chukua dakika 1 kutafakari juu ya taswira hii

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
497
Watoto%2Bwanoishi%2Bkatika%2Bmazingira%2Bmagumu%2Bwakiwa%2Bwamejipumzisha%2Bkatika%2Bmaegesho%2Bya%2Bmagari%2Bkatikati%2Bya%2Bjiji%2Bleo.jpg
 
taswira iliyonijia ni....maisha bora kwa kila mtanzania
 
Kwa hawa vijana maisha hayana maana na wakikua naona wataihukumu jamii inayowatesa kwa kufanya wasiyathamini maisha yao!!
 
watatoka wakianzia wapi? Lazima wawe na msingi wa kuwawezesha kutoka-ukweli unabaki pale pale, maana ya maisha bora kwa kila mtanzania c kumuhudumia kila mtu-ni katika suala zima la sisi wote kufanya kazi kwa bidii. Kazi ni pamoja na malezi bora kwa mtoto kama mzazi. Hii imetokana na wazazi ether kuzaa watoto wengi na kushindwa kuwahudumia au ni watoto wanaotelekezwa na wazai wao baada ya kushidwa kutoa huduma. Hapa claumu serikali wala rahisi. Ukweli ni kwamba lazima tuwe na utamaduni wa kuzaa watoto ambao tuna uwezo wa kuwatunza. Tusipobadilika katika hilo-Afrika hatutaendelea.

Ushuri wangu kwa wana JF-Amini nawaambia laana unayoipata kwa kumtelekeza mtoto ni kubwa na huwezi kuwa na maisha ya furaha duniani. Ni bora kuzaa watoto ambao una uhakika utaweza kuwatunza kama mzazi bila ya kutegemea msaada wowote kutoka kwa watu wengine.
 
......Inasikitisha kuona hawa watoto wapo katika hali hii.
Halafu ili wimbi la watoto wa mitaani naona linazidi siku hizi, utakuta katoto kadogo kanaomba omba.
Hili si kosa la serikali, ni kosa la wazazi.........mtu kama huwezi kuhudumia watoto nafuu usizae maana ukizaa na watoto wakiwa na maisha kama haya ndio mwanzo wa kuzidisha wimbi la vibaka mitaani.

Watoto kama hao hawana future nzuri maisha yakiwa magumu ndio hao wanaofanya vitendo vya kuhatarisha maisha ya watu.
 
watatoka wakianzia wapi? Lazima wawe na msingi wa kuwawezesha kutoka-ukweli unabaki pale pale, maana ya maisha bora kwa kila mtanzania c kumuhudumia kila mtu-ni katika suala zima la sisi wote kufanya kazi kwa bidii. Kazi ni pamoja na malezi bora kwa mtoto kama mzazi. Hii imetokana na wazazi ether kuzaa watoto wengi na kushindwa kuwahudumia au ni watoto wanaotelekezwa na wazai wao baada ya kushidwa kutoa huduma. Hapa claumu serikali wala rahisi. Ukweli ni kwamba lazima tuwe na utamaduni wa kuzaa watoto ambao tuna uwezo wa kuwatunza. Tusipobadilika katika hilo-Afrika hatutaendelea.

Ushuri wangu kwa wana JF-Amini nawaambia laana unayoipata kwa kumtelekeza mtoto ni kubwa na huwezi kuwa na maisha ya furaha duniani. Ni bora kuzaa watoto ambao una uhakika utaweza kuwatunza kama mzazi bila ya kutegemea msaada wowote kutoka kwa watu wengine.
Kikwete alipoingia madarakani hakusema kuwa maisha bora ni kwetu kufanyakazi bali alisema maisha bora kwa kila mtanzania inawezekana na akaahidi kuyaleta. Mkataba wa TRL ulicheleweshwa kwa mtaalam chenge kuupia kwa makini (akiwa waziri wa miundombinu) leo hii unavunjwa na kuelezwa kuwa hauna maslahi kwa taifa, air tanzania iliwekewa bilions za fedha lakini leo hii hiko chali ... Hayo ndo maisha bora ya kikwete. Unapiga hatua moja mbele unarudi sita nyuma... je, tutafika? Watoto wengi n.k ni sawa lakini siyo agenda rasmi!
 
kwa kweli mie picha hizi zinazoonesha watoto wa mitaani mara nyingi nikiziona hunifanya mnyonge hata siku nzima,na wkt mwingine ninalia maana hawa watoto wanapata sio shida tu ya kukosa chakula,elimu,tiba na sehemu salama za kuishi bali wana maisha ya hatari sana.kukosa kwao elimu na mambo wanayokumbana nayo huku wakiwa hawapati upendo anaostahili kupewa binadamu na hasa mtoto kutawafanya waje kuwa vijana wenye hasira,chuki na wasioogopa kufanya chochote hasa mabaya.hawa watoto leo ni malaika kama walivyo watoto wengine wote,lkn haya mazingira yatawafanya wawe viumbe wabaya sana.
SIO SIRI HUWA NAJIULIZAGA,HIVI MTU AKIWA KIONGOZI WA NCHI HUWA ANAONDOKWA NA ROHO YA HURUMA NA UBINADAMU?.
Kwa nini viongozi wa nchi yangu hawaumwi na roho kama jinsi inavyoniuma mie ninapowaona hawa watoto wa namna hii?
kama roho inawauma kwa nini hawafanyi kitu kumaliza hili tatizo?
kwa nini inawezekana kumjengea GAVANA wetu mjumba kama wa mbinguni badala ya kuprioritize vitu muhimu mojawapo ikiwa ni watoto wanaoteseka mitaani?
nina maswali mengi na kila ninapojiuliza hasira zangu zinazidi kupanda,nadhani napoteza muda kuuliza maswali ngoja nivue hichi kimini nitinge magwanda niingie msituni,nimechoka kulia kwa kuwaona ndugu zangu wakiteseka.
i will be back.
 
mimi natafuta wafadhili kisha naingia nao msituni tukitoka huko ama zenu ama zetu manake sisi maisha kwetu hayana thamani hofu kwenu.....kaeni mkao wa kula
 
Back
Top Bottom