Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

Heshima Kwako Bujibuji,

Ninamfahamu Mwl,Mwakasege tangu mwaka 1980s wakati akifanya kazi halmashauri ya wilaya ya Arumeru kama afisa mipango.Sina hakika ila mwanzo mwa miaka ya 1990s aliacha kazi serekalini akajiunga na KKKT makao makuu kama katibu mipango na miradi.Wakati wote huo tayari alikuwa mhubiri mzuri sana akitumika zaidi New life crusade.Mwishoni mwa mwaka 2000s alikorofishana na aliyekuwa katibu mkuu wa KKKT Bwana Mwegoha akaacha kazi na kuanzisha NGO yake inayojishulisha na masuala ya mipango [uchumi].Pia aliachana na New Life Crusade akaanzisha taasisi yake inayojishuhulisha na masuala ya dini sina uhakika sana na jina la hiyo taasisi yake nadhani inaitwa MANA.

Mwl C Mwakasege hapendi kuitwa Nabii au Mtume kama wanavyopenda kuitwa baadhi ya watumishi wa mungu,mara nyingi nimemsikia akijiita mwalimu.Taasisi yake haina mipaka ya madhehebu wala maubiri yake hayafungamani na madhehebu kama ilivyo kwa akina Mzee wa upako,Mchg Dr G lwakatare au Askofu Mkuu Z Kakobe.
 
Asante sana kiongozi.
Kuna ndugu yangu anahitaji maombi, je anapatikana wapi?

Arusha.

Ni maombi au kitu kingine? Mpeleke mgonjwa wako kwa kakobe au mzee wa hammer pale ubungo chaibora-nyumba ya ufufuo na uzima
 
Asante sana kiongozi.
Kuna ndugu yangu anahitaji maombi, je anapatikana wapi?

Asante mkuu unaweza kuwasiliana nao kwa kupitia ...

Christopher & Diana Mwakasege
P. O. Box 2166,
Arusha, TANZANIA.
Phone: +255-27-2504289
Fax: +255-27-2504289
Email: tasoet@nexusdigital.co.tz.

Natumaini nitakuwa nimekusaidia wewe na ndugu yako anaehitaji maombi.
 
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Mhubiri,
je kanisa lake liko wapi?

Christopher Mwakasege is a true servant of God. Mtawatambua kwa matunda yao. Matunda yake kwa muonekano na kwa malisho ni upendo, uvumilivu, utu wema, upole, kiasi, fadhili, unyenyekevu,amani na uaminifu.
Sasa kama haya yote tunayaona kwa mtu si ndio tunda la roho hilo, kwani tangu lini mbuyu ukazaa maembe?
 
Ngongo,
nimependa comment zako na jinsi ulivyojaribu kumwelezea Christopher Mwakasege. Kwa kweli ni mwalimu na siyo mchungaji hana kanisa na ameweka wazi kuwa yeye ni mwalimu na siyo mchungaji hivyo hahitaji kanisa. Mungu aendelee kumbariki...
 
Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.

Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.
 
Asante mkuu unaweza kuwasiliana nao kwa kupitia ...

Christopher & Diana Mwakasege
P. O. Box 2166,
Arusha, TANZANIA.
Phone: +255-27-2504289
Fax: +255-27-2504289
Email: tasoet@nexusdigital.co.tz.

Natumaini nitakuwa nimekusaidia wewe na ndugu yako anaehitaji maombi.

naomba web yake, kama unaijua, kuna wakati nilikua naitumia lakini ikafika mahali ikagoma kufungua....
 
Hakika Tanzania inaendelea kujengwa na wenye mioyo migumu wachache na kuliwa na wenye meno wachache wakati wengi wa watanzania wameduwaa wakiwa hawaelewi kinachotokea. Utamaduni wa kazi na uthamani wake kujenga ubinadamu umepotezwa. Jawabu tufanye kazi n a kumuweka Mungu mbele.Hatuhitaji watalaam kuhusu hili kwani sote tunajua.
 
Ni mwalimu mzuri sana. Kama alivyosema member hapo huu huwa hafungmani na mkanisa haya yanayojiita ya kiroho na wala halazimishi wanaopata huduma yake kulipa mapesa kibao. Huyu si mfanya biashara kama walivyo wengine, anafundisha habari zote hata za mafungu ya kumi na halazimishi muumini kumpelekea.

Anafundisha pia kwa kutumia taaluma yake ya uchumi, ni kwa namna gani utaweza kufanikiwa, yaani kuwa mjasiriamali na mfanyakazi productive.

Anafundisha kweli hasa masuala ya ndoa. Halazimishi ndoa zilizoshindikana bali anafundisha ukweli kuhusu ndoa hizo na kama kweli zilipata kibali cha Mungu kufungwa au wana ndoa walilazimishana kuona kutokana na cirumstances na mwsihowe are incompartible??? Keep it up mwalimu Christopher and Diana Mwakasege.
 
Heshima kwako Maane,

Ni kweli kabisa uliyosema jamaa ni kichwa hasa ukibahatika kuhudhuria semina zinazohusu ndoa,mara nyingi hizi semina ni kwa wanandoa tu utakubali Mwakasege kajaliwa kipaji na mwenyezi mungu.Antoa somo kiasi kwamba semina ikimalizika mnajiona kama mmefunga ndoa jana.
 
AMINA. Kweli Mwakasege ana karama ya kuitwa Mwalimu.
 
Back
Top Bottom