Chuo Kikuu cha DSM Kinaendeshwa kisiasa?

Ndugu, ukistaajabu ya Musa utaona ya Firahuni, Siasa katika vyuo vyetu ni tatizo linalozidi kukuwa siku hadi siku, utakumbuka uwepo wa wimbi la wanasiasa wenye vyeti feki toka katika vyuo vyetu ni moja ya impact tunayoiona leo kutokana na mfumo siasa kujipenyeza katika mfumo taaluma wa elimu.
Jiulize wale waliomtunuku JK Phd ya heshima walikuwa hawahawa wanazuoni wenye kufuata mrengo wa kitaaluma ama walikuwa wanazuoni-siasa, wenye kufanya lolote elimradi kuwaenzi na kuwafurahisha watawala?
Baregu aliondoka hapo UDSM sababu ya kuwa ktk opposition,
Dadi aliondolewa pale Arusha sababu ya kuwa Opposition,
Leo wahadhiri wataalamu wananyimwa mikataba ya nyongeza pindi wanapogundulika ni wapinzani wa mabwanyeye

mwasisi wa huo mchezo ni Mwl Nyerere,katafute Historia ya akina Christopher Kasanga Tumbo,Prof Babu,Oscar Kambona,Mzee Aboud Jumbe uone walivyofanywa na mwl Nyerere wakati waliyoyasimamia ndio leo yanatokea,Kambona alipinga ujamaa wa kisiasa wa nyerere akafukuzwa,mzee jumbe alipigania serikal 3 akafukuzwa,nan leo naweza akawapinga hawa wazee!
 
Wewe nawe usiwe punguani hakuna kitu cha Serikali kisichoendeshwa kisiasa, ndio maana watu wanataka uongozi.

Ingekuwa Serikali na taasisi zake haziendeshwi kisiasa ni nani angegombea uongozi wa siasa?
Men, universities are independent institutions all over the world. Hizi ni taasisi ambazo serikali huwa haipaswi kuziingilia kabisa. Fuatilia kokote kwingineko duniani, except Africa na hasa Tanzania.
 
Men, universities are independent institutions all over the world. Hizi ni taasisi ambazo serikali huwa haipaswi kuziingilia kabisa. Fuatilia kokote kwingineko duniani, except Africa na hasa Tanzania.

Independent institutions only if they were created independently. Why don't you ask Nyerere supporters why he made everything "mali ya umma" and they all failed. He failed to realize that Universities are independent bodies. Blame his system.

Kikwete is changing all that, with katiba mpya.
 
wewe unategemea nini wkt chuo kiko chini ya Prof. Mukandala? je hujui Mukandala na Kikwete wakoje? Je hujui kwamba Bana naye ni mtu wa karibu wa Mukandala? tena Muhaya mwenzie.

Dr. kitila asingeweza kupewa, kwani pale school of Education aliyopo kuna fungu kubwa sana la Pesa kila mwaka kwa ajili ya Teaching Practice (TP), na ile pesa inaliwa na VC, 2 DVCs, Dean of School of Education na TP Coordinator. Hivyo, kumweka Dr. Kitila pale ni kujua ni kwa namna gani kuna pesa inapitia pale Education kwa ajili ya wakubwa wa chuo kama ilivyo REDET.

Dr. Kitila alikuwa na sifa zote za kuwa Dean of School, kwani ni Senior Lecturer toka mwaka juzi na amewahi kuwa mkuu wa Idara, na zaidi yuko smart.

Infact, msitegemee makubwa chini ya Prof. Mukandala, kwani hata yeye nafasi hhiyo alipewa kwa upendeleo wa kisiasa na JK.

Hilo jina la kitila limekakaa kama la kichaga. Sasa kama huyo Kitila ni mchaga unategemea hizo pesa zingesalimika?
 
Ni katika uongozi wa akina Mukandala na wenzake ambapo UDSM inaonekana kukosa mwelekeo na kuwa tawi la chama cha ccm.Mukandala na REDET na usawhiba wake na JK ni vitu vilivyowazi kabisa.usitegemee Mukandala kucheza ngoma tofauti na muziki wa JK.Thamani ya UDSM pengine inaweza kurudi mara tu ya Mukandala kumaliza muda wake na wakti huo JK akiwa amemaliza uongozi wake ,la sivyo atapenyeza ushawishi wake kuweka kiongozi dhaifu kama yeye na hapo sasa ndio utakuwa mwisho wa hadhi ya udsm milele.Muundo wa udsm sasa unaruhusu school au college kuwa na votebook yake na kusimamia mapato yake ya kawaida ingawa 20% ya mapato yote yanaingia kwenye fuko kuu ambalo ndilo Mukandala na Mgaya wanatumia.Hivi kila school ina admistrative machinery and structure ya kuhandle issues zote bila kutegemea decisions kutoka kwa akina Mukandala.Kwa vyovyote vile bia kuwa ccm partisan wakti pale UDSM hakika wewe pia ni mzigo kwa menejiment.
 
Back
Top Bottom