ni mtu mwadilifu sana huyu.
ana heshima kwa waumini na serikali kwa ujumla.
wasiomjua kabisa ndio wanaosema hovyo juu yake.
asiyejua maana haambiwi maana!
naomba web yake, kama unaijua, kuna wakati nilikua naitumia lakini ikafika mahali ikagoma kufungua....
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?
Heshima Kwako Bujibuji,
Ninamfahamu Mwl,Mwakasege tangu mwaka 1980s wakati akifanya kazi halmashauri ya wilaya ya Arumeru kama afisa mipango.Sina hakika ila mwanzo mwa miaka ya 1990s aliacha kazi serekalini akajiunga na KKKT makao makuu kama katibu mipango na miradi.Wakati wote huo tayari alikuwa mhubiri mzuri sana akitumika zaidi New life crusade.Mwishoni mwa mwaka 2000s alikorofishana na aliyekuwa katibu mkuu wa KKKT Bwana Mwegoha akaacha kazi na kuanzisha NGO yake inayojishulisha na masuala ya mipango [uchumi].Pia aliachana na New Life Crusade akaanzisha taasisi yake inayojishuhulisha na masuala ya dini sina uhakika sana na jina la hiyo taasisi yake nadhani inaitwa MANA.
Mwl C Mwakasege hapendi kuitwa Nabii au Mtume kama wanavyopenda kuitwa baadhi ya watumishi wa mungu,mara nyingi nimemsikia akijiita mwalimu.Taasisi yake haina mipaka ya madhehebu wala maubiri yake hayafungamani na madhehebu kama ilivyo kwa akina Mzee wa upako,Mchg Dr G lwakatare au Askofu Mkuu Z Kakobe.
Amen.Jamani
nimefurahiswa kuona mnavyomsifia makwasege ombi langu
tusiwe tu wahudhuriaji wa semina zake,,,tufanye yale anayoubiri
tusiwe watu wa kusiia;mwakasege ameokoa roho yake nafurahi ata mungu ameona maandishi hya je wewe roho yako itakuwa wapi;badilika ishi na neno la mungu achana na zinaa;dhambi,ulevi,uasherati,ufiraji na mengine kama hayo
ukifnya hayo utakuwa unampongeza zaidi mwakasege huku malaika wa mbinguni wakishangilia;acha kubaki mshangiliaji ama mkosoaji wa watumishi wa mungu anza kufurahia matunda yao kwa kufwata yale mungu anayowatumia kukuabilisha wewe hapo utakuwa unamfurahisa mungu na mwakasege kwa ujumla
mungu akusaidie hili in jesus name
ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?
Uffff!
Unajua nilipoiona hii thread niliogopa kuifungua, nikasema haya na huyu naye anashambuliwa kwa lipi tena!. Mwisho nikajipa moyo nikasema ngoja tu nifungue nione, yaani nimefurahi kuona kumbe sivyo. Kumbe watu wa Mungu mmeona jinsi mtumishi wa Mungu alivyojitoa kuitenda kazi ya Bwana, Mungu awabariki sana wote kwa comment zenu. Niliingiwa na wasiwasi sababu thread zimekuwa nyingi za kuwasema watumishi wa Mungu mpaka nikasema isije ikawa JF sasa ikatumika kuwakatisha tamaa watumishi wa Mungu. NIMEFURAHI SANA, MBARIKIWE!
Kinachofurahisha kuhusu huyu jamaa ni kwamba jumapili anaingia kanisani kama waumini wengine tu.
HAJIKWEZI KWA HALI YOYOTE, NA ANAKUWA MYENYEKEVU SANA KWA WACHUNGAJI.
wANAJARIBU KUMPA VITI VYA MBEELE KANISANI, japo yeye asingependa iwe hivyo.
Anasikiliza kwa utulivu mahubiri ya wachungaji wake kama vile hajui kitu.!
Mungu mbariki sana mtu huyu.
Nchi ya Tanzania inahitaji sana watu wa namna ya mtu huyu, maana ndo wanaosababisha nchi hii angalau iwe na amani iliyopo, na ana uwezo wa kusoma alama za nyakati za kiuchumi wa taifa hili na za kiroho.
Mungu mbariki mtu huyu tena.
Mkuu,Ni mtu mwadilifu sana huyu.
Ana heshima kwa waumini na serikali kwa ujumla.
Wasiomjua kabisa ndio wanaosema hovyo juu yake.
Asiyejua maana haambiwi maana!
Huyu si ndiye yule tapeli aliyesema Haiti wamepata maafa kwa sababu ya uchawi?
Na yeye tapeli mchawi tu.
Huyu si ndiye yule tapeli aliyesema Haiti wamepata maafa kwa sababu ya uchawi?
Na yeye tapeli mchawi tu.
Huyu si ndiye yule tapeli aliyesema Haiti wamepata maafa kwa sababu ya uchawi?
Na yeye tapeli mchawi tu.