Chupi yako unaanika wapi.................?

mnaanikaje chupi nje jamani...chupi,soksi pamoja na taulo vinaanikwa bafuni tena unafunga taa maalum kwa ajili ya kukausha na kuua bacteria
Huku uswahilini tunakoishi haiwezekani maana choo/bafu ni vya kugombania.
 
As far as I know wanatumia drier. Na sio nchi za baridi tu, hata bongo! Ulishawahi kupata picha mashuka ya hotels, towels na serviettes? Ama hospitali ya muhimbili wafue sghuka, waanike na kuanua? Ila ya taa maalum ndo nilikuwa mbado kuona. Kuishi ni kujifunza, asante kwa kunijuza mkuu.
sio theoretical ndugu ulimwengu mkubwa zunguka uone teknolojia...ushawahi jiuliza zile nchi za baridi kali inayoambatana na snow huwa wanakausha vipi nguo
 
mh.......sasa huku kwangu kwa bi nyau, nikianika kapichu kangu haka ka vikamba kamba tu cjui ndio mnaitaje NAAMBIWA nawatega waume wa wenzangu..................
 
Suala la kunyosha chupi kwangu ni ngumu sana, maana nguo tu ya kuvaa kunyosha ni ishu.
 
Salaam wa JF,
binafsi napenda na sipendi mtu asiye wangu aione chupi yangu pasipo sababu ya msingi, lkn nakuta jirani yangu yeye anafua na hupenda kuanika chupi zao (mke na mume ) nje ktk kamba, siku moja nikamuuliza kwa nini anaanika nguo ya ndani nje haoni kuwa anajivunjia heshima kwa watu na watoto, sikumuona kujali, nawauliza wenzangu ni ipi sehemu bora ya kuanika chupi............!!

wengine tunavaa boxer nasio chupi naomba ulekebishe swali lako maana limekaa kikike zaidi..
 
jamani kwa kua nimeona maoni ya watu wengi wanaanika nje. Ninaanzisha bishara ya utalii wa kyupiz Tanzania.

Kuna zile kubwa zimebana pote

kuna zile kubwa zimebana juu chini zinapepea kama maskio

kuna medium size za krimplin

kuna vikamba kamba (aka migwasho gwasho)

kuna za maua kama bataflai

kuna rangi ya binzari

kuna zile za kuogelea

kuna za maneno(utajiju, karibu, my love) au chata ya jani
hivi VIP bado zipo? Hizi nazipenda sana maana ukijifanya mjuaji tu inapanda hadi shingoni.

Naomba ushauri, nifanye utalii wa picha au wa kwenda mbugani (live kutoka kwenye kamba) ?????
 
Duh, sikuwezi mwali wewe! Utatufunda siku tunakuoza. Sijawahi kupiga pasi pichu in my life! Sasa zile za nanihii si unam
Panga 10 afu unalalisha pasi? Hongera mamito!

me huwa navaa za cotton, zile za naanihii sijawahi kuvaa wala kufikiria kuvaa. afu nisipo pasi nahisi kama zanikwangua. c wajua coton tena!
 
Mi ninazo kama thelathini hivi, navaa zikifika 15 zimechafuka nafua na kuanika hizo 15 zote nje kwenye kamba,then zikifika 15 tena kama kawa,kama una muda wa kuzishangaa nikianika kwenye kamba sawa we endelea ila ziko 30,hauwezi kuzijua zote na hata ukiziona kwenye kamba kesho nikitoka hauwezi kujua nimevaa ipi, ni mke wangu tu anayeweza kujua hivyo unabaki kuwa kama haujaona tu!

na wanaume mnakuwaga na chupi nyingi hivi?kha.hii pata ona bado!
 
mh.......sasa huku kwangu kwa bi nyau, nikianika kapichu kangu haka ka vikamba kamba tu cjui ndio mnaitaje NAAMBIWA nawatega waume wa wenzangu..................

umeona enh ?mi nawambia hawanielewi!ndo mwanzo wa kuwekewa kigoma cha brazil!ahaaha a.k.a kigodoro
 
ukisema sayansi kimu kizaz cha leo ni MSAMIAT MPYA HUO,,,,,ILA ILE ILIKUA NI ELIMU BORA SANA,HADI SASA NAKUMBUKA HATUA ZA KUFUA NGUO MFANO SHATI AU SURUALI,UNAANZIA WAPI HADI WAPI

unakumbuka kunyosha kwa wanga!dah elimu ilikuwa yetu bwana!
 
Wana Jf bana, wana maisha ya kijamaa sana...

ikitoka drying machine inakuwa teyari kuvaliwa.....
 
Back
Top Bottom