Ni kosa kubwa kwa mkusanyiko mkubwa wa wanafunzi pale UDSM kutokuwa na chombo chao kinachowaongoza katika mambo mbali mbali ndani na nje ya chuo hicho. Wanafunzi wanaweza kabisa kuunda DARUSO yao ya chini meza na kutaarifiana mambo mbali mbali kuhusiana na yale yanayowapa karaha mbali mbali katika muda ambapo wapo pale kama wanafunzi.
Serikali wasomeshe watu bure harafu wafute hiyo DARUSO.
Tanzania ni masikini acheni matusi hapa,kitendo cha mzee wangu kule kwenda kufua na kuoga kule motoni ni kielelezo tosha hata basic needs zake hawezi tosheleza.
Acheni propagada hapa eti anatumia pesa vibaya wanazitowa wapi hizo fedha za kutumia vibaya kama NESI analipwa elfu 70 kwa mwezi kwa mwaka anakuwa na laki 8 na unamtaka mtu huyu alipe laki 5 kwa mwaka atazitowa wapi na mda wote yupo kazini?
Tena huyu Nesi kwa Tz eti ndiye anaishi maisha yale STD,Acheni matusi kabisa Tanzania ni masikini acheni matusi kabisa.
Kama serikali yenyewe imefanya ile ada ya shule za msingi bure eti kwa kigezo kuna watoto wanashindwa pata ile ada je? unategemea huyu mtoto ataipata hii ya chuo?
Anatumia fedha vibaya wapi kwa ile chupa ya gongo ya USD 0.015 na kiasi hicho cha fedha kulewesha watu 10 hiyo ndiyo matumiza mabaya?
Hivi wewe ulishawahi kuona mtu amevaa nguo ambayo imepigwa viraka hadi nguo inapoteza rangi yake kutokana na kuwa viraka ni seheemu kubwa kuliko nguo original?
Hayo matumizi mabaya ya fedha ,hizo fedha wanazipata kwa kilimo cha mkono? ama uvuvi wa kutumia kasia?
Hakuna NESI hospitali serikali analipwa 70,000 p.m angalia vema record zako. Mishahara Afya imeboreshwa kuliko sekta zinyine 2006 kima cha chini ni 150,000 hadi 200,000.
Wengi mnakaa Ughaibuni na hatufanyi utafiti wa kutosha kwanza...kwa kifupi to some sektas life and pay is better now than before!
Utashangaa unakaa Ulaya ukifika Tz peers wako wako mbali na wamekuzidi kimaendeleo mbali!
Karibuni nyumbani tujenge taifa!
Hii imekaa vizuri na inatia moyo kuona kuna baadhi ya viongozi wanakuwa na mtizamo tofauti na sera zilizowekwa ambazo zinaonyesha wazi kuwabagua watu.
Sulihisho la hili tatizo ni kuwa na kigezo kimoja tu cha kupata mkopo na sio huu utaratibu wa kuwa na asilimia 100,80,60... hii ni uzushi wa wazi kabisa kwani kwa nchi kama TZ hauwezi kupima kipato halisi cha mtu na mtu anaweza kujaza hizo form kwa namna yeyote ile. Pili kwani hata hao wenye uwezo sio kwamba wazazi wao wameokota tu hizo pesa .. wamezinfanyia kazi so nao pia hauwezi kusema serikali iwatenge.
Suluhisho ni moja tu.. kuweka grade... yeyote atakayepata division I ukipata hiyo basi unapata mkopo asilimia 100 bila kujali unatoka familia masikini ama tajiri. Hiyo ndio njia ya kuondoa ubishi wote huu.
Mwisho najiuliza serikali ni nani??? mbona huyu jamaa kiongozi mkubwa bungeni akiwa kama mwenyekiti wa kamati na yeye anasema serikali iwe makini... nilitarajia angetoa kauli yake akiwa yeye kama hiyo serikali... hii inasikitisha kuona kwamba hata hao viongozi nao wenyewe wanajiona sio serikali sasa serikali ni nani..????
Wee acha propaganda
Huu mtazamo wako wa kushindana kimaisha sijui peers na kitu gani ,ni propaganda zinahusiana nini na umasikini wetu.wewe unafanya kushindana na aliye ulaya ili uje umzidi hapo ndipo tatizo la ufisadi lipoanzia ,kwanza umemzidi kwa lipi? kielimu,kimali za kufisadi wananchi ,kimtazamo ama kinini?
Wewe huoni aibu kwa serikali ya Poland kunipa mimi elimu bure toka bachala hadi masters wakati serikali yetu yenyewe inanyima watanzania elimu ni Upuuzi kabisa.
Hawa wapolish mbona wameweza kunimpa mimi msaka nyoka elimu ya bure yumkini si raia wao ni vipi serikali yetu inashindwa kulipia watu wake???
kwanza ni aibu tupu.
Jamani mwenye data nzuri ya fungu wanalopata wafanyakazi wa serikali kwa ngazi zote watuwekee hapa.
watu wana entertain atoms za kipuuzi kabisa
Samahani kwa maneno makali
Hatimaye Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika mkakati wa kuhakikisha kwamba wanaingia chuoni wale tu wanaostahili, kuanzia tarehe 18--23, Menejimenti ya Chuo imetoa ilani kwa watumiaji wa njia zinazopita chuoni hapo kutotumia njia hizo! kwa maana nyingine kwa mjibu wa ilani hiyo ambayo nimebahatika kuiona milango miwili ama geti mbili tu zitatumika, kuingia chuo italazimika kupita geti maji na kutoka itakuwa geti la Chuo cha ardhi, mageti mengineyo kama Changanyikeni nk hakuna ruksa hata kidogo! katika kipindi hicho! sisi wakaazi wa Changanyikeni nk tunashauriwa kutumia njia ya msewe kuelekea Ubungo na kama tunahitaji kwenda Mwenge basi njia ni Makongo juu! wanafunzi wa shule za msingi wataruhusiwa kupita katika lango la chuo kama tu watakuwa na sare zao za shule, na kwa wafanyakazi wote wa chuo watalazimika katika kipindi chote hicho kutumia vitambulisho vyao na kuwaonyesha walinzi wa chuo auxiliaries vitambulisho vyao! na kwa kada nyinginezo kama Wanajeshi wote watalazimika kutii utaratibu huo uliowekwa na Chuo, mh! ndiyo mambo hayo ya private roads nk wana exercise jurisdiction yao! Ilani haijasema kwasisi wengine ambao makulaji yetu na masuala ya chinywaji tunategemea UDASA club, Hillpark nk status yetu ni vipi? lakini pia kwa wengineo tulio na marafiki na ndugu wa karibu malekchara hapo mlimani ilani haijasema kabisa inakuwa vipi? ama kama ninashida yoyote itakayonilazimu nifike chuo itakuwa vipi? Je uamuzi uliochukuliwa umezingatia kabisa mibadala yote ambayo ingewezekana kuchukuliwa? ama ndio haya mambo ya kumeneji ki makenika? Je kulikuwa na ulazima wowote wa kutupa adhabu sisi wakazi wa pembezoni mwa chuo? ama wananchi wengine wa kawaida? ama tunapata adhabu kimtindo kwasababu ya ndugu na wadogo zetu 'jeuri'?
Shy si nasikia Udasa club ni kwa members wa udasa only? sasa wewe ufuate nini huko while si member wa udasa? na hapo hillpark unaposema kwani ni lazima ukale hapo?? au ndo kujiamini kwako kwa kutaka kuwapima polisi kama wana ubavu au la?? hahahaha haya bwana lakini kumbuka KUNGURU MJANJA..............................??