Chuo Kikuu cha Nelson Mandela

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
Serikali ya Tanzania inawekeza zaidi ya Tsh Bilioni 30, kujenga Chuo kikuu kipya cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela huko Arusha. Chuo hicho kitakuwa cha pekee barani Afrika na kitatoa Shahada za Uzamili na Uzamivu.
libeneke lake hili hapa: NM-AIST Arusha.
Watanzania tutumie nafasi hii kupata wataalam waliobobea katika Sayansi na Taknolojia
 
"Chuo hicho kitakuwa cha pekee barani Afrika" ??????????????
  • Hivi mbona watanzania tunapenda sana maneno haya ya; "ya kwanza, ya aina yake', cha pekee! Jamani,bado sijaona results za kipekee kama tunavyopenda kujisifia kuhusu taasisi zetu. Hebu kwanza tuboreshe products zetu zionekane kwamba kweli zinatoka kwenye taasisi / kiwanda cha kipekee!
 
Upekee wake ni kule kuingiza siasa kwene realities...au huo sio upekee? tangu lini chuo kikatumika kama mabango ya kumnadi mgombea uraisi kama sio upekee huo? nalala niote ndoto nzuri mie ngoja niache hasira jinamizi la JK lisijenibana buree
 
Jamanii tatizo hivi vyuo vinaazishwa bila mipando. Vyuo vilivyopo vinatushinda kila kukicha migomo na migome ni ya madai ya kweli si uongo. Baada ya kuboresha kwanza hivi vilivyopo kama dit ,ardhi,udsm ,mzumbe ambavyo kwa kweli vinahitaji uboreshwaji mkubwa sana lakini matokeo yake tunakimbilia kuazisha vyuo vingine. Mfano hicho udom kimeazishwa kisiasa lakini elimu inayotolewa pale hakuna kitu hata kidgo.
Ushauri kwa hawa viongozi ambao wako kisiasa zaidi boresheni kwanza hivi vyuo vilivyopo.
 
Waratibu wanadai Chuo hiki ni cha pekee kwa maana kitatoa Shahada za Uzamili na Uzamivu yaaani Masters degree na Doctorate tu.
hakuna Shahada za kwanza hapo. na experience inaonesha matatizo mengi ya migomo ktk vyuo vyetu vinginevyo ni ile ya wanafunzi wa Shahada za kwanza au chini yake. sijawahi kusikia Mwanafunzi wa Masters degree au Doctorate anagoma.
 
"Chuo hicho kitakuwa cha pekee barani Afrika" ??????????????

  • Hivi mbona watanzania tunapenda sana maneno haya ya; "ya kwanza, ya aina yake', cha pekee! Jamani,bado sijaona results za kipekee kama tunavyopenda kujisifia kuhusu taasisi zetu. Hebu kwanza tuboreshe products zetu zionekane kwamba kweli zinatoka kwenye taasisi / kiwanda cha kipekee!
Nani unataka ukuboreshee products unazosema??, kama wewe mwenyewe hujafanya hata theluthi kuboresha hizo products!!!. Charity begins at home. Jiulize mpaka sasa umeifanyia nini nchi yako sio KULAUMU tu kila kitu.
 
Upekee wake ni kule kuingiza siasa kwene realities...au huo sio upekee? tangu lini chuo kikatumika kama mabango ya kumnadi mgombea uraisi kama sio upekee huo? nalala niote ndoto nzuri mie ngoja niache hasira jinamizi la JK lisijenibana buree
...hivi kuna Sheria ambayo inamzuia Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya juu kushiriki siasa ktk Nchi hii???!!.hebu tuanzie hapo. Zingatia pia hawa viongozi wengi waliopo hususani wabunge walijinadi ktk kampeni zao kutaka kuchaguliwa kwa kuwa tu waliwahi kuwa mawaziri/marais wa Vyama vya wanafunzi vyouni kwao, SIASA hizo.
 
Naomba msaada na kuelimishwa. Elimu hasa nini?

Nchi yetu imetoa graduates kibao tangu tupate uhuru lakini mambo ni yaleyale. Makandarasi wanaojenga barabara mbovu na majengo mabovu wanya madigrii kibao, madaktari wanaopasua watu vichwa badala ya miguu ni madaktari bingwa, wasomi, wanaopanga mipango mibovu isiyotekelezeka ni wasomi. Tatizo letu sisi tunapenda makuu lakini wavivu, hatupendi hata kufikiri.
 
nice, till we see what have been attained then we can be at a good point whether to say CHUO CHA PEKEE OR NOT
 
Back
Top Bottom