mengi!watatumaliza hawa jamani!
 
Hawa jamaa ni wajinga sana. Nakushauri kitu kimoja, kwa ulevi wao, kutoelewa sheria wanazo zi enforce, Njaa ya pesa waliyonayo ndiyo inasyosababisha mambo kama haya na yale ya type ya Kamanda wao zombe. Wakati mimi nasoma 'O' level miaka ya mwisho ya Themanini, nilliuwa nasoma na watu wajinga sana, walevi, wavuta bangi, wezi wa mali za shule na wanafunzi wenzao. Hawa watu nilikuja kuwakuta ni police hapa Dar na wanabeba silaha..... can you imagine.???. Sijatoa ushauri niliokusudia mwanzo... Siku nyingine wakikusimamisha jitahidi sana usi-lose temper... watakupiga risasi halafu wataanza......rirrikuwa rinapambana na porisi tukarishinda....... kazi tunayo wajomaba...
 
Yaani polisi wa Tanzania siwaamini kabisa katika madaraka yao wanayopewa. Kwanza sidhani kama wanapata mafundisho ya kutosha kabla ya kupewa dhamana ya kubeba bunduki. Pili hawa ni wala rushwa wakubwa sana na sasa hivi pia ni wauaji wa Watanzania wasiokuwa na hatua yeyote. Nimewahi kuwa na incidents nyingi na polisi kwa kukamatwa eti wanataka wanifanyie upekuzi nilifanya ukaidi kwa nguvu zangu zote lakini unapoona bunduki inaelekezwa kwako basi unaweza kabisa kupoteza maisha yako, hivyo ilibidi nisalimu amri.

Kuna kesi moja walitaka kunibambikia kesi ile kama ingeenda mahakamani basi ningefungwa kifungo cha miaka mingi sana, bahati nzuri kile nilichoandika katika ile ripoti ya polisi na walichaoandika vijana ambao nao walihusika katika kasheshe lile ilikuja kuthibitika kama ni kweli kabisa ukilinganisha na ripoti iliyoandikwa na polisi. Basi hapo ndipo nikaponea chupu chupu lakini bado walikuwa wanataka niwape michuzi, nikawaambia michuzi yangu wataisikia redioni.
 
... "Sting Operations" ni muhimu katika kupunguza bughudha kama hizi, walau basi kwa kuwa rekodi na kurusha kwenye TV matukio ya kigangwe na ukiukwaji wa haki kama haya, (ITV nadhani walifanya hivi mwaka jana). Kwani kuthibitisha maovu yao mbele ya sheria ni vigumu hapa nchini mwetu kwa jinsi mambo yalivyo shagalabagala pahali pengi kwenye system. Hata wasipohukumiwa, walau "name and shame" itakuwa imejaribiwa.

SteveD.
 
... "Sting Operations" ni muhimu katika kupunguza bughudha kama hizi, walau basi kwa kuwa rekodi na kurusha kwenye TV matukio ya kigangwe na ukiukwaji wa haki kama haya, (ITV nadhani walifanya hivi mwaka jana). Kwani kuthibitisha maovu yao mbele ya sheria ni vigumu hapa nchini mwetu kwa jinsi mambo yalivyo shagalabagala pahali pengi kwenye system. Hata wasipohukumiwa, walau "name and shame" itakuwa imejaribiwa.

SteveD.

ngugu yangu steve, wakishajua unawarekodi si ndio watakumalizia kabisa?
the goodthing kuna jamaa yangu jana kaniletea recording camera ambayo ukiiweka kwenye shati inarekodi vizuri picha na sauti na ni ndogo mithili ya kalamu, nadhani nitaitumia hii whenever I go.
 
Yaani kweli wanataka kutuambia tusiendesha hata magari yenye majina ya wake au waume zetu?? Eti mbona kadi ya gari na leseni majina tofauti. Jinga hilo.
 
Back
Top Bottom