Bluray
JF-Expert Member
- Mar 25, 2008
- 3,449
- 127
Bluray,
..watetezi wa hoja kwamba chuo hicho kijengwe ktk mikoa ya pembezoni wanaamini kwamba kitatoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa maeneo hayo.
..vilevile wanaamini kwamba kujengwa kwa chuo ktk maeneo hayo kutalazimisha kujengwa kwa supporting infrastructures kama hospitali,shule,barabara,uwanja wa ndege etc.
..wengine pia wanaamini wananchi wa sehemu hizo ambazo tunasema "zimesahauliwa" watajisikia "vizuri" and part of a "larger Tanzanian-family" kwa mradi kama huo kupelekwa karibu na maeneo yao. wanadai hii itajenga umoja wa kitaifa.
..nakubaliana na approach yako kuhusu suala hili, but sometimes it is hard not to empathise na wananchi wa hii mikoa ya pembezoni.
..wasiwasi wangu ni kwamba unaweza kujenga chuo hicho huko pembezoni halafu wananchi wa maeneo ya karibu wakabaki kuwa watazamaji tu wakati wanaosoma hapo ni vijana toka maeneo ya mbali.
NB:
..leo hii ukiwapa wananchi wa Kigoma/Lindi/Mtwara/Tabora hayo mabilioni yaliyopangwa kujenga chuo cha Mandela watumie kwa ajili ya elimu, je watatumia pesa hizo kujenga shule za sekondari kadhaa au kujenga chuo kikuu kimoja?
Inabidi tuwe na "from the ground up approach", badala ya top down approach.Inabidi miradi na huduma ziende kwenye proven demand, siyo ku speculate kuwa tutapata demand. Haya mambo ya top down ni part and parcel ya command system, vijiji vya ujamaa, ma hudro electric project makubwa ambayo tunakuwa bilked "Confesion of An Economic Hitman" style.
Tengeneza mazingira ya wananchi kuwa na proven demand ya chuo, kwa kuanzisha shule za sekondari nyingi, then ukiwa na demand, au hata projection nzuri ya demand, unajenga chuo.Sio unajenga chuo kikuu sehemu inayohitaji shule za msingi na sekondari.