Chuo Kikuu cha Udaktari Bugando.KIBOVU TANZANIA NA INAENDESHWA KISANII.

CHIETH

Senior Member
Aug 15, 2011
179
67
CHUO KIKUU CHA UDAKTARI CUHAS-BUGANDO NI CHUO CHA UBABAISHAJI. HIVI MAJUZI mKUU WA KITIVO CHA UDAKTARI ALITAKA KUWAFUTIA UDAHILI WANAFUZI WA MWAKA WA TATU ETI HAWAKUFANYA MITIHANI KATIKA MASOMO AMBAYO HAWAKUFUNDISHWA. cHUO HIKI KINA MATATIZO MAKUBWA YA UFUNDISHAJI HASA KWA MASOMO YA UDAKTARI. MADAKTARI WANARINGA, WANATUKANA WANAFUNZI, HAWAFUNDISHI NA WAMEJAA MAJIGMBO. hUENDA MADAKTARI WANAOTOKA HAPA WAKAWA WABOVU ZAIDI. TUNAOMBA WAZAZI MUWE MACHO NA CHUO HIKI KAMA MNAWATAKIA WATOTO WENU MAENDELEO MEMA.

Haya yalikuwa ya huko nyuma,semester iliyo pita. Hata hivyo kwa sasa kuna mabadilko makubwa baada ya thread hii hapa miezi miwili iliyopita. Wanafunzi wa mwaka wa 3 (2011/2012) wanapata dose ya shule kama inavyohitajika.

Kwa hili ninaomba wanaJF kuwapongenza uongozi wa CUHAS_Bugando kwa kuwa wasikivu na kufanya maboresho makubwa sana ya ufundishaji.

Ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu wanaJF kwa maoni.
 
poleni sana kwa matatizo hayo. kimsingi mfumo mzima wa elimu hapa bongo umeharibika vibaya na siyo bugando tu, vyuo vingi vya medicine wanalalamikia ubora wa elimu ktk vyuo vyao hasa katika masomo ya basic science na kujikuta wanahesabu miaka yao mitano iishe tu ili wapate magamba yao na kurudi mtaani watajuwa mbele kwa mbele. cha msingi mnapaswa kutambua changamoto zilizoko vyuoni (kama ukosefu wa walimu sababu mara nyingi utakuta wanaofundisha ni wanafunzi pia, yaani MMED anamfundisha undergraduate) na mchukue tahathari wenyewe kwa kukomaa kivyenuvyenu kama kwa kutumia sources mbalimbali kama vitabu, intenet n.k kujisomea kama open university vile ili kufukia hayo mashimo japo kiduchu.poleni sana
 
Ni jana tu, nilikuwa mahali, likanijia wazo kuusu ubora wa elimu yetu katika vyuo vya udaktari.
Kama nako mambo ni haya, basi tumekwisha. Wahusika wanajua haya.
Tujiulize kwanini wakiumwa immediately wanakimbilia India.
 
Nilichokuwa nataka muelewe wanajammi forum ni kwamba chuo hiki kinaendeshwa bila kufuata misingi ya viuo vikuu na haitimizi malengo ya TCU. Nasema hivi kwa sababu chuo kimeshindwa kuwa na lecturers wa clinical subjects. Wanafunzi wanaorotate kwenye departments mbali mbali hapo bugando kwa kweli wanatukanwa, wanabezwa, wakati hao wanaotukana hawajawi kuingi darasani kufundisha. Natoa mfano wa somo linaloleta ugomvi kati ya MD3 na Dean wa fuculty of medicine, Management of diseases. Somo ilitakiwa ifundishwe tangu MD1 hadi semester ya 7. Somo hili limekuwa haifundishwa ipasavyo na kumekuwa na ubabaishaji mkubwa. Wanafunzi hao wamekuwa wakilalamika eti wafundishwe laikni waliambulia patupu. Ndipo walipo amua kuandika barua kwa dean ili mtihani uhairishwe hadi hapo watakapofundishwa. Dean badala ya kutumia busara ya kimenejimenti akaamua kutumia udikteta wa makadaktari kujiona kuwa ni watu bora zaidi duniani.
Swala hili ndugu zangu halijaisha na hivi sasa dean na kamati yake inampango wa kuwatungia mitihani migumu wanafunzi hao ilibaadhi yao wadisco.
Kuna uwezekano wanafunzi wengi wa bugando wakadisco next semester. Naombea mfutilie swala hili la Bugando wana usalama wezangu. Huenda serikali ikapoteza haela nyingi iliyokwisha wekeza kwa wanafunzi hawa.
Ahsante sana.
 
Si ajabu kwani hata marks za kujiunga tofauti na muhimbili, teh!
sidhani kama marks za kujiunga zinaweza kuwa sababu katika hilo. nilichomwelewa mtoa maada ni kwamba analalamikia kutofundishwa katika masomo husika. sidhani hata hao unaodhani walifaulu kwa kiwango cha muhimbili wanaweza kufaulu kwa kiasi wa walichofaulu huko kwa mazingira kama ya bugando
 
Nilichokuwa nataka muelewe wanajammi forum ni kwamba chuo hiki kinaendeshwa bila kufuata misingi ya viuo vikuu na haitimizi malengo ya TCU. Nasema hivi kwa sababu chuo kimeshindwa kuwa na lecturers wa clinical subjects. Wanafunzi wanaorotate kwenye departments mbali mbali hapo bugando kwa kweli wanatukanwa, wanabezwa, wakati hao wanaotukana hawajawi kuingi darasani kufundisha. Natoa mfano wa somo linaloleta ugomvi kati ya MD3 na Dean wa fuculty of medicine, Management of diseases. Somo ilitakiwa ifundishwe tangu MD1 hadi semester ya 7. Somo hili limekuwa haifundishwa ipasavyo na kumekuwa na ubabaishaji mkubwa. Wanafunzi hao wamekuwa wakilalamika eti wafundishwe laikni waliambulia patupu. Ndipo walipo amua kuandika barua kwa dean ili mtihani uhairishwe hadi hapo watakapofundishwa. Dean badala ya kutumia busara ya kimenejimenti akaamua kutumia udikteta wa makadaktari kujiona kuwa ni watu bora zaidi duniani.
Swala hili ndugu zangu halijaisha na hivi sasa dean na kamati yake inampango wa kuwatungia mitihani migumu wanafunzi hao ilibaadhi yao wadisco.
Kuna uwezekano wanafunzi wengi wa bugando wakadisco next semester. Naombea mfutilie swala hili la Bugando wana usalama wezangu. Huenda serikali ikapoteza haela nyingi iliyokwisha wekeza kwa wanafunzi hawa.
Ahsante sana.
walimu wa hayo masomo wapo? vinginevyo swala litabaki palepale, mfumo mzima wa elimu uko distorted toka juu hadi chini. sina uhakika sana na uwajibikaji wa tcu sababu kuna mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakifanyika kienyeji lakini tcu kama chombo kinachosimamia uendeshaji wa hivi vyuo hawajasema chochote. nyinyi huko mnalalamikia kutofundishwa clinical skills lakini pia kuna vyuo vya medicine havina walimu wa pathology kabisa, somo ambalo ni key katika medicine na tcu wanalitambua hilo lakini hakuna tamko lolote toka kwao. vyuo vingi vya binafsi wanaweza kufuatilia ulipaji wa ada tu kwa maana wako kibiashara zaidi na hawajali ufanisi ktk elimu wanayotoa
 
Ni jana tu, nilikuwa mahali, likanijia wazo kuusu ubora wa elimu yetu katika vyuo vya udaktari. <br />
Kama nako mambo ni haya, basi tumekwisha. Wahusika wanajua haya.<br />
Tujiulize kwanini wakiumwa immediately wanakimbilia India.
<br />
<br />
kwa sababu tanzania hakuna madaktari ila ubabaishaji tu! Walimu wa kufundisha hakuna je,hao wanafunzi wajisomee mwenyewe kama wanavyosoma kiswahili? Ukizingatia midude yenyewe migumuuu
 
Back
Top Bottom