Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?

Sio mhubiri ila ni mwalimu na wala sio mchungaji hana Kanisa lake.
Hutakujamsikia anahubiri mambo ya madhehebu, anafundisha uchumi katika Kanisa na kufanikiwa katika maombi yako. Ni mchumi kwa taaluma yakle na anaishi Arusha, anazungukia miji mingi tu hapa nchini kama uko DSM vizia akija anapendelea kufanyia mafundisho yake Kinondoni jirani na Open University, viwanja vya Hananasifu?

Leka
 
Of course yeye na Lowasa ni family friends. Enzi zake aliwahi kumchukua kwenye delegation yake kwenda Marekani. Mnataka Lowasa awaombe radhi kwa kosa lipi ilihali aliishwaachieni Uwaziri Mkuu wenu.
 
Mwalimu huyooooooooooooo Dar kuanzia tarehe 7 - 14 March 2010, jamani jiandaeni kwa maombi yenu, watu wampokee Yesu na Mungu amlinde yeye na kamati yake. Atakuwa Kinondoni, uwanja wa Biafra, karibu na OUT, Don't miss. Barikiweni
 
Mungu amitieni nguvu, ni faraja kujua kwamba kuna kundi kubwa tu la watu wenye hofu ya Mungu. Tuendelee kuombeana sisi kwa sisi na nchi kwa ujumla, tuache kunyoosheana vidole, sababu hakuna mwenye haki hata mmoja kati yetu ni maneno yake Mungu. Mbarikiwe saana naomba Mungu wa Bwana Wangu Yesu Kristo awabariki munoo
 
Christopher Mwakasege is a true servant of God. Mtawatambua kwa matunda yao. Matunda yake kwa muonekano na kwa malisho ni upendo, uvumilivu, utu wema, upole, kiasi, fadhili, unyenyekevu,amani na uaminifu.
Sasa kama haya yote tunayaona kwa mtu si ndio tunda la roho hilo, kwani tangu lini mbuyu ukazaa maembe?

Unayesema wewe siyo Mungu!Acha bwana!!!!!!
 
Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.

Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.
Mungu yupo kila mahali na anasikia kwa lugha yoyote utakayoitumia. lakini kwenda Israel sio kosa maana ni hija ya hiari. Kama mtu anaamini kwamba atasikilizwa zaidi na Mungu wake akienda kukanyaga ardhi iliyokanyagwa na Bwana Yesu na Watakatifu wa kale, ruksa. Maana Mungu anaangalia moyo na wala hababaishwi na sura ya mtu.

Mwakasege anakuwa na semina za mara kwa mara Dar es Salaam na zinapokaribia hutolewa matangazo makanisani. Hudhuria kimojawapo cha vipindi vyake, hata ukitaka kumtegea kama atatereza kuisema vibaya serikali utamaliza mpaka dakika za ziada wala hutomsikia hivyo. Anayasema mabaya bila kumsema mtu au kundi la watu moja kwa moja. Yeye sio mhubiri bali ni mfundishaji. Uchumi katika Imani na Maombi yenye kuleta tija ndio agenda zake kuu mara nyingi.
 
Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.

Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.

Dah! Na huko Israel ndipo alimpeleka Sedekia yule mwimbaji n akafia huko huko....
 
Duh nimefurahi jinsi watu walivyomueleza Mwalimu Mwakasege next time nitaomba mnipe wasifu wa Nabii na Mtume Mwingira, nitapenda sana kumjua huyu mtu kiundani. manake kamkamata mke wangu na kanisa lake.
 
Kwa walio ughaibuni- USA na UK, Mwl Mwakasege huwa anafanya ziara za kiutumishi huko na kuendesha semina za neno la Mungu kwa Watanzania waluiopo nchi hizo. Keep followingf up via www.mwakasege.org
 
Mwishoni mwa mwaka 2000s alikorofishana na aliyekuwa katibu mkuu wa KKKT Bwana Mwegoha akaacha kazi na kuanzisha NGO yake inayojishulisha na masuala ya mipango [uchumi].
kazi ipo!
 
Hakika Tanzania inaendelea kujengwa na wenye mioyo migumu wachache na kuliwa na wenye meno wachache wakati wengi wa watanzania wameduwaa wakiwa hawaelewi kinachotokea. Utamaduni wa kazi na uthamani wake kujenga ubinadamu umepotezwa. Jawabu tufanye kazi n a kumuweka Mungu mbele.Hatuhitaji watalaam kuhusu hili kwani sote tunajua.
Fafanua please hueleweki
 
Ni mwalimu mzuri.
Nilipookoka alikuwa mwalimu wangu mzuri wa kwanza kwa njia ya kanda. Mafundisho yake yalinijenga sana na kunipa mwanzo mzuri sana.
sijawahi kumuona physicaly na bado sijapata bahati kuhudhuria moja ya semina zake labda namuona katika tv.
 
Da,
Bora nimpeleke kwa Joti wa ze comedy kuliko kwa hao jamaa wajasiriamali

Ahahaaaa! Great thinkers bana. Ndo maana nawakubali sana. Mpeleke mgonjwa wako hospital mkuu.
Huyu mwakasege mwenyewe semina zake hadi ulipie kiingilio. Style mpya tu ameamua kuwa mgombea binafsi afungamani na upande wowpte. Sttategies bana.
 
Duh nimefurahi jinsi watu walivyomueleza Mwalimu Mwakasege next time nitaomba mnipe wasifu wa Nabii na Mtume Mwingira, nitapenda sana kumjua huyu mtu kiundani. manake kamkamata mke wangu na kanisa lake.

Pole sana mkuu! Kuna mahali kwenye biblia wanasema tuwaheshimu wapakwa mafuta wa bwana. Naogopa kuwadis hawa wanaojiita walimu, manabii na what have you lakini neno moja linatosha......ni wafanyabiashara wahuni.
 
Ni mwalimu mzuri.
Nilipookoka alikuwa mwalimu wangu mzuri wa kwanza kwa njia ya kanda. Mafundisho yake yalinijenga sana na kunipa mwanzo mzuri sana.
sijawahi kumuona physicaly na bado sijapata bahati kuhudhuria moja ya semina zake labda namuona katika tv.
mhh......nasikia mna kanisa lenu pale Ubungo mnafufua misukule.....
 
Back
Top Bottom