Chuo cha Mapenzi chafunguliwa Morogoro

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Wale washauri nasaha, na wanasaikolojia wanaotoa huduma ya ushauri katika kituo cha MARINATHA mjini morogoro wameamua sasa kufungua chuo maalumu kwa ajili ya kufundisha mambo ya mapenzi kwa vijana na wanandoa.

Baadhi ya kozi zitakazofundushwa ni pamoja na
A. Kwa ajili ya wenye ndoa au walio kwenye mahusiano
1. Namna ya kutawala 'mapenzi' ukiwa katika masomo (jinsia zote)
3. Mwanaume bora kwa mpenzi wake (kwa ambao hawajaoa lakini wana wapenzi) (wanaume tu)
4. Mwanamke bora kwa mpenzi wake (kwa ambao hawajaolewa lakini wana wapenzi) (wanawake tu)
5. Mume bora kwa mkewe (wanaume tu)
6. Mke bora kwa mkewe (wanawake tu)
7. Namna ya 'kumhandle' mpenzi asiye mwaminifu (jinsia zote)
8. Namna ya kufanya unapohisi mwanandoa mwenzio sio mwaminifu (jinsia zote)
9. Vikolezo vya kumfanya mpenzi wako aamue kufunga ndoa na wewe (jinsia zote)
10. Vikolezo vya kunogesha tendo la ndoa/ngono. (wanaume peke yao na wanawake peke yao)

B. Kwa ajili ya walio 'single'
1. Sifa za mwanaume mwenye mapenzi ya dhati (kwa wanawake tu)
2. Sifa za mwanamke mwenye mapenzi ya dhati (kwa wanaume tu)
3. Namna ya kuishi ili uwe mwanaume bora kwa wanawake (kwa wanaume tu)
4. Namna ya kuishi ili uwe mwanamke bora kwa wanaume (wanawake tu)
5. Jinsi ya kumtongoza mwanamke (kwa wanaume tu)
6. Jinsi ya kumtongoza mwanaume (kwa wanawake tu)
7. Namna ya kufurahia maisha bila mpenzi

Kwa sasa wadau wa chuo wanakamilisha hatua za mwisho za usajili. Chuo ilikuwa kianze tangu mwaka 2010, lakini kulikuwa na mabishano makali juu ya kuruhusiwa wananfunzi, na pia mtaala wa kozi ya 'vikolezo vya kunogesha tendo la ndoa/ngono' uliwekewa ngumu na wizara ya utamaduni, hata hivyo tumefanikiwa kuwaelewesha na baada ya marekebisho kidogo ya kupunguza 'makali', mtaala umekubaliwa.

Baada ya siku chache watatoa matangazo kwenye magazeti na vipeperushi.

Vyote mnakaribishwa.
 
****** mwili mzima . Badala ya kufundishi jinsi ya watu kujiondo kwenye umasikini wanafundisha mapenzi . Kweli kwa mtindo huu sijui kama ukimwi utaisha.
 
Dahhh. Nahamu ya kupata PHD ya mapenzi .. je ni practical na theory? Au ni moja kati ya hizo mbili ..

Ni practical na theory, maadili ya kitanzania yakizingatiwa. Hata hivyo tangu awali washauri hawa walikuwa wanafanya 'ushauri' wa faragha kama watu wawili wakijitokeza na kuthibitisha kuwa wao ni wanandoa/wapenzi...
 
I'm more interested in practical bit ..

Maadili ya kitanzania yatakayo zingatiwa ndio
Yapi hayo.?
 
I'm more interested in practical bit ..

Maadili ya kitanzania yatakayo zingatiwa ndio
Yapi hayo.?

AfroD kama wewe ni mTz si unajua sio maadili kuvuana nguo (zote) hadharani (kwa mfano). Japo kwa kuwa ni watu wazima, demonstrations za kutumia madoli, picha na video zimekubalika...
 
Mapenzi huwa nayaona kama ni an art na kwa sehemu ndogo sana kama skills ambayo mtu huipata kwa training, by the way, haya mambo yakiendekezwa nchi itaondoka na umaskini kweli???
 
****** mwili mzima . Badala ya kufundishi jinsi ya watu kujiondo kwenye umasikini wanafundisha mapenzi . Kweli kwa mtindo huu sijui kama ukimwi utaisha.

Walijaribu kufanya hivyo lkn wakashindwa. Ni kile kilichokuwa cha TANESCO. Bora kibadilishiwe matumizi mwenzangu loh!
 
Mapenzi huwa nayaona kama ni an art na kwa sehemu ndogo sana kama skills ambayo mtu huipata kwa training, by the way, haya mambo yakiendekezwa nchi itaondoka na umaskini kweli???

Kuna vitu vinaitwa BA na MA huko mavyuo vikuu, so art inafundishwa. Na kuna faida gani nchi ikawa na utajiri na watu wasio na furaha?
 
Haya mambo huwa ni natural (ya asili), hakuna mtu anaefundishwa. Kama ni kweli, hawa wanataka kula pesa za watu tu. Kwa watakaoenda kusoma chuoni hapo naomba wamuulize mwalimu wao kama alifundishwa kutongoza (mwanaume), na kama alifundishwa kujibu wakati anatongozwa kwa mara ya kwanza (mwanamke).
 
Wanafanya hivyo kwa sababu wamekuwa wakipata watu wengi sana wenye matatizo ya mahusiano wakitaka ushauri, na kuwa wanaona kuwa kuna basic things watu wengi hawajui, ambazo zikiwa applied zinapunguza matatizo.

Kama ni suala la kula ela, sidhani maana tangu mwanzo walikuwa wanalipisha kati ya 20,000 na 100,000 kwa ushauri na wameponya mahusiano mengi...
 
Cjui kinaanza lin na sh.ngap mana nahitaji mastar ya utongozaji watoto wazury wazury,af cjui wanafundisha na kutongoza wake za watu?
 
Ni practical na theory, maadili ya kitanzania yakizingatiwa. Hata hivyo tangu awali washauri hawa walikuwa wanafanya 'ushauri' wa faragha kama watu wawili wakijitokeza na kuthibitisha kuwa wao ni wanandoa/wapenzi...

Dah, kwa hiyo pana vitanda na mabafu kwa ajili ya practical?
Na dawa za penzi zipo?
 
Dahhh. Nahamu ya kupata PHD ya mapenzi .. je ni practical na theory? Au ni moja kati ya hizo mbili ..

practical yawezekana kweli......................maana mtenda na mtendewa yabidi wawe wanapingu.........
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom