Chuki na unafiki....

.. Wewe kama ni mmoja wa hawa watu wenye chuki na watu usiowafahamu embu chunguza tatizo lako lilipo. Na kama tatizo liko kwao (inawezekana kuna namna wamekuboa) wasiliana nao uwajulishe badala ya kuwachekea kinafiki huku roho yako ikilika taratibu kwa chuki na kujiabisha kwa kujipeleka kwa marafiki zao (watu wanaofahamu kiukweli) na kujifanya wewe unawajua wakati huwajui...

... huku roho yako ikilika taratibu kwa chuki ... !! Lizzy nafikiri inabidi kufuata ushauri ulioutoa hapa kwa sabau tatizo la roho kulika taratibu kwa chuki ni kubwa kuliko inavyoonekana ... infact ni msingi wa magonjwa mengi!

..kabla sija post.. Ni seme ASANTE kwa thread nzuri!! Lol!
 
... huku roho yako ikilika taratibu kwa chuki ... !! Lizzy nafikiri inabidi kufuata ushauri ulioutoa hapa kwa sabau tatizo la roho kulika taratibu kwa chuki ni kubwa kuliko inavyoonekana ... infact ni msingi wa magonjwa mengi!

..kabla sija post.. Ni seme ASANTE kwa thread nzuri!! Lol!
AJ Asante imepokelewa na maoni yamekubalika. Endelea alafu asante yako inakuja.

@ Fynest chuki inaweza kumfanya mchukiwaji aongeze juhudi kwenye shughuli zake kwahiyo inawezekana ikamjenga. Ila sasa ndio awe ngangari , yani hakatishwi tamaa kirahisi.
 
kuna binadamu wana chuki tu...
bila sababu.........

nina ndugu zangu wana chuki kali mpaka najiuliza tuliwakosea nini? angalau hao ni ndugu tumeishi pamoja

lakini kuchukiana kwenye mitandao ya kijamii? hususan kama humu ambapo hata id ni za kutunga? huyo mtu ana tatizo kubwa sana.... akawaone wataalamu wa saikolojia.

kwanza maisha mafupi haya kwa nini umchukie mtu?

ila ndo maisha, ni changamoto tu hizo
 
Yeahhh ni bora umweleze mtu ili kama kweli kakutenda vibaya ajirekebishe badala ya kujitesa mwenyewe.

Huwa nahangaika na baadhi ya rafiki zangu wanafiki, ukimpigia simu anakuwa hapokei tofauti na mwanzo alikuwa hata akikuta missed call, anakupigia yeye. Sasa ukiona hivyo, basi unaanza kumuuliza kama kuna utata wowote, baada ya muda unakuta kuna kitu ulimkwaza na akakubali kukwazi kweli. Mengine manaume kabisa sijui ndo Manaume suruali niini. Huu mimi huwa nauuta ujinga sana.
 
kabla sijachangia humu nitafurahi
nikiwa kidoogo well informed.....
anyone please pm me.....
We nae unapenda PM...
Wakati tukiwa leave kuna thread ilianzishwa humu na member alijiita Lipualipua akisema AshaDii kafariki. Watu walipoanza kushangaa na kumuuliza source akajibu: hivi mnadhani yeye sio mtu kama nyinyi? yeye hawezi kufa?
Thread ikafungwa na MODs, Kaizer akaanzisha counter-thread ya kusema kua AshaDii ni mzima na anatuma salam from where she is. Aliporudi mwenyewe alianzisha thread pia ya kusema she is very sad anaweza kuzingishiwa kifo.
The main ideas zilizo changiwa ni kwamba lipualipua anamchukia AshaDii na nakumbuka Lizzy aliuliza itakuaje wamchukie wakati hawamjui, wanamchukia kwa kipi?
Sasa naona hilo swali halikupata jibu kichwani mwake wala hajaona post inayo mrihisha katika kujibu hilo swali, ndio ameamua kulifungulia thread kabisa ili watu wanao wachukia fellow members (bila kuwajua outside JF) wajifungue, wajieleze.
 
We nae unapenda PM...
Wakati tukiwa leave kuna thread ilianzishwa humu na member alijiita Lipualipua akisema AshaDii kafariki. Watu walipoanza kushangaa na kumuuliza source akajibu: hivi mnadhani yeye sio mtu kama nyinyi? yeye hawezi kufa?
Thread ikafungwa na MODs, Kaizer akaanzisha counter-thread ya kusema kua AshaDii ni mzima na anatuma salam from where she is. Aliporudi mwenyewe alianzisha thread pia ya kusema she is very sad anaweza kuzingishiwa kifo.
The main ideas zilizo changiwa i kwamba lipualipua anamchukia AshaDii na nakumbuka Lizzy aliuliza itakuaje wamchukie wakati hawamjui, wanamchukia kwa kipi?
Sasa naona hilo swali halikupata jibu kichwani mwake wala hajaona post inayo mrihisha katika kujibu hilo swali, ndio ameamua kulifungulia thread kabisa ili watu wanao wachukia fellow members (bila kuwajua outside JF) wajifungue, wajieleze.


nashkuru kwa maelezo yako
ajabu watu na roho zao na akili zao
i hope ASHADII hajakuwa discouraged kwa ujinga wa watu au mtu wa ovyo ovyo
 
Siamini macho yangu hee watu wana vipaji vya mipasho humu MMU.fungue band ya taarabu.Mwimbo wa kwanza uitwe "choko choko mchokoe pweza binadamu ...."KWA KHERINI ENDELEENI MI NILIKUWA NAPITA TU.
 
Nadhani tulikuwa na mawazo yaliotaka kufanana...

Madhara Ya Chuki, Uhasidi Na Uadui (Falsafa Binasfi)

....
Naweza kuuhita ugonjwa huu kwa jina la maradhi ya kimaadili yanayompata mtu, maradhi haya ya chuki na uadui ni miongoni mwa maafa makubwa ya ufanisi na utulivu wa nafsi, yanaotokana na tabia mbaya ya hasira ya kushindwa katika medani ya kutafuta maisha au kushindwa kwako katika kile unachokitafuta katika kuboresha maisha yako, kiasi ya kuvuruga mtiririko wa fikra chanya na kupelekea kuvuruga uthabiti wa kiroho wa mtu. Huenda ni kutokana na sababu Fulani fulani za kukosea hapa na pale au kujaribu hiki na kile.

Kushindwa uku umfanya muhusika kupata hamaki na kujichukia na kupelekea kuwachukia wale waliofanikiwa kimaisha, kiasi ya kwamba kwa wale wasio na uvumilivu uamua kuwasingizia mambo haya na yale wale wanao waona kuwa ni maadui zao. Kiasi ya kusahau kuwa kufanikiwa au kuto fanikia ni mipango yako tu kutokuwa mizuri au kwa kutaka kutumia njia ambazo si za kimaadili, kama vile wizi au utapeli.


Moyo wa kuweka kisasi na kukomoana ni dalili ya unyonge wa nafsi. Na ni ishara ya maudhi na maonevu aliyoyapata mtu udogoni mwake aidha shuleni, mtaani kwake alipokuwa akiishi au aliyo yaona katika familia au wazazi wake. Mambo haya huweka athari mbaya na kinyongo katika moyo wake kwa kadiri kwamba nafsi yake husumbuliwa na aina moja ya chuki iliyotia fora. Kwa ufupi, kukomoana na kulipiza kisasi ni njia mojawapo wanayoitumia wenye kujihisi duni ili kufidia kushindwa kwao. Hutumia visingizio mbalimbali kuwakera wengine na utenda uhalifu wa hatari kulipiza kisasi kwa yale yaliomsibu alipokuwa mdogo, akitafuta kujifariji ukubwani kwa masahibu ya utotoni. Watu wa aina hii mara nyingi wanakuwa wamelelewa katika koo duni na wakapata vyeo au kusafiri nchi za mbali na kujiona kuwa wao ni bora, hivyo kupelekea kuwa wajeuri. Kwa njia hii hutaka kufidia uduni waliolelewa nao katika koo hizo. Na ujiona ni watu bora kuliko wengine, na hutaka kutumia uhasidi na ubinafsi wao kujitangazia ubora wao. Wengi wetu tunaweza kuwatambua watu wa aina hii miongoni mwetu...

souce: [SUB]Madhara Ya Chuki, Uhasidi Na Uadui (Falsafa Binasfi)[/SUB]
 
Nadhani itakua wiki moja imepita sasa tangu niulize kwenye thread fulani kama inawezekana mtu akapata adui hapa JF kwasababu binafsi bado sijaona uwezekano wa kumchukia mtu ambae sijui yukoje in reality na wala hajanifanyia lolote baya hapa mtandaoni.

Naelewa kwamba huku mitaani hua inatokea mtu , hata ndugu yako au rafiki akawa anakuchukia bila sababu maalum.Yani unakuwa hujamfanyia lolote baya, tena inawezekana ukawa mtu wa kumsupport na kumsaidia sana.Chuki ya namna hii naamini mara nyingi hua inasababishwa na wivu,yani yule mwenye chuki anatamani alichonacho mwenzake kingekua chake (pesa,mpenzi mzuri, familia inayompenda, marafiki wanaomjali, kazi nzuri n.k). Na mara nyingi hali hii hua inapelekea hao wenye wivu kutafuta namna ya kumvurugia huyo mwingine hata kwa kusambaza maneno yasiyo na ukweli.Ila sasa naomba kuuliza, sehemu kama hapa JF, sehenu ambayo wengi hatufahamiani inakuaje mtu anakua na chuki tena kali na mwenzake? Tatizo ni nini? LIKE anazopokea? Thread anazoandika? Watu anaointeract nao jamvini? Muda anaospend online? Namna anayoandika? Mambo anayoonekana kujua? Kama jibu ni moja ya hayo hapo juu nini kinakusumbua wakati hatujuani hivyo na wewe unaweza ukatumia hata google kuandika kitu kizuri kikakubalika bila yeyote kujua hazikua juhudi zako mwenyewe?
Jumanne njema.
Asante Lizzy Kwa kututakia Jumanne njema, na mimi nakutakia Jumma tano njema!
Nilisubiri mkalale wote ndio nije nijibu ili msinikatikizi katika 'reasoned argument' yangu. :)
Nimesoma maswali yako na nadhani jibu sio rahisi kama unavo fikiria. JS ni community with its dynamics. Na moja ya hizo dynamics ni POWER. Sababu namna za ku-interact ziko limited, tunakua pia limited katika namna yetu ya kutumia na kuonesha power. Huhwezi tumia powe unayo nje ya JF sababu it is not relevant here (how do we know?).
vitu vinavyo leta power katika community ya JF ni vitu tunavyo weza kuona: avatars, ID,Likes, Posts, reputation power, the ability to get people to post after you, to quote you, to talk about you etc. Kuna ambavyo tunaweza kubadilisha (avatar, started threads, started posts, likes given etc) na vingine hatuwezi (likes received, pages of threads started, visit on your home page etc)
How is that a power? sababu ni nyingi ila c
ha msingi ni kwamba people need to differenciate themselves. Hakuna member anae taka kua kama member mngine, kila mtu ni separate individual. na kila mtu anataka kua as good as possible. na vitu vinakufanya kua good ni hivyo vinavyo onekana. Ukisha weka hiyo kua 'good' na kua 'bad', tayari umeleta kua 'better' na kua 'worse'.
Kwangu mimi ku-interact na member (on post and PM) ni muhimu. Kwako wewe kuchangia thread kwa maneno ya busara ni muhimu. kwa mngine kua na avatar nzuri ni muhimu, or kupata likes etc. kwa wengi hapa ni mchanganyiko wa vitu vingi. na hivyo vitu ndio vinamfanya mtu kua better au worse "than...". mimi najicompare na mi mwenyewe. I am better than I was when I joined, au I am worse than I was in my last post etc. ila inaonekana kuna watu wanajicompare na wengine humu ndani ya hii community yetu ya JF: I have started less post than Lizzy, my avatar receives less complement that Afrodenzi, my personality is not as sexy as preta au my political knoweledge is nowhere compared to faiza foxy.
Kwa vile sisi ni binadamu tunakua na reaction tatu: indifference, kufurahia au kuchukia (this late hasa kwa vitu hatuwezi badilisha)
Sasa in the case ulio toa tunaweza kuangalia: what is AshaDii power? among other tunaweza kumention kua ameanzisha threads nyingi, na nyingi zilipendwa, anajua ku-keep attention ya members kwenye threads anazo changia, posts zake zina pendwa na wengi, and last but not least, she 'is seen to be' a key figure in MMU na Chit Chat sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuchangia na kubadilisha mweliekeo wa majadiliano. so in that regard AshaDii holds some form of JF.
From there we have some hints on the mobiles of our 'suspect', kazi kwako kujenga "profile' na ikibidi jenga a 'sketch'...
 
Hivi kweli unamchukia mwenzako, rohoni unaishi kwa amani kweli? Dah!! Kwa hiyo unapomuona au ukiona tu post yake, tayari we roho inakufinya?? Mtakufa siku si zenu!!!
 
Back
Top Bottom